Mbowe amshauri Kombani ajiuzulu

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515
Mbowe-November17-2014.jpg

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amemtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani, kujiuzulu kwa kuwa anaona ufisadi unaofanyika ndani ya serikali.

Aidha, alisema Kombani ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ulanga Magharibi, hana tuhuma zozote kuhusu Kombani, lakini anaona wizi unaofanywa na baadhi ya mawaziri ili kulinda heshima yake ajiuzulu ili aendelee kuwa msafi.

"Celina anajua kuwa kuna wizi wa kutisha serikalini, sijamsema Celina kwa sababu sina tuhuma zake, nikiwa nazo nitasema ili kuendelea kulinda heshima yake anatakiwa ajiuzulu," alisema Mbowe.

Mbowe alisema hayo wakati wa ziara yake ya operesheni ya "Delete CCM" kuelimisha wananchi kuhusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa na kuikataa Katiba iliyopendekezwa katika Jimbo la Ulanga Magharibi, mkoani Morogoro alipokuwa akihutubia wakazi wa eneo hilo.

Katika mkutano huo uliofanyika Kijiji cha Mwaya Kata ya Mang'ula wilayani Kilombero, alisema kwa sasa kuna tabaka kubwa katika elimu tofauti na kipindi alipokuwapo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, wanafunzi wote bila ubaguzi wa walikuwa wakisoma shule moja.

Alisema kwa sasa watoto wa mawaziri na viongozi wengine serikali wanasoma shule za kimataifa huku watoto wa maskini wakisoma shule za kata ambazo hazina maabara, walimu na vitabu.

Alisema serikali inaendelea kuwabebesha wananchi mzigo kwa kuwachangisha michango ya maabara huku mamilioni ya fedha yakiibiwa na viongozi badala ya kujenga maabara.

Aliwataka wakazi wa Kilombero katika uchaguzi wa serikali za mitaa kuwachagua wapinzani kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ili walete uwazi katika mapato na matumizi ya fedha za serikali kila baada ya miezi mitatu tofauti na chama tawala.

CHANZO: NIPASHE
 
Sio hivyo tu! Pia wakati wa Nyerere, wanafunzi wote walikuwa wanapewa ufadhili wa serikali bila kujali anasoma nini. Sasa ni watoto wa wakubwa mdio wanasoma kwa raha
 
RIP... Mama
Mungu akuweke upande unaostahili..
Tabia za kuita wenzenu wagonjwa..
Ooh ikulu siyo hospitali ,si kauli nzuri.
 
Mbowe-November17-2014.jpg

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mibowe

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amemtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani, kujiuzulu kwa kuwa anaona ufisadi unaofanyika ndani ya serikali.

Aidha, alisema Kombani ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ulanga Magharibi, hana tuhuma zozote kuhusu Kombani, lakini anaona wizi unaofanywa na baadhi ya mawaziri ili kulinda heshima yake ajiuzulu ili aendelee kuwa msafi.

“Celina anajua kuwa kuna wizi wa kutisha serikalini, sijamsema Celina kwa sababu sina tuhuma zake, nikiwa nazo nitasema ili kuendelea kulinda heshima yake anatakiwa ajiuzulu,” alisema Mbowe.

Mbowe alisema hayo wakati wa ziara yake ya operesheni ya “Delete CCM” kuelimisha wananchi kuhusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa na kuikataa Katiba iliyopendekezwa katika Jimbo la Ulanga Magharibi, mkoani Morogoro alipokuwa akihutubia wakazi wa eneo hilo.

Katika mkutano huo uliofanyika Kijiji cha Mwaya Kata ya Mang’ula wilayani Kilombero, alisema kwa sasa kuna tabaka kubwa katika elimu tofauti na kipindi alipokuwapo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, wanafunzi wote bila ubaguzi wa walikuwa wakisoma shule moja.

Alisema kwa sasa watoto wa mawaziri na viongozi wengine serikali wanasoma shule za kimataifa huku watoto wa maskini wakisoma shule za kata ambazo hazina maabara, walimu na vitabu.

Alisema serikali inaendelea kuwabebesha wananchi mzigo kwa kuwachangisha michango ya maabara huku mamilioni ya fedha yakiibiwa na viongozi badala ya kujenga maabara.

Aliwataka wakazi wa Kilombero katika uchaguzi wa serikali za mitaa kuwachagua wapinzani kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ili walete uwazi katika mapato na matumizi ya fedha za serikali kila baada ya miezi mitatu tofauti na chama tawala.

CHANZO: NIPASHE

Hatunaga kashfa kiukweli Poleni Wafiwa CCM na hasa Watanzania wote. Hivi kweli Lowassa akikasirika akaja kuenda mahakamani nani atapona
 
Hamna jipya. Kamanda Selina katutoka, Majembe mengine yapo tunasonga mbele.
 
Na kwake tutarejea.Waheshimiwa..Lusinde,Mwingulu na Mh sana Magufuli pamoja na sisi wengine tusi ibeze kazi yake Mola.
 
Aidha, alisema Kombani ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ulanga Magharibi, hana tuhuma zozote

...........
...........
:amen:
 
Umeiba comment Jile

Kabisa kaka........Umenikamataje?.....Nimeipenda unajua ccm wamelewa sn madaraka mpaka wamejisahau na wanakumbuka wkt kumekucha na watz wameshafanya maamuzi ya kuikataa
 
Back
Top Bottom