"Watu wa Usalama wa Taifa wamesambaza barua kwa masheikh wa Ruvuma na Mbeya inayoeleza kuwa waumini wa dini hiyo wasihudhurie mikutano ya CHADEMA kwa kuwa ni chama cha Kikristo na kina Ukabila," alisema Mbowe huku akionyesha barua hiyo kwa umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo
Walimlea sana Lipumba naona sasa Chadema inataka kula naye sahani moja hakuna kuleana ni mwendo live live kwa wanafiki wote wawe chama tawala ama wapinzani.Hawa jamaa wanapiga kote kote, yaani no stone will be left unturned and untouched.
hawana tofauti na KK hawa...Ndio maana tukastuka na kuhoji tangu mapema kuhusu kazi haswa ya hawa TISS!...wANAKUWA KAMA KAMPUNI YA MTU BINAFSI!PHP:"Watu wa Usalama wa Taifa wamesambaza barua kwa masheikh wa Ruvuma na Mbeya inayoeleza kuwa waumini wa dini hiyo wasihudhurie mikutano ya CHADEMA kwa kuwa ni chama cha Kikristo na kina Ukabila," alisema Mbowe huku akionyesha barua hiyo kwa umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo
Kwanini wao? Nafurahi kusikia kuwa hakuna chama cha kidini lakini imechukuwa muda kukubali hilo! Tulizoelea kusikia CUF kuwa ni cha udini!CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemshutumu Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, kuwa ni miongoni mwa wanasiasa wanaowahadaa wananchi kutojiunga na Chadema kwa sababu ya dini zao.
Akituhubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Tunduru jana, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema kwa muda mrefu viongozi wa CCM wakiwatumia viongozi wa dini na baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitoa shutuma kuwa chama hicho kina udini na ukabila na kueleza kuwa madai hayo hayana ukweli wowote.
"Mheshimiwa Lipumba namuheshimu sana, lakini amekuwa akiwahadaa wananchi kwa kuwataka wasijiunge na CHADEMA kwa kuwa ni chama cha udini na ukabila". Tanzania hakuna chama kama hicho alisema.
"CHADEMA kina watu wa dini na makabila tofauti. Kuna watu wanaotoka Arusha, Mbeya, Iringa na hata Zanzibar, sasa huo udini wanaosema unatokea wapi?" alihoji Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
Katika mkutano huo, Mbowe alionyesha barua aliyoeleza kuwa imesambazwa na maofisa wa usalama wa taifa kwa masheikh wa Ruvuma na mkoani Mbeya ikiwataka Waislamu kutohudhuria mikutano ya CHADEMA kwa madai ya udini na ukabila.
"Watu wa Usalama wa Taifa wamesambaza barua kwa masheikh wa Ruvuma na Mbeya inayoeleza kuwa waumini wa dini hiyo wasihudhurie mikutano ya CHADEMA kwa kuwa ni chama cha Kikristo na kina Ukabila," alisema Mbowe huku akionyesha barua hiyo kwa umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Source: Tanzania Daima
Ngekewa ndugu yangu, umesahau kuwa aliyeongoza kukiita CUF chama cha kidini ni huyo huyo Kikwete?Kwanini wao? Nafurahi kusikia kuwa hakuna chama cha kidini lakini imechukuwa muda kukubali hilo! Tulizoelea kusikia CUF kuwa ni cha udini!
. Ni aibu TISS kupandikiza chuki na kuigawa Mama TZ kwa misingi ya udini na ukabila. Hofu ya TISS kwa vya vya upinzani ni nini. Je ni beneficiary wa ufisadi wa CCM na serikali yake?.
Hapana watu kama Lipumba wakiachwa waendelee eti kutunza heshima watu watachukulia wanachosema ni kweli hakuna siasa za heshima sasa mtu anakatiwa live.Wow.... WOw CDM tafadhali sana chungeni midomo ili mueleze sera zenu zikubalike. Acheni kutolea uvivu watu au kujibishana na watu kama Nape. Inakuwa sasa mnacheza miziki mingi kwa pamoja ebu elezeni sera zenu kwa ufasaha ili watu wawaelewe vyema kwani mumeshaungwa mkono tayari na umma. Acheni kutaja majina ya akina Lipumba n.k elezeni sera kisha semeni juu ya udini huo bila kutaja majina yao.
Wow.... WOw CDM tafadhali sana chungeni midomo ili mueleze sera zenu zikubalike. Acheni kutolea uvivu watu au kujibishana na watu kama Nape. Inakuwa sasa mnacheza miziki mingi kwa pamoja ebu elezeni sera zenu kwa ufasaha ili watu wawaelewe vyema kwani mumeshaungwa mkono tayari na umma. Acheni kutaja majina ya akina Lipumba n.k elezeni sera kisha semeni juu ya udini huo bila kutaja majina yao.
Kweli mkuu na alivyotajwa next time kabla ya kuropoka Lipumba atakuwa anajiuliza mara mbilimbili hata akisema watu watakuwa na mawazo ya kuwa huyu jamaa ni mdini, wanavyofanya Chadema ni sawa kabisa mbona wao wanatajwa tena kwa majina kwanini wao wakitaja wanaambiwa wasiattack.Mkuu siasa za siku hizi sio za kuuma uma maneno. Sio za kinafki. Usipotaja majina na kueleza ukweli vizuri utaambiwa toa ushahidi. Ukitaja biashara imekwisha.
I think sio vizuri kupuuzia kauli za kipuuzi zinazotolewa na wanasiasa wengine kwani zinaweza kuwa na madhara makubwa sana. Ni lazima kuzishughulikia na kisha kuendelea kutangaza sera.
Unakumbuka kampeni za uchaguzi zilipoanza 2010? Ni nini kilimfungam mdomo makamba? Baada ya kuambiwa aeleze umma kwa nini alifukuzwa ualimu mkuu. Simple, ndivyo siasa za Tanzania zinavyoenda. Hoja kwa hoja, upupu kwa upupu.
TISS,PCCB,DOWANS,RICHMOND,EPA,MEREMETA.
Ee Baba wa mbinguni naomba uingilie kati.