Mbowe akubaliana na Nyani Ngabu?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,255
113,668
Hey, ni mimi na si mwingine ambaye nishasema mara nyingi sana humu kuwa, ingekuwa ni juu yangu mimi basi nisingeshiriki chaguzi zozote zile zifanyikazo Tanzania chini ya usimamizi na uendeshwaji wa tume ya taifa ya uchaguzi yenye muundo iliyonayo sasa hivi ambapo kimsingi huwa inaundwa na mwenyekiti wa CCM.

Ni uamuzi rahisi sana ambao hauna ugumu wowote ule.

Soma hii mada yangu ya mwaka jana [na ninazo kadhaa zenye maudhui yafananayo].

Sasa leo inasemwa kuwa Mbowe naye kasema kuwa kuanzia sasa hawatashiriki tena chaguzi mpaka hapo kutapokuweko walau na tume huru ya uchaguzi. Rejea uzi huu hapa chini...

Nikisema sasa Freeman Mbowe anakubaliana na Nyani Ngabu au Freeman Mbowe aukubali ushauri wa Nyani Ngabu, nitakuwa nimekosea?

Oh...halafu majuzi hapa Tundu Lissu katumia maneno yangu pia 😉

Heheheeee.....I’m just sayin’
 
Kule Twitter CHADEMA na baadhi ya wanaharakati muda mrefu wameshasema suala la kutokuwa na imani na chaguzi zozote chini ya NEC hata kama kuna mabadiliko ya uongozi! Na hili lilishika kasi zaidi baada ya ACT kutaka kushiriki uchaguzi wa Muhambwe. Kwahiyo Mbowe kakubaliana na CHADEMA na Wanaharakati wengine. Sasa kama na wew ni mmoja ya hao wanaharakati, basi jibu ni sawa, amekubaliana na mwanaharakati wewe vilevile.
 
Toka 2005 mimi huo ndo umekuwa msimamo wangu.

Matter of fact, ni tokea 1995.

Nishasema kuwa ilikuwa ni makosa kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila katiba mpya na tume mpya ya uchaguzi iliyo huru!
 
Toka 2005 mimi huo ndo umekuwa msimamo wangu.

Matter of fact, ni tokea 1995.

Nishasema kuwa ilikuwa ni makosa kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila katiba mpya na tume mpya ya uchaguzi iliyo huru!
Wameuchukua ushaur wako kwa sabab jamaa wamenusa kuwa Bi Mkubwa ni mwepes kumtikisa lkn km Bi Mkubwa akikaza bila shaka 25 hasusi MTU.
 
🤩🤩🤩🤩🤩💃🏽💃🏽💃🏽💃🏽
Upo Juuuuu👏🏼👏🏼👏🏼
Kaka Mbeba Maboksi..
 
Back
Top Bottom