Mbowe: Rais, wanaopinga ushiriki wa Taifa kwenye vita ya Corona wanawaza uchaguzi na huruma yako ktk uteuzi. Ukweli lawama zote zitakuangukia wewe

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,599
217,991
Mbowe.png

HOTUBA YA MBUNGE FREEMAN MBOWE KWA UFUPI

Nimezungumza na Rais kwenye simu nimemuambia tafadhali shirikisha Jamii pana ya Watanzania ili jambo tulibebe wote, huu ni msiba na msiba haachiwi Mtu mmoja, kwa nia njema kabisa, tushirikiane kwa pamoja kwenye mapambano haya dhidi ya virusi vya corona.

Mhe. Rais unafiki haujawahi kuliacha taifa lolote salama, usikae wakati wote ukafikiri sisi ambao tunajaribu kukushauri, kuikosoa Serikali yako na kuilekeza, eti tuna nia mbaya au nongwa na wewe, hapana! , tunafanya hivi kwa nia njema na mapenzi sana kwa nchi yetu."

Mhe. Rais lawama zote za janga la Corona zitakuangukia wewe, huu ni ukweli wa Mungu na mimi kama Mbowe, mtu mdogo sana katika nchi yetu, nikwambie Rais wangu, wanaopinga ushirika wa taifa katika vita hii wanawaza uchaguzi na kuomba huruma yako katika uteuzi.

Nasikitika kwa niaba ya CHADEMA kwa namna ushauri wetu wa kuwataka Wabunge wajiweke karantini ulivyopokelewa vibaya na kuonekana tunashindana, Spika ametumia majukwaa mbalimbali kunishambulia na kuninidhalilisha mimina Viongozi wenzangu bila kuiona nia yetu njema.

Spika kila akitaka kuahirisha Bunge lazima apande na Mbowe, tumekutana Bungeni na Spika miaka 20 iliyopita sijawahi kumvunjia heshima hadharani wala sirini, nimesoma Kibaha na Spika amesoma pale ni mwanafunzi mwenzangu wa shule moja, namuheshimu,naliomba Taifa kumuombea.

Tuligoma lockdown tukashindwa hata kufanya partial lockdown na tukaruhusu ugonjwa kuenea na kuua wapendwa wetu, tulidhani tunalinda uchumi wetu na kusahau uhai wa watu wetu, sasa Corona inaendelea kutula wote, inakula uchumi wetu tupende tusipende.

Namshukuru Mungu kwa sasa Mwanangu ambaye alikuwa mgonjwa wa corona hatimaye amepona baada ya kukaa karantini kwa siku 57 nina uhakika amejifunza mengi, Familia nayo imejifunza mengi, nawashukuru Madaktari na wahudumu wengine

Kufuatia kikao hiki, Kamati Kuu imejadili kwa kina, miongoni mwa agenda mbalimbali, Janga la Corona na athari zake kwa taifa letu, mataifa ya jirani na dunia nzima katika ujumla wake.

Kamati Kuu,ilijiridhisha kuwa janga hili halihitaji masihara, mzaha wala usiri katika kulikabili.Ilitambua kwa mara nyingine umuhimu wa kuweka tofaui zetu pembeni na kutoruhusu chuki za kisiasa, hodhi za kisiasa, kiburi cha madaraka na mamlaka katika kupambana na vita hii.

Mwisho
 
Magufuli kusikia tu Mhe, Mbowe ataongea leo., Limekurupuka huko lilikojifisha ili mradi tu. linajiongeresha kanisani huko.
 
Hatutaki upotoshaji wa Mbowe

Mikusanyiko hairusiwi la sivyo ataenda lala selo
Kwa woga huu bandia, wa kuogopa kila jina la Mbowe linapotajwa, mnawapa ushujaa hata wale wasiostahiki.
Au hii ni namna nyingine ya kuendeleza upigaji wa wana-CCM kwa kuijengea CCM dhana ya uoga ili wababaishaji waendelee kuchota pesa kwa kisingizio cha kutoka taarifa?
Mimi siamini kuwa CCM inatakiwa kuwaogopa Watanzania kiasi hicho, na hususan kumuogopa Freeman Mbowe kiasi cha kumfanya IGP Simon Sirro aonekane kituko!
 
Back
Top Bottom