Mbowe aituhumu CCM kukihujumu Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe aituhumu CCM kukihujumu Chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by UWEZO_WAKO, Apr 10, 2012.

 1. UWEZO_WAKO

  UWEZO_WAKO Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe, amedai kwamba chama chake kimebaini mpango wa CCM kutaka kukidhoofisha chama hicho bungeni na kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

  Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa NMC mjini hapa juzi, Mbowe alidai kwamba chama hicho tawala kinatumia dola kutekeleza mpango wake huo. Alikuwa akizungumza katika mkutano uliondaliwa na chama chake baada ya Mahakama kumvua Ubunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

  "Tunaionya Serikali ya CCM ijue kamwe hawatafanikiwa katika njama hizi na hata wakitupiga risasi mimi na Dk Willibrod Slaa, bado nguvu ya mageuzi nchini haitafutika kwani kuna makamanda wengi wapo ambao wanataka mabadiliko ya kweli katika nchi hii," alisema Mbowe.

  Alisema nguvu ya chama hicho, bungeni haitapungua kutokana na kuondolewa Lema, bali imeongeza kiu ya kuendelea kupigania utawala wa haki.

  "Tutakwenda bungeni kutetea mihimili mitatu ambayo ni Bunge, Mahakama na Serikali kutoingiliwa na kila kimoja kifanye kazi yake inavyostahili," alisema Mbowe.

  Mbowe aliionya Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa kuacha kuingilia mambo ya siasa kwa kukipendelea CCM huku akitamba kwamba kina uhakika wa kushinda Uchaguzi Mkuu wa 2015.

  Nape: Mbowe hana hoja
  Alipoulizwa kuhusu madai hayo ya Mbowe, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema: "Hana hoja ya msingi."

  Aliendelea: "Huwezi ukaiba halafu ukataka usishtakiwe. Wao (Chadema) wanatapatapa kwa kuwa wanajua walicheza rafu nyingi kwenye uchaguzi na wanajua mahakama itatenda haki."

  "Ninawaomba Watanzania wawapuuze na namtaka Mbowe aziache Mahakama zifanye kazi yake ya kutenda haki. Mahakama ni chombo huru na kinapaswa kufanya kazi kwa uhuru bila kuingiliwa," alisema.

  Rufani kesho
  Chadema leo kinatarajia kufikisha Mahakama Kuu rufani ya kupinga kutenguliwa kwa matokeo ya ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini.

  "Tutakwenda Jumanne Mahakama ya Rufani kwa majaji watatu kusikiliza rufani yetu, hatutaki majaji watupendelee Chadema au CCM. Tutawaomba watende haki kwani umma wa Watanzania unasubiri kwa hamu uamuzi wao,"alisema Mbowe.

  Alisema kutokana na mazingira ya kesi hiyo na mahitaji ya Jimbo la Arusha Mjini kuwa na mwakilishi bungeni, wana imani rufani hiyo haitachukua muda mrefu kutolewa uamuzi.

  Katika huku yake ya Aprili 5, mwaka huu, Jaji Gabriel Rwakibarila alitengua matokeo ya ubunge katika jimbo hilo na kumzuia Lema kugombea nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano, baada ya kujiridhisha kuwa alitumia maneno ya kashfa, matusi na udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mgombea wa ubunge wa CCM, Dk Batilda Burian.


  Source: Mwananchi
   
 2. O

  Original JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Polisi, Mahakama, Jeshi na usalama wa taifa aka CCM vyote ni mali ya CCM ama ni matawi ya CCM. Hakuna haki wala demokrasia ndani ya Tanzania.
   
 3. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Nape haeleweki kabisa, anataka asikike bila kuwa na points za msingi.
   
 4. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Wananchi tuna matumaini makubwa na cdm, haturudi nyuma, Nape kuna siku atatambua jinsi majaji na mahakimu wanavyozinanga sheria za nchi, na hasa atakapokuwa na chama cha upinzani ccm.
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Napata tatizo kidogo hasa pale ambapo vyombo vya ulinzi vinapotuhumwa kukisadia Chama cha mapinduzi, hivi kwa nini tusiwe tunapewa ushahidi na wanaolalamikia vyombo hivyo badala ya tuhuma tu jambo ambo linaweza kuonekana kama ni kuvipaka matope. Mbona kuna tuhuma zingine huwa kuna ushahidi unatolewa na walalamikaji?

  Tumeshuhudia katika majukwaa wanasiasa wakitoa barua mbalimbali zinazoonesha njama mbalimbali za kuhujumiana pamoja na kwamba pengine zinakuwa na ukweli ndani yake na wakati mwingine hazikuwa na ukweli. Hili la kutuhumu vyombo ya ulinzi mbona linaonekana la kizushi zaidi.
   
 6. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  si unajua tena maneno ya wakosaji!
   
 7. J

  J.o.s.e.p.h Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani msipoteze muda na Nape hawana jipya na Chama chake la kuwaeleza watanzania.
   
 8. K

  KABALE Member

  #8
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  kila mara ninaposoma maoni ya nape kuhusu swala lolote la kitaifa naihurumia ccm.
  pamoja yote yanayoendelea ndani ya ccm, kama wanaona huyu kijan is one of the creams on top...basi wasitegemea la maana toka kwake....he is fit to ccm district spokesman....

  anyway waendelee kumuweka hapo wanatoa advantage kwa washidani wao.....shit
   
Loading...