Mbona yalikuwa makubwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbona yalikuwa makubwa!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mtambuzi, Nov 24, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 2005, nilikuwa naelekea Mbagala kwenye kiwanda cha kutengeneza kanga na vitenge cha KTM. Nilikuwa ndio kwanza nimefungua biashara ya kuuza kanga na vitenge na nilikuwa nachukulia mzigo wangu kiwandani moja kwa moja.

  Siku hiyo nilikuwa naenda kuweka order kwa ajili ya wiki inayofuata, na safari yangu ilianzia pale Kariakoo ambapo nilipanda basi aina ya DCM na kupata kiti. Naijua adha ya usafiri wa Mbagala, lakini siku hiyo usafiri haukuwa na tabu sana, labda kwa sababu ilikuwa ni mchana. Nikiwa nimekaa kwenye kiti , alikuja abiria mwingine na kukaa kwenye kiti hicho na mara basi likaanza kuondoka baada ya kupata abiria wa kutosha. Alikuwa ni msichana tu, ambaye alionekana kama mgeni kidogo hapa Dar, na hiyo ilitokana na mavazi yake na hata ongea yake, hasa pale alipomsalimia mama mmoja aliyekaa kiti cha jirani. Sikujishughulisha naye kwani nilikuwa nimejiinamia nikisoma gazeti.

  Huyu binti alikuwa akinitizama sana, na alikuwa akinichunguza kwa udadisi, wakati wote alikuwa akinitizama kama ananitilia mashaka, ilibidi nimgeukie na kumuuliza kama anashida gani, maana nilianza kumuona kama kero. Alinitazama kwa taharuki na kuniambia, ‘eh, ulijua mwenyewe sitakushika hivyo, ulijua una akili kama maraika. Sasa leo nimekushika au sikukushika?' kwanza, nilifikiri ni mzaha, ingawa sikuwa nimemwelewa ana maana gani. ‘Unasema na mimi?' Nilimuuliza. Alisonya na kusema, ‘kumbe ivo nasema na nani mwingine?' alikuwa na lafudhi ya Kiiringa kabisa. ‘Umejitia mjanja, ati unajifanya kunibaka, ukajua sikushiki.' Alisema na nilianza kupata wasiwasi.

  ‘Wee binti wacha wendwazimu wako, yaani mimi nimekubaka wewe?' nilisema na sauti yangu ilikuwa na kitetemeshi kwa sababu ya hasira na hofu. ‘Hee, yaani unataka nikupigie kelele wakupeleke polisi. Nataka uniambie kwa nini siku ile ulipokuja kulala kwa dada ulininyatia usiku ukanigeuzaga mkeo?' Hapo nilizidi kuchanganyikiwa, kwa sababu pia abiria wengi walikuwa wamevunja shingo kutaka kujua kulikoni. ‘Sikiliza binti, nadhani umechanganya mambo. Mimi naitwa nani?' Yule binti alisema, ‘bwana wee usitake kunichanganya. Wee si binamu yake dada, hakujui nani wewe. Wewe si Julius. Mii nikionaga mtu siku moja tu, simsahaugi tena….. Ndio maana tangu siku ile hujaja tena kwa dada.' Aliunganisha madai.

  Sasa nusu ya basi walikuwa wanasikia kinachoendelea. ‘Naomba tushuke twende kituo cha polisi ili tukajue mwenye haki.' Nilisema, nikiwa sina hakika kama natoa pendekezo sahihi. ‘Twende kwani mie naogopa, twende ukafungwe miaka 30 ukome kubaka watoto wa wenzio. Jitu kubwa linanyatia wanawake ………' Baadhi ya abiria walicheka na wengine waionyesha dalili zote za kutaka kujichukulia sheria mikononi, maana hata miaka 30 jela nilishahukumiwa mle mle ndani ya basi.

  ‘Dereva ingiza basi kituoni, kuna mtuhumiwa wa ubakaji humu ndani ya basi amenaswa.' Abiria mmoja pandikizi la mtu alisema huku akiwa amenikazia macho, nilianza kuwa mdogo kama sisimizi…….. Lakini abiria mwingine alidakia, ‘kwani wewe binti unamjua huyu kaka kwa jina? ‘Namjua, anaitwa Julius anafanya kazi kwenye kutengeneza semeti ni dereva. Yule abiria alisema, ‘braza, unaweza kutupa kitambulisho chako tuone?' Nikajua mambo yamekuwa mambo. Nilitoa kitambulisho changu cha kupigia kura na kadi ya benki. Havikuwa na jina la Julius. Yule abiria alivisoma kwa sauti na kusema, ‘binti inawezekana umechanganya mambo, na ujue kumsingizia mtu jambo kama hilo ni kosa la jinai'

  ‘Je kama kabadilisha jina mii nitajuaje. Basi, kama ni hivyo mimi namwachia Mungu.' Ilibidi nikatishe safari na kushuka njiani ili nirudi nyumbani, kwani uso wote ulikuwa umesawajika kwa fedheha………Kumbe mtu anaweza kukufanya ukauawa hivihivi…………………….! Sikuwa namjua yule binti, na wala katika maisha yangu sijawahi hata siku moja kufikiria kumnyatia hata house girl wangu, au hata kutongoza hovyo.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Ndefu mno, samaraizi basi.
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Dah, im speechless...!!
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Pole, ngoja waje wenzio watasoma...................LOL
   
 5. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  ntarudi kuisoma_kwa sasa niko busy.
   
 6. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  na waje tu.....
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Kumbe na wewe unapenda fupi?
  Wenzio ni vibanga, tumepigwa na mkoloni au unataka anirushe dirishani? Na hapa ppf tower ntaangukia kwenye lami niwe chapati

   
 8. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  kaka pole sana. inasikitisha na kufurahisha pia! Lakini kama usingekuwa na kitambulisho chochote naona kweli ungehukumiwa kwa kosa ambalo sio lako. Na hasa polisi wetu walivyokuwa wavivu siku hiyo hiyo ungeswekwa rumande bila hata maelezo. Pole mkuu, natafuta vitambulisho vyangu vyote leo leo!!!
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Kumbe the moral of the story ni lifananishwa na mbakaji.

   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ni tukio ambalo bado nalikumbuka............................
   
 11. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #11
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Umeona eh! Ahsante kwa kusoma simulizi hii ndefu, lakini yenye kufundisha..................
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  pole sana rafiki, our world is not fair.
  Sasa itabidi uanze rasmi kutongoza mahausi gel, kuwanyatia na ukishindwa kabisa uwe unawabaka, ndio watakuheshimu.
   
 13. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Nawe una vituko.....
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Aisee! we acha tu, huu utu uzima nilionao, ninayo mengi ya kusimulia.....................
   
 15. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hi ndo stail ya machangudoa. Wakikuona dizaini fulani wanakutokea eti umewarusha na ka vipi wanakujazia watu. Kuepuka unamkatia kiasi unaanza mbele!
   
 16. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  kumbe ni simulizi za mama na mwana
   
 17. B'REAL

  B'REAL JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 3,107
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 160
  dah!!mtambuzii banaa kama yamekukutaa kwelii pole...hii halii ishawai kunitokea nikafananishwaa,na jamaa mmoja alimuibiaa m2 mwanzaa sasaa tukaja kukutana arusha,jamaa aliniganda mbayaa.
   
 18. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,408
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  Mi nilikuwaga nasikiaga tu kwamba marehemu hakuwaga na kosa kumbe inakuwa hivi...........!!!!
   
 19. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,993
  Likes Received: 1,046
  Trophy Points: 280
  Pole sana kaka. Bahati nzuri kwako ulikuwa na Kitambulisho na Kadi ya Benki tena vyote vikiwa na jina tofauti.

  Hivi ingetokea Kwa bahati mbaya (nzuri) kitambulisho na kadi hiyo ya Benki vikawa na jina la Julius, sakata hili lingekuwaje?
   
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  pole na hongera
   
Loading...