Mbowe ajitosa kuwatetea Watumishi wa Umma waliofukuzwa

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,911
2,890
Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni mheshmiwa Freeman Mbowe amesema haridhishwi na mtindo wa rais Magufuli kufukuza watumishi wa umma bila kuwasikiliza.

Aliyasema hayo mbele ya maaskofu akidai kuwa zaidi ya watumishi 160 wameondolewa kazini pasipo kusikilizwa huu sio utawala bora alidai mh Mbowe.
 
mwenyekiti wa chama cha chadema na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni mheshmiwa freeman mbowe amesema haridhishwi na mtindo wa rais magufuli kufukuza watumishi wa umma bila kuwasikiliza aliyasema hayo mbele ya maaskofu akidai kua zaidi ya watumishi 160 wameondolewa kazini pasipo kusikilizwa huu sio utawala bora alidai mh mbowe

Mboya anachanganya mambo- kwa utaratibu mfanyakazi anasimamishwa kwanza kupisha uchunguzi. Kisha Mfanyakazi atasikilizwa na tume baada ya tume ya uchunguzi kumaliza kazi yake. Presence ya mfanyakazi wakati wa uchunguzi may obstruct investigation or may affect his/ her work performance
 
Ni sawa na hadithi fulani hivi jamaa na punda wake akiwa na mzigo...
Mwanzo alipanda yule punda akiwa na mzigo juu yake alilaumiwa sana akiambiwa anamtesa punda.
Akaona isiwe shide amwache punda akiwa na mzigo yeye atembee kwa miguu,pia alilaumiwa kwanini anajitesa kutembea kwa miguu tena kwa umbali mrefu huku akimwacha punda anaenda na mzigo pekee.
Akaona isiwe shida aache mzigo na apande punda hapo ndo kabisaa akasemwa ujinga gani huu hata chakula habebi na huko aendako anashindwa hata kubeba akiba ya masurufu.
Huyo ndo binadamu haachi kusema
 
What the @&!!; kusikilizwa vipi yaani? si watu wanafikishwa namahakamani? namshukuru Mungu kukataa mabadiliko yale feki.. leo tungekuwa tunakiona cha moto.

unafahamu sharia na kanuni za utumishi wa umma wewe? hahahahah...by the way kwani kuna mabadiliko gani hadi sasa?

Au ngonjera za kwenye media? ivi kweli wewe unaona mabadiliko yapo...yepi hayo?
 
Nadhani anasema haya kwa sababu mafisadi wengi walikuwa wanawaunga mkono wakati wa kampeni, nashukuru mungu sikupoteza kura yangu.
Mbowe mwache rais awatumbue tu sio lazima akuridhishe wewe, sisi tuliomchagua ndio tunaridhika na utendaji wake.
Hivi kweli pale bandarini kuna mtu ameonewa kweli au ndio michango ya chadema ilipokuwa inatoka?
 
unafahamu sharia na kanuni za utumishi wa umma wewe? hahahahah...by the way kwani kuna mabadiliko gani hadi sasa?

Au ngonjera za kwenye media? ivi kweli wewe unaona mabadiliko yapo...yepi hayo?
Mbowe atakuwa alikunywa "ukawa"..kabla ya kuongea...maanake tunapoelekea atakuja kutukana...hajamsikia PM Majaliwa alivyosema bado watawashughulikia wabadhirifu bila kujali idadi...kwa akili za Mbowe alitaka kwasababu160 wameshachukuliwa hatua basi waliobaki waachwe..ndio maana huwa nasema kuna ombwe la uongozi chadema.
 
Obedi Mbangwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanyamapori wakati wa Sakata la Twiga kusafirishwa nje ya nchi kinyemela alisimamishwa kwa mbwembwe nyingi na Nyalandu tena akiwa bunge. Lakini alikuja kushinda kesi na serikali kumlipa gharama zake zote. Kumsimamisha mfanyakazi bila kufuata sheria za kazi ni kuipa serikali hasara kwa kuwa lazima itashindwa mahakamani.
Lakini pia nimpongezi Dr JPM kwa style yake ya Uongozi japo maamuzi mengine yatakuwa na hasara kwa taifa lkn uwajibikaji kwenye ofisi za umma unarudi kwa kasi kubwa.
 
Mbowe atakuwa alikunywa "ukawa"..kabla ya kuongea...maanake tunapoelekea atakuja kutukana...hajamsikia PM Majaliwa alivyosema bado watawashughulikia wabadhirifu bila kujali idadi...kwa akili za Mbowe alitaka kwasababu160 wameshachukuliwa hatua basi waliobaki waachwe..ndio maana huwa nasema kuna ombwe la uongozi chadema.

Kuna mtu aliyesema wasishughulikiwe?

Washughulikiwe tena sana tu...Ila utaratibu wa kisheria na kikanuni za ajira ufuatwe katika kuwashughulikia....

Kuna kosa gani katika kukumbusha kuwa kanuni na sharia za utumishi wa Umma zifuatwe?
 
What the @&!!; kusikilizwa vipi yaani? si watu wanafikishwa namahakamani? namshukuru Mungu kukataa mabadiliko yale feki.. leo tungekuwa tunakiona cha moto.

Sidhani kama anazuia wahalifu wasichukuliwe hatua ila sheria ichukue mkondo wake kusiwepo na HASARA kwa serikali ya kulipa mabilioni baadaye.Maana kuna watu wengine ni kweli wanatimuliwa tu kazini na watendaji bila kusikilizwa.

Ifike mahali timua timua iwe na evidence based.Mfano unamtimua Mkurugenzi eti ameshindwa kumsupervise subordinate wake mbele ya mkutano wa wadau na wafanyakazi wa taasisi unategemea huyo mkurugenzi atanyamaza??Akienda kushtaki nini kitatokea???

Ninamuunga mkono Mbowe kwa zile kashfa ambazo hazina factual evidence kama hiyo ya huyo mkurugenzi wasikilizwe kwanza.Issue wale wezi ambapo unapata hata hizo evidence hao iendelee,tuwaangalie hawa ambao kila kukicha watendaji wa Magufuli wanawafukuza,wakija kushtaki TAIFA limeliwa,serikali italipa mabilioni
 
Kuna mtu aliyesema wasishughulikiwe?

Washughulikiwe tena sana tu...Ila utaratibu wa kisheria na kikanuni za ajira ufuatwe katika kuwashughulikia....

Kuna kosa gani katika kukumbusha kuwa kanuni na sharia za utumishi wa Umma zifuatwe?
Watu ni wapotoshaji, kanuni na sheria za utumishi ziliwekwa ili zitumike hata pale mtumishi anapokosea na anaposingiziwa kwa sababu za kibinadamu. Mbowe kasisitiza kufuata sheria sio kuhukuniana kwa hisia na chuki.
Tukiendelea na mitindo hii basi tutajikuta tunaamua kuwa ni sawa tuu hata vibaka kupigwa mawe na kuchomwa moto bila kuwafikisha mahakamani eti hayo ndio mabadiliko na tumechoka na vibaka
 
Mahakama ipi imewatamka hao kuwa Mafisadi? Mbona ni jambo jepesi tu kueleweka? The Right to be Heard sio Optional jamani, ukishindwa kumpa mtu Haki ya Kusikilizwa huko mahakamani mnaenda kuuza sura tu, na baada ya hapo mtapaswa kuwalipa mamilioni ya kodi za Wananchi kama Fidia! Endeleeni kukurupuka muone mwisho wake!

Ni haki ya NATURAL JUSTICE

Amesema Chakaza kuwa endapo tutaendekeza utamaduni huu basi itakuwa sawa tu kwa wananchi tukikamata mwizi piga moto palepale

sharia na kanuni zipo ili zifuatwe

serikali inatakiwa iwe mfano katika hilo ili kuepusha kuingiza taifa katika hasara zisizo na lazima
 
What the @&!!; kusikilizwa vipi yaani? si watu wanafikishwa namahakamani? namshukuru Mungu kukataa mabadiliko yale feki.. leo tungekuwa tunakiona cha moto.
Ushabiki kweli unatia upofu! Hata wewe unashindwa kuelewa mantiki ya Mbowe ni nini? Wewe si ulikuwa mtetezi wa kuheshimu sheria na taratibu zikizowekwa kufuatwa?
Kumbe wrote ule ulikuwa unafiki?
 
Sa mbona nashndwa kuelewa ccm ndyo wapinzani au watawala?mbna wamekuwa wanapigana kuondoa ufisadi while cdm wanautetea?kweli mbowe kauza chama kwa mafisadi.tunahitaji mbadala wa cdm ili nch iende sawa

Watu wafukuzwe tena wafukuzwe sana...ila ufukuzaji ufuate sharia na kanuni za utumishi wa umma
 
Back
Top Bottom