Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,838
Katika mambo yoote niliyosikia kuhusu Mke wa D.Trump, Melania Trump sijawahi kusikia Wazungu wakicheka lafudhi ya Kiingereza chake, huyu Mama anatokea nchi ya Slovenia ambayo iko Ulaya ya Mashariki hivyo Kiingereza chake ni cha kujifunza tena ukubwani, lkn hakuna Mzungu anayeona kuwa ni ishu, sasa ni kwa nini?
Hivi huyu Mama angekuwa ni Mtanzania au Mwafrika halafu anaongea kiingereza kwa lafudhi ya Kitanzania, hali ingekuwaje?
Je, ni kwa nini sisi (Waafrika) ambao wote siyo native english speakers huwa tunawacheka Waafrika wenzetu wasio na lafudhi ya Kizungu, ili hali sisi wenyewe hatujui hicho kiingereza chenyewe? Hivi mtu kama Tundu Lisu ambaye amezaliwa na kukulia Singida Mashariki ana uhalali gani wa kukosoa na kucheka Kiingereza cha Raisi Magufuli, kweli? Kuna mtu anaweza kunielewesha hapa?
Msikilize hapa Melanie Trump akihojiwa na jinsi lugha ya Kiingereza inavyompa shida!
Melania Trump!