Mbowe amlipua JK kuhusu katiba mpya

Mbowe hana vilipulio kile kichwa hakina kitu haiwezekani uishie kidato cha nne uje umlipue msomi kama jk sijui ataanzia wapi yeye ishu zake ni muziki tu.

Hotuba za m-kwele ni kama za kwenye kitchen party au Sendoff... ni hotuba nyepesi zisizokuwa na mashiko kabisai!! Ukisoma kwa kutumia jina la mtu matatizo yake ndiyo haya!!!..
 
Hao wanaojiita wasomi tz wanawezakujivunia nini kwa wananchi wao? na wananchi wanakuonaje na usomi wako fanya uchunguzi wa elimu yako usije ukawa watu wanakucheka kila ukigeuka.
 
Kitila, you have put things in the manifesto which made me walk out of CCM (Kitila, umeweka mambo katika ilani ambayo yalinifanya mimi nitoke CCM). Nikamuulize yapi hayo mzee, akanieleza sera kama vile za elimu bure, serikali kusimamia kilimo, na akanionyesha sura kama mbili hivi katika ilani ambazo kwa maoni yake, na kweli ndivyo ilivyokuwa, zilikuwa haziendani na msimamo wa CHADEMA kiitikadi na kifalsafa.
 
Hao wanaojiita wasomi tz wanawezakujivunia nini kwa wananchi wao? na wananchi wanakuonaje na usomi wako fanya uchunguzi wa elimu yako usije ukawa watu wanakucheka kila ukigeuka.
vya kujifunia mbona vingi,piga picha Tanzania ya miaka ya 60 kisha fastforward Tanzania ya miaka ya 2000,uone tofauti.
 
kamanda ameongea ukweli ccm wanafiki wanabeza tumeshawazoea hamna jipya hatma ya ccm ni 2015
 
Najivunia kuongozwa na dr. jk,narudia dr.jk.ila samahani lkn udk.kaupataje? Au nikiini macho?mwl,J.K, Mr.B.W.Mkapa na Mr.Mwinyi mbona hata cku moja hawakutumia dr.
 
Naona mmeshindwa kujadili hoja mnaongea propaganda,Nakumbuka wapizani walishaitwa kila aina ya tunsi hivyo hatukati taama'
 
Kwa mbowe kuheshimu maoni ya wananchi ni kukubaliwa serikali tatu kama anavyotaka yeye na wakati huohuo hakuna ushahidi kuwa wananchi wote wanataka serikali tatu.
Yeye ndo anaforce anachotaka kiwe,wakati jk ashasema hata yeye hajui mwisho kutakubalika serikali ngapi.
Suala la mbowe kurudi kwa wananchi kama matokeo anayotaka yeye hayatapita halina impact kwani limeshazoeleka wao kwenda kuuza sura kwa chopa.

Mkuu Elungata mimi nadhani ingekuwa busara kwa bunge la katiba kuboresha maoni ya wananchi na sio kuyafuta, halafu wananchi ndo kupitia kura ya maoni wangekubali au kukataa kila ambacho wenzao wachache waliopata na nafasi ya kutoa maoni kwa tume. Sasa inavyoonekana CCM wamejiandaa kufuta vitu vingi kwenye rasimu na kupeleka kwa wananchi yale ambayo CCM wanataka. This is very sad kwa kweli.
 
Attachments

  • 1391525705905.jpg
    1391525705905.jpg
    62.2 KB · Views: 88
Mwenye CV ya mbowe atuwekee hapa, naona anongea kama mtu alieishia std 7.

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk

Huyu aliyeongea hiyo hapo chini na mwandishi wa bbc yeye naye mtuwekee cv yake hapa...
 
Attachments

  • 1391525774388.jpg
    1391525774388.jpg
    31.3 KB · Views: 96
Mbowe ni Mnafiki,Hajui Siasa Ni Kweli Alisema Live kwenye Mkutano Tatizo lake JAZBA NA KUPENDA SIFA Akishangiliwa Jukwaani Hapimi Asemacho ni KUROPOKA tuuu Kutafuta CHEAP POPULARITY
KATIBA ina Sehemu Kuu 3 ya Kwanza Ilikuwa 1. TUME YA KURATIBU MAONI
2.BUNGE LA KATIBA 3.KURA YA MAONI sasa Yeye Anadanganya Watu Kama vile Ile RASIMU YA PILI NDIO KATIBA TIYARI wakati Anajua VIZURI SAAANA kuwa BUNGE LA KATIBA kwa Mujibu wa Sheria Ambayo CHADEMA walishiriki Kuipitisha Lina MAMLAKA YA KUJADILI yaliyomo ktk RASIMU NA AMA KUONGEZA,KUREKEBISHA NA HATA KUPUNGUZA.
Anaposema Jambo fulani Likiondolewa NGUMI ZITAPIGWA MAANA YAKE NINI?? UHUNI WAKE APELEKE BILICANAS KULE!
NA kama Anasema Wengi wanataka Serikali 3 Si Watakataa Kwenye KURA YA MAONI WASI WASI WAKE WA NINI????

Sent from my BlackBerry 9981 using JamiiForums
 
010812.jpg

[h=2]
[/h]JUMANNE, FEBRUARI 04, 2014 06:52 NA KULWA KAREDIA

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amemjibu Rais Jakaya Kikwete kwamba asiingize utani katika masuala mazito ya taifa. Mbowe alisema Katiba ya Tanzania, itaamuriwa na wananchi wenyewe na si Chama Cha Mapinduzi (CM) ambacho kimekuwa na mkakati mkali wa kutaka kuua maoni ya wananchi.

Mbowe ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tu baada ya Rais Kikwete kudai amesikia kiongozi huyo wa upinzani akitangaza kutumia nguvu kupata Katiba mpya.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo juzi kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, wakati akihutubia sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa CCM. Alisema amesikitishwa na kauli hiyo na kuwataka Watanzania kutobabaishwa.

Kikwete alisema Katiba mpya itapatikana kwa hoja za kila upande kulingana na mapendekezo yake.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Mbowe alisema Rais Kikwete hapaswi kuchukulia utani katika mambo mazito ya taifa.

“Namuomba Rais Kikwete asichukulie utani mambo ya taifa suala la Katiba mpya. Anapaswa kuzungumza mambo ya msingi ambayo yanaleta tija.

“Siku zote Katiba ya nchi inapatikana kwa dhamira nzuri lakini tumebaini wenzetu hawa CCM hawaheshimu hoja za wananchi.

“Hebu tujiulize jinsi Jaji Joseph Warioba alivyotumia fedha nyingi kukusanya maoni ya Watanzania, leo CCM hao hao wanayakataa tuwaeleweje?” alihoji Mbowe.

Alisema Jaji Warioba ametoa hoja za msingi lakini kwa sababu ya uoga wa CCM wanataka kupindisha ukweli wa mambo.

“Mzee wa watu huyu amezunguka taifa zima kwa fedha za walipa kodi wa nchi hii, sasa wanataka watumie wabunge wao kukwamisha mchakato huu,”alisema Mbowe.

Alisema kama utawala wa Rais Kikwete utashindwa kuleta Katiba mpya ambayo inakidhi matakwa ya Watanzania, wao wataendelea kudai utawala mpya utakapoingia madarakani uwe ni wa Chadema au CCM.

“Nawahakikisha Watanzania, ikija Katiba mbaya tutaendelea kuidai kwa nguvu zote iwe CCM imeingia madarakani au sisi, Kikwete awe madarakani au asiwepo hatulali kamwe.

“Katiba ni maridhiano ambayo yanabeba maoni ya Watanzania sasa kwa nini CCM hawataki kuyafuata?” alihoji Mbowe.

Alisema CCM haina hatimiliki ya Katiba mpya na kwamba wakati wa kufanya uamuzi mgumu wa kupindisha maoni ya Watanzania umefika.

“Hawa watu hawana hatimiliki ya Katiba mpya, kwa nini wanajawa uoga kiasi hiki? Wanaogopa serikali tatu, nakwambia sitaki utani kwenye ya msingi,”alisema Mbowe.

NJE YA BUNGE

Mbowe alisema atahakikisha wanajadiliana vya kutosha ndani ya Bunge kuona haki inatendeka.

“Tutabishana kwa kila namna ndani ya Bunge,wakituzidi kete kwa rafu zao bungeni tutarudi kwa wananchi kuwashitaki maana hawa ndiyo walengwa… hatutaki kufika huko kama kila mtu ataweka busara zake chini.

“Dhamira ya CCM ndiyo inatufanya tutoe kauli hizi lakini nakwambia hapa hakuna mcheza ngumi… hoja ndiyo jambo la msingi tu,tutatumia maandamano nchi nzima maana haya ni haki ya msingi ya kila mtu,”alisema Mbowe.

kp31012014.jpg
 
Mbowe hajitambui! Ana hamu na damu za watu kama Idd Amin.
 
Back
Top Bottom