Mbona ufugaji na biashara ya nyama na mayai ya kware umeyeyuka ghafla?

Wakenya walituthibitishia sisi wengi wetu ni kizazi cha "copy and paste".Hatuumizi vichwa kufikiri,kujihoji na kutafuta masoko wenyewe.
Kumbe ilianzia Kenya? ila sio mbaya kwani hata wao walimiminika Loliondo kwenye kikombe cha Babu.
 
Tanzania, ndiyo mahala pekee ambapo ukisema kuwa kinyesi cha nyoka ni dawa ya ugonjwa wowote ule ama ni dawa ya utajiri watu watafuga nyoka ili wapate hicho kinyesi bila kufanya uchambuzi na utafiti.

Jiulize,. Kama Taifa tunategemea utafiti wa taasisi uchwara ya TWAWEZA, ili kufanya maamuzi unategemea chochote hapo kwenye kware!?

Zaidi, hapo Tanzania, watu wamekaa kwa ajili ya kupiga deal na kusepa.

Mara Mitiki, oooh Oooooh Ufuguji wa Nyuki, Kilimo Kwanza, maara wiwiwii, Kilimo ni Biashara, oooh Oooooh, Kilimo cha Uyoga , Ufugaji wa Samaki.

Kilichobakia ni Ufugaji wa Ndevu nao itakuja kusemwa ni project yenye hela na soko.

Kwa kifupi, watanzania tunapaswa kujitathimini tunakoenda na hasa kupima haya matamko.
Zaidi ya hapo, tutakuwa tunaonekana kama waganga wa kienyeji.
Ha ha ha ha ha ha ha nimecheka sana......

SONY Xperia Z5 Premium
 
hapo ni pale watu wa marketing wanapokuwa wazuri kuliko uzuri wa bidhaa yenyewe
 
Ndiyo kilichobakia sasa.

Maana humu jf nimeona , mara ufugaji wa ng'e, mara ufugaji wa nyoka .
Mambo chungu nzima bado tu kusikia project ya kufuga NDEVU.




kama hivi
 

Attachments

  • images.jpeg.jpg
    images.jpeg.jpg
    8.3 KB · Views: 32
Wakuu kama mtakumbuka kupitia jukwaa hili miaka miwili mitatu iliyopita tulihamasishana sana kuhusu ufugaji wa kware ili kunufaika na biaashara ya nyama na mayai. Tuliambiwa pia mayai ya kware yana afya kulinganisha na mayai ya kuku.

Ghafla, sioni tena ule ''moto'' wa ufugaji wa kware, nini kimesababisha? je, hakukufanyika utafiti? Je, ile afya au virutubisho kwenye mayai ya kware haikuwa kweli?


Siku hizi watu tunafuga kunguru na bundi kwa kwenda mbele tu....kware wa nini?
 
Back
Top Bottom