Roho iliuma ulipoona anaolewa na mwingine ni vzr kuachana naye na kutafuta mwingine ambaye mtaelewana.
Asante sana kwa kunielewa. Umeandika sahihi kabisa kuhusu sababu yangu ya kuleta huu uzi.
Ila napenda kusahihisha kuwa hajawahi kunikataa, mimi ndiye nilikuwa sieleweki kwake alipokuwa anauliza habari ya ndoa. Sikuwa tayari. Halafu tangu alipoanza kusisitiza kuhusu ndoa sikumtendea vizuri sana, hilo nimekiri tangu mwanzo. Hata mimi nilikuwa sijielewi kipindi kile, naona kama alikuwa mbele yangu sana kwenye hayo mambo. Basi tulipokubaliana kuwa haiwezekani tukakubali kutenganishwa na hizi mishemishe za kutafuta riziki, mikoa tofauti. Hadi alipokuja kunitaarifu kuwa anaolewa, na nikamuunga mkono maana tulishakubaliana kutakiana mema katika maisha. Nilipomuona yule mchumba wake siku ile ya send off yake, yani kitu nisichokielewa kikaniambia ndani ya roho yangu kuwa this is the wrong guy, given what I know about her. Na nikabaki kwenye masikitiko kuwa mimi na yeye tunatakiana heri kwenye maisha lakini hii aliyopata naona kama ni shari, si heri. Na yametokea.
Na baada ya kuolewa hatukuwasiliana tena. Tumepeana namba upya juzi tulipoonana kwa bahati tu kila mtu akiwa kwenye shughuli zake.
Naweza kusema ni instinct tu kutokana na ukaribu tuliojenga.
Ex-GF wangu alipoolewa mwaka 2010 desemba nilileta thread hii hapa: https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/94798-ex-gf-wangu-kaolewa-jana.html.
Watu walininanga na kunisuta sana eti ni wivu unanisumbua. Walionielewa ni wachache sana. Juzi tuesday nimekutana naye kaniambia wameachana, tena kwa talaka kabisa ya mahakamani.
Jamani muwe mnakubali tu kuwa kuna ukaribu fulani ukishakuwa nao na mtu wako, basi hata kwa hisia tu unaweza kujua kinachomfaa na kisichomfaa.
Mimi nilipokuwa naye sikuwahi kumuuliza size ya kiatu au ya bra, nikifika dukani nikitazama tu naona hiki kitamtoa na kweli hata mwenyewe alikuwa anashangaa. Nilijua hisia zake na taste yake, yaani kwa karibu kila kitu.
Anyway, yaliyopita yamepita. She is happy with her child and professional life, kiuchumi pia yuko vizuri. Mimi pia bado niponipo.
Kuna waliotabiri kuwa ningeleta thread nyingine kumhusu, basi utabiri wao umetimia.
Kitu gani kinakusababisha kudhani kuwa hatuelewani na huyu?
si suala la shehe yahya, ni kwamba nilikuwa vizuri sana naye, nisingekosea observation ile.
Bado niponipo kaka. Hupendi?
Ukipewa chance ya kurudiana nae utafanya hivo? utakubali kulea mtoto wake? wewe una mtoto?
muda wote mliokuwa apart anaweza kuwa amebadilika tabia na mind yake imekuwa tofauti, kama unafikiria kuwa na mahusiano nae usitegemee kuwa atakuwa kama kipindi mko wachumba. Just note that and all the best.
Kumbe bado una mawazo naye? Ndiyo maana ulikuwa unafuatilia maisha yake kwa karibu. Utakuwa umechangia kwa % kubwa kuachana kwao.
Aiseee.....kwa hiyo umefurahi??????????
Asingekubali kuolewa na mwingine zaidi yako.
Badilika au bado upo upo tu.
Mimi nilipokuwa naye sikuwahi kumuuliza size ya kiatu au ya bra, nikifika dukani nikitazama tu naona hiki kitamtoa na kweli hata mwenyewe alikuwa anashangaa. Nilijua hisia zake na taste yake, yaani kwa karibu kila kitu.
Ungekuwa wewe ungefanyaje? Ungekasirika?