Mbowe amuumba Mkama kwenye msiba wa Makani baada ya kuongea UWONGO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe amuumba Mkama kwenye msiba wa Makani baada ya kuongea UWONGO

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jun 12, 2012.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,168
  Trophy Points: 280
  Kwenye shughuli ya kuuaga mwili wa Mzee Bob Makani, Mbowe ameumuaibisha sana katibu wa CCM bw. Mkama kutokana na kuongea maneno ya UWONGO.
  Kwenye kadamnasi hiyo, Mkama aliudanganya umma uliofurika katika viwanja vya Karimjee kuwa, eti Mzee Bob Makani alikuwa ni muasisi pekee wa Chadema ambaye hajatokea kanda ya kaskazini.

  Mbowe ilipofika zamu yake, akaorodhesha majina ya waasisi wote wa Chadema na kuelezea mikoa waliyotoka.
  Kitendo hicho kilimvua kabisa nguo bw. Mkama ambaye dhahiri alikuwa akitaka kuutumia msiba mzito wa mwasisi wa Chadema kujijengea jina na umaarufu.
  Aibu hiyo ilishuhudiwa na mwenyekiti wa CCM bw. Kikwete.
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mukama naye hana akili kama wenzake? amba bwana inatakiwa watoke tu hakuna namna ya kuwabeba.
   
 3. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  CCM kweli inapigwa bao kila iendako
   
 4. D

  Dereck Tito Senior Member

  #4
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Asante kamanda!! Hii inadhihirisha Ushindi na kujiamini kuliko ndani ya CDM. Hakuna mambo ya Yes! Yes! hapa. Ila kwao kumebakia nini? AIBU! AIBU! AIBU! Katika kila liwatokalo. CCM sasa basi, someni nyakati!!!
   
 5. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Mkama kichwani kamasi tupu,Dr.slaa na mbowe waliwai kumwambia kuwa"MKAMA HUKUWAI KUGOMBEA HATA UDIWANI UONE SIASA ZILIVYO HASITHUBUTU KUSHINDANA NA MAKAMNDA" asivyo akilii na kujiashau kama kuku kajiumbua tena yeye,m/kiti wake na magamba wenzake wa ccm kwa akili kichwani za kushindwa kusoma alama za nyakati na aina ya maadui anao pambana nao kuwa sio saizi yake na hawezi kujenga na kuwashinda.
  My take:mkama aachane na siasa kwani imethibitika kuwa hawezi hasa kujenga hoja ila kwa kuwa ccm hupenda vilaza na wababaishaji kwao wanamuona almas kumbe wananchi tunamwona KIMBA.
   
 6. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu bujibuji......heshima kwako....
  Pengine ungetoa hiyo orodha ili tupate nondo za kuwashughulikia wanaotaka kuaminisha watu vinginevyo kinyume cha ukweli ulivyo....

  Pili title ilinistua kidogo....AMUUMBA...Nilidhani kageuka Mungu.....Kumbe amuumbua....
   
 7. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  buji buji mbona kaeleweka mkuu,soma historia ya chadema ni kama TANU na harakati za kudai uhuru ilikuwa na waasisi kutoka pande zote kama akina bibi titi wa dsm,nyerere wa msm,simba wa vita(kawawa) morogoro,kingunge ngombare mwilu huyu hana dini na sijui hanatokea wapi lakini kwa upande wa chadema kuna mtei,hayati bob makami na wengineo na zaidi watu wamezidi kujiunga wenye na wasio na dini kutoka pande mbalimbali za tz kama kina baregu(kagera),zito.lisu,na wengine unao wajua tatizo la na ccm ni ni ukosefu wa akili na ufikili duni wa kutaka kuendeleza siasa za kizamani za kipropaganda na kuwatisha watu kuwa wa wapinzani wakichukua nchi vita vitatokea na upumbavu mengine yalio vichwani mwao, wasijue vijana tumesoma na tunajua DHAHABU IPI NA MAVI YAPI lakini wasivyo akili wanataka kutukanyagisha mavi kwa kila namna wanayoijua wao lakini wanashindwa wanabaki na aibu wao waizi,mafisadi,wauza twiga,wazulumaji wa haki za raia na manyanyaso mengine hayo ndio watu tunataka kumuona mkama akiyaongelea la sivyo tutaendelea kumwona huyu mzee na ccm yote hawana akili hata kidogo watu tumechoka na tumepinda hatuambiwi hatusikii lolote juu ya chadema big up mwenyekiti wetu mbowe.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mukama awatibua CHADEMA

  • MBOWE AKEREKA, AMJIBU KWA VIELELEZO

  KATIKA kile kilichoonekana kama vijembe vya kisiasa kuutawala msiba wa muasisi wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Bob Makani, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, jana alijikuta katika wakati mgumu kutokana na kauli yake kupingwa vikali na Freeman Mbowe.
  Mukama wakati akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya chama chake katika viwanja vya Karimjee zilikofanyika shughuli za kuuaga mwili wa marehemu, alimsifu Makani akisema alikuwa ni Katibu Mkuu wa Kwanza wa CHADEMA kutoka nje ya kanda ya kaskazini kati ya waasisi wenzake tisa. Mbali na sifa nyingi alizommwagia marehemu, Mukama pia alisema CHADEMA wanatakiwa kuweka kumbukumbu hiyo kwa kuwa alikuwa ni mtu shupavu asiyependa kuongea wala kuhubiri kwa muda mrefu na asiyekumbatia udini, ukabila na ukanda.
  Hata hivyo, wakati Mukama akieleza hayo, viongozi wengi wa CHADEMA walionekana kushangazwa na kauli ile ambapo Mwenyekiti wa chama hicho, Mbowe, katika salamu zake alitumia mwanya huo kumjibu kwa vielelezo.

  Mbowe
  Mbowe alisema kuwa kitendo cha kusema kuwa CHADEMA kiliasisiwa na watu tisa kutoka eneo moja la kanda ya kaskazini ni uchafuzi wa kihistoria ndani ya chama hicho. Katika kuonesha kukerwa na kauli hiyo, Mbowe alilazimika kuwataja waasisi na mikoa yao kuwa ni


  • Edwin Mtei (Arusha),
  • Makani (Shinyanga),
  • Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa),
  • Edward Barongo (Kagera),
  • Mary Kabigi (Mbeya),
  • Menrad Mtungi (Kagera),
  • Costa Shinganya (Kigoma),
  • Evalist Maembe (Morogoro) na
  • Steven Wassira (Mara).


  "Mimi wakati huo nilikuwa mdogo na shughuli zangu zilikuwa ni kuandaa vikao na mikakati ndani ya chama. Nashangaa sana wakati nakumbuka historia ya chama hiki, hivyo watu wasijaribu kuipotosha," alisema Mbowe.


  Mbowe pia aligusia suala zima la uanzishwaji wa mchakato wa Katiba mpya akisema ni lazima kufanyike na marekebisho ya mfumo wa kisheria ili kuwapa nafasi wenye uwezo kuingia bungeni na kutoa michango ya maendeleo kwa jamii. Alisema mwaka 1995, 2000 na 2005 Makani aligombea ubunge Shinyanga Mjini akashindwa, hivyo ni vema watu kama hao wenye mchango mkubwa wakaingizwa bungeni kwa ajili ya kuleta changamoto mbalimbali.


  Rais Kikwete amlilia

  Rais Jakaya Kikwete naye alielezea kuhuzunishwa kwake na msiba huo na kusema kuwa Bob Makani alikuwa ni mtu muhimu na msaada mkubwa katika michango yake aliyowahi kuitoa katika kukuza uchumi wa nchi. "Nilisikia taarifa za msiba ambao ulinihuzunisha na kushtuka sana nikajaribu kumpigia simu Mwenyekiti wa Chama, Mbowe, lakini hakupatikana kwa kuwa alikuwa katika shughuli kubwa huko Ruangwa, nikamtumia ujumbe mfupi na baada ya kuupokea akanipigia na mimi nilikuwa katika shughuli sikupatikana, hivyo nikampigia tena baadaye ndipo tukazungumza," alisema Kikwete. Rais Kikwete alisema kuwa ni vema kuhuzunika kwamba tumepoteza mtu muhimu lakini pia iendane sambamba na kusherehekea na kuyaenzi mambo yake mazuri ambayo ameyafanya wakati wa uhai wake.

  Prof. Lipumba akumbusha enzi

  Kwa niaba ya vyama vya upinzani, Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba, alimwelezea Makani kuwa alikuwa mtu mzuri na kwamba CHADEMA inatakiwa kuiga mfano wake wa kuunganisha watu. Alisema alikuwa ni mwana mageuzi aliyeasisi harakati za mabadiliko ya Katiba na kusema alipata suluba pamoja naye katika mapambano hayo. Pia alikumbushia enzi zao za shule akisema Makani alikuwa na akili nyingi darasani. Muasisi wa CHADEMA ambaye aliwahi kuwa Gavana wa Benki Kuu na Mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho, Erdwin Mtei, alimtaka Makani kuwa alikuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu, na ameeleza masikitiko yake ya kuondokewa na mwenzake.

  Mtei
  Mtei alisema Makani kwa nafasi yake katika BoT alikuwa ni mtu aliyejali maslahi ya nchi na pia mwepesi wa kutoa taarifa za fedha.

  Dr. Slaa
  Akisoma wasifu wa marehemu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa alisema walifaidi utawala wa sheria na aina ya uongozi wa Makani kutokana na kuwa mwanasheria. Alisema Makani ni mfano wa kuigwa kwa kuwa alikuwa ni mtu wa watu aliyekuwa na kipaji cha kuelewa wananchi ambapo urefu wake uliweza kuonekana kila mahali alipoenda sambamba na ucheshi wake.


  • Asema kuwa Makani alizaliwa mwaka 1936 katika Hospitali ya Kolandoto, Shinyanga na kusoma shule ya msingi Ibadakuli mkoani humo.
  • Alifauru sekondari na kupelekwa Chuo Kikuu cha Makerere, ambako alifuzu na kupata Shahada ya Kwanza katika Uchumi (BA Economics).
  • Mwaka wa 1961 alikwenda Chuo Kikuu cha Liverpool, nchini Uingereza na 1965 akatunukiwa Shahada ya Sheria (LLB) alirudi nchini ambapo aliajiriwa na serikali kama Mwanasheria wa Serikali kwa muda mfupi kabla hajapandishwa cheo na kuwa Exchange Control Manager wa Benki Kuu.
  • Makani ni mwasisi wa CHADEMA mwenye kadi namba tatu baada ya Edwin Mtei, na marehemu Brown Ngwilulupi. Mwaka wa 1998 akachaguliwa kuwa mwenyekiti chama hadi 2003.
  • Makani pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa bodi za wakurugenzi katika Shirika la Ndege Tanzania, Williamson Diamond, Tanzania Breweries, Benki ya Taifa ya Biashara na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Law Society.
   
 9. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  alikosa staha na busara
   
 10. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  aikosa staha!
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nadhani Marehemu Brown Ngwilulupi alikuwa anatokea Mbeya Kama Sijakosea, kuna mwenye uhakika?
   
 12. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #12
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  sisiem imekosa wazee wenye busara kabisa ndio maana huezi ona mwinyi na kina warioba wanahusika kiviiiiiile kwenye mambo ya ndani ya chama ..wamebaki kina makamba na huyu mkama eti ndio wazee wenye hekima
   
 13. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #13
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  CCM wameonyesha kuwa wao ni magamba ya ukweli
   
 14. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #14
  Jun 12, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,143
  Likes Received: 10,500
  Trophy Points: 280
  Makamba alisema Nape na Mukama ndo wanao iua ccm aibu iliyoje.
   
 15. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #15
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mkiona uji wa mgonjwa unarudishwa nyumbani, andaeni mazishi!
   
 16. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #16
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  ulikuwa hujui ccm wote hawajui kufikiria kabla ya kutenda?
   
 17. Sir oby

  Sir oby JF-Expert Member

  #17
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  mkama hajui asemalo na amepata alichokihtaj,
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Teh teh eti kimba ingekuwa mm ningejiuzulu!
   
 19. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #19
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,380
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Aibuuuuuuuuuu!
   
 20. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #20
  Jun 12, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Kwa nin watu wanafanya msiba uwanja wa siasa? tulitarajia hapa watu watulie wakimuombea marehemuapumzike kwa amani na pia kukumbuka yale yote mema aliyosimamia! Mkama namfananisha na magimbi fulani kule kwetu hata uyapike kwa mwezi hayaivi ndio kichwa cha Mukama!!
   
Loading...