Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,800
Daudi ametoa kauli hiyo, Alhamisi Oktoba 17, 2024, Jijini Dodoma wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kati ya taasisi zinazohusika na usimamizi wa maadili.
Akizungumza kwenye kikao hicho, Daudi ameeleza kuwa ofisi yake imeanza kupokea malalamiko kuhusu mmomonyoko wa maadili, hususan vitendo vinavyohusiana na uhusiano ya jinsi moja, jambo ambalo limepingwa vikali na serikali.
"Vitendo hivi vinakiuka maadili ya Kitanzania, na tunapaswa kukumbuka kuwa si kila kitu kinachotoka nje ya nchi ni kizuri," amesema Daudi, akiongeza kuwa vitendo hivyo vinaharibu utaratibu wa maadili kazini.
Daudi amebainisha kuwa serikali tayari imeanza kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaojihusisha na vitendo hivyo, na amesisitiza kuwa kuwahamisha watumishi hao hakutatui tatizo, kwani wanaweza kuendeleza tabia hizo katika maeneo mapya.
"Tulikemee hili kwa nguvu zote. Hatuhitaji mambo kama hayo serikalini. Sisi ni taifa lenye maadili yetu, na hili si sehemu ya maadili hayo," ameongeza Daudi.
Daudi pia ametoa wito kwa viongozi wa dini na jamii kuchukua hatua kali dhidi ya vitendo vya mahusiano ya jinsia moja, akisisitiza umuhimu wa kulinda maadili ya taifa na kuhakikisha jamii inaendelea kuzaliana kwa mujibu wa mila na desturi za Kitanzania.
Alisema, "Tufikirie mara mbili; wananchi wameacha kuzaliana, na tukiendelea hivi, baada ya miaka kadhaa tutashuhudia wanaume na wanawake wakiingia kwenye ndoa za jinsia moja. Ni lazima kila mmoja achukue nafasi yake, hasa taasisi za dini."
Chanzo: Jambo Tv
===================
SERIKALI YAKEMEA WATUMISHI WA UMMA WASIOFUATA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMANA. LUSUNGU HELELA-DODOMA
SERIKALI imeonya ukiukwaji wa maadili kwa watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na viashiria vya mapenzi ya jinsia moja na mavazi yasiyofaa jambo ambalo limekuwa likichafua taswira ya serikali.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 17,2024 jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi,wakati akifungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma.
Bw.Daudi amesema kuwa Ofisi imeanza kupokea tuhuma na malalamiko kuhusu kuwepo kwa viashiria vya mmomonyoko wa Maadili kinyume na mila na desturi za nchi yetu vinavyohusu vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kwa baadhi ya watumishi wa umma.
Amesema kuwa, vitendo hivyo ni miongoni mwa vitendo vya kijinai kwa mujibu wa sheria za nchi lakini pia ni vitendo vya kinyume na maadili kwa mujibu wa miongozo ya utumishi wa umma.
“Hivyo, tumieni kikao kazi hiki, kujadili na kubadilishana uzoefu ili kuja na mapendekezo ya namna sahihi ya kudhibiti vitendo hivi na namna sahihi ya kushughulikia masuala haya yatakapojitokeza katika maeneo yenu ya kazi kwa baadhi ya watumishi wanaohusishwa navyo ili kuepuka kuchafua taswira ya utumishi wa umma kwa ujumla,”amesema Bw.Daudi
Aidha ameziomba taasisi za Dini nchini kusimamia maadili na kuonya na kukemea vitendo hivyo vya ndoa ya jinsia moja katika jamii ya kitanzania mana wao wana nguvu na Sauti kubwa ya kusikika zaidi.
“Hivi sasa zipo nchi zimeacha kuzaliana kutokana na kushamiri kwa vitendo hivyo vya mapenzi ya jinsia moja,,Tanzania hatutaki kufika huko ndio mana tunakemea,”amesema
Kuhusu mavazi yasiofaa ameelekeza watumie waraka namba 6 wa utumishi wa umma unaozungumzia mavazi kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaochafua taswira ya serikali kwa kuvaa hovyo ndani na nje ya utumishi.
Amesema kuwa zipo taasisi ambazo viongozi wake wameanza kulegalega kwa kutochukua hatua na kuacha watumishi wakivaa mavazi kinyume cha maadili ya utumishi wa umma.