Mbowe amvaa Spika Makinda

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]JUMATATU, APRILI 16, 2012 05:42 NA BAKARI KIMWANGA, DAR ES SALAAM



freeman-mbowe1.jpg
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe
anna%20makinda.jpg
Spika wa Bunge, Anna Makinda
Amlalamikia uchaguzi wa ubunge Afrika Mashariki
Atishia Chadema kwenda mahakamani

Mrema alia wapinzani kupewa kiti kimoja

WAKATI Bunge likitarajia kuwachagua wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kesho, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe amemvaa Spika wa Bunge, Anne Makinda akimtaka atumie busara katika suala zima la mgawanyo wa viti hivyo.

Mbali na hatua hiyo, Mbowe amesema kama haki haitatendeka, Chadema kitakwenda katika Mahakama ya Afrika Mashariki, kudai haki zaidi.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mbowe alimtaka Spika Makinda kutumia busara katika jambo hilo, kuliko kutumia ubabe ambao utakuwa hauna tija na maslahi kwa taifa.

Alisema ni vema ikaeleweka, uwakilishi katika Bunge la Afrika Mashariki huendana sawa na vyama vilivyo na wabunge na si vinginevyo.

“Tuamini jambo hili ni la kutumia busara na imani yangu, kama kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, tutalizungumza kupitia vikao vyetu vya ndani ili kufikia muafaka. Itakuwa hakuna tija kama waking’ang’ania kufanya uchaguzi huu, huku vyama vya upinzani vikipewa kiti kimoja cha uwakilishi.

“Hii si haki hasa kwa nchi kama Tanzania ambayo viongozi wake wa taifa, wamekuwa wakitumia muda mwingi kuhubiri kukua kwa demokrasia, lakini yanapofika masuala ya kitaifa, wanashindwa kutoa haki.

“Ikiwa wataendelea na uchaguzi huu, bila kulipatia ufumbuzi sakata hili, basi kwa uongozi wetu CHADEMA, tutatumia vyombo vya nje ikiwemo Mahakama ya Afrika Mashariki kudai haki hii ya msingi vya vyama vyetu vya upinzani.

“Pale Uganda, Chama cha DP kiling’ang’ania jambo hili na kufanikiwa kwenda kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki na kufungua kesi, siku ya mwisho kikashinda, sasa iweje sisi tufumbie macho,

MREMA NAYE AIBUKA

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Dk. Agustine Mrema, alisema sasa umefika wakati kwa Spika Makinda, kutumia nafasi yake walau kutoa nafsi mbili kwa kambi ya upinzani, kuliko kuwa na nafasi moja kama ilivyo sasa.

“Hili suala limefikishwa kwake Spika, nianachojua Mama Makinda ni mtu ambaye anaamini katika demokrasia, acha tusubiri busara zake katika hili kwanza. Ila kwa maoni yangu ingekuwa vizuri kambi ya upinzani, ikapewa nafasi mbili, badala ya moja kama ilivyo sasa.

“Hili linawezekana, ila ninaomba tumuachie yeye kwa sababu ni kiongozi imara na anayezingatia demokrasia ndani na nje ya Bunge letu,” alisema Mrema.

Wiki iliyopita,Chadema ilitangaza kupinga uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutokana na mchakato unaoendelea kutokuwa huru na haki.

Kutokana na hali hiyo, chama hicho kilimtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda, Katibu wake, Dk. Kashilillah na Serikali kuchukua hatua za haraka kurekebisha kasoro zilizojitokeza, ili kuhakikisha uchaguzi huo unawezesha wabunge kupatikana kidemokrasia na kwa kuzingatia maslahi ya umma.

Katika uchaguzi huo, CCM ina nafasi ya wagombea nane na vyama vya upinzani mgombea mmoja.

CHADEMA kilidai kulingana na idadi ya wabunge wa CCM kuwa 258, chama hicho kilistahili kupata viti visivyozidi saba, lakini wamepewa viti nane, huku vyama vya upinzani kwa ujumla wake vimepewa kiti kimoja.

CHADEMA, ilisema kwa kuzingatia ibara ya 50 ya mkataba wa Afrika Mashariki na uwakilishi wa vyama vyenye wabunge, CCM ilistahili kupata viti visivyoziti saba, Chadema chenye wabunge 48, kilistajili kupata kiti kimoja na chama cha CUF chenye wabunge 36 kilistahili kupata kiti kimoja.


….kule kuna vyama kama hapa Tanzania, walipunjwa viti kama tunavyofanyiwa, ninapenda ieleweke lengo si kwenda mahakamani, Spika pamoja na katibu wake, watatumia busara ili kulimaliza jambo hili bila kuadhirisha uchaguzi baada ya kuonekana una doa. Ni vema walau kati ya viti tisa, tungepewa viwili kutokana na uwiano wa vyama vyenye wabunge ili kuleta usawa na taswira sahihi,” alisema Mbowe.

 
Asante mkuu, kuna thread inaendelea kuhusu hili jambo but naamini Spika hana washauri wazuri au wanamtumia kupoteza umaarufu wa SSM
 
Ninyi mnajua maana ya Speaker? Maanake, hasa kwa huyu Bi. Kiroboto, ni "Msemaji". Sasa Bi. Kiroboto ni Msemaji wa Chama cha Magamba, Majambazi na Mafisadi waliosahau Mapinduzi! Anawatumikia wale ambao dakika za mwisho walitaka "Msemaji" wao safari hii awe Mwanamke, hivyo kamanda wao mmoja na Gamba 1 wakashindwa kuipata jinsia ya kike kwa wakati wakajikuta wametupwa nje!

Hao ndio Nyundo na Jembe bwana. Kaaaaaaaaaaaaaaaaaaazi Kweli Kweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mwaka huu kweli jamaa hawatapumua kabisa. Kila sehemu walishaharibu na jamaa wanashituka na kujenga kwa kasi.
 
lakini jamani sheria inasemaje kwanini utaratibu mzima ulioundwa upatikanaji wabunge ukoje? kwa sababu inaonekana kama chadema inamuomba huyu mama atumie hiyari yake tu inakuwaje kwani sheria zinasemaje? kama sheria iko upande wao basi kuna haja ya kuchukua njia waliochukua wenzao moja kwa moja kabla usiku haujaingia.
 
Hivi huyu mama aliolewa? Au alioa yeye? Sijapata kuona mama limekaa kikatili kiasi hichi. Yani hana mshipa wa aibu
 
Kakaa Sana Madarakani tangu Mzee Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete angalipa picha yake chini kwenye mkutano na Papa na Rais Mwinyi

p5.jpg
 
Baniani mbaya ila kiatu chake kizuri. Na ubaya wake wote, amekula kuku zaidi kwenye maisha.

Nafikiri hili kwa hapa si muhimu. Kwani u-HANDSOME wa Kikwete umetusaidia nini?
Huyu mama nikiiona sura yake najisikia kuchefuka!
 
Hivi huyu mama aliolewa? Au alioa yeye? Sijapata kuona mama limekaa kikatili kiasi hichi. Yani hana mshipa wa aibu

Kaka kiona unan'chekesha sana bwana kama hajaolewa yatuhusu nini tena hayo? sisi tunataka afanye kazi iliyomuweka pale kwa mujibu wa sheria haki na nidhamu, aolewe asiolewe hiyo ni juu yake na ndugu zake jamii haina manufaa na ndoa yake hiyo ni personal issue
 
Huyu mama anashindwa kujua anaishi karne tofauti na alipokulia. Hatuangalii nani kasema ila unasema nini. Mama jiuzulu tuu tukupongeze!
 
Asante mkuu, kuna thread inaendelea kuhusu hili jambo but naamini Spika hana washauri wazuri au wanamtumia kupoteza umaarufu wa SSM

Spika hashauriki mkuu............ Sio kwenye siasa tu, ni kwenye kila kitu!!!
 
Back
Top Bottom