Mbona siwaelewi DAWASCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbona siwaelewi DAWASCO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WILSON MWIJAGE, Nov 25, 2011.

 1. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dar es salaam pamoja na kuwa na wakazi wengi ina tatizo kubwa la maji achilia mbali matatizo mengine. Maji hayatoki kwenye mabomba kama wakazi wake wanavyotegemea, Pamoja na ukweli kwamba watu mkoani Dar es salaam wanaongezeka kila siku lakini pia miundombinu ya maji haitoshi kabisa kukabiliana na tatizo hili. Ni miaka 50 sasa jiji kumbwa kuliko majiiji mengine linakosa maji safi, salamA na ya uhakika. Hili kwa sasa si suala hasa ila suala langu ni hili;

  Hapa eneo la Mlalakuwa (Savei) kuna baadhi ya mabomba ya maji ambayo yalipasuka kwa kukanyagwa na magari au kukatwa kwa makusudi kwa muda mrefu na muda wote yanamwaga maji barabarani. Si tu kwamba wenye mabomba hayo hawaangaiki kuyafunga mabomba yao bali pia wenye dhamana na maji hayo (DAWASCO - KAWE) ndo kabisa hawana habari. Hii ni kero si tu kwa watembea kwa miguu pekee bali pia kwa wanaokosa maji ya kutumia majumbani mwao.

  Wakazi na wenyeji wa eneo hili wanasumbuliwa na kelele za mara kwa mara zinazosababishwa na DAWASCO kwa matangazo ya kuwakatia maji wale wote ambao hawajalipia bili zao za maji. Si kwamba napinga watu wasilipie bili zao za maji ila napinga kukanyaga tope kila siku linalosambazwa na magari likiwemo gari la matangazo la DAWASCO-KAWE.

  Wito wangu kwa wenye mabomba na DAWASCO (wahusika) timizeni wajibu wenu kwasababu maji ni UHAI
   
 2. Petiro

  Petiro JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ufanisi wa Dawasco uko chini sana zaidi ya kupiga porojo na kwamaana maofisa wake ni makada wa magamba hawachukuliwi hatua yeyote.
   
 3. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,393
  Likes Received: 2,438
  Trophy Points: 280
  :mad::angry::mad::angry::mad::angry:Kwa kifupi DAWASCO, TANESCO na MUHIMBILI, yaani ni kama hivi vitengo havipo kabisa, wahusika wamelala, utasikia kila kukicha wako kwenye semina, warsha, mikutano na upuuzi wa kila aina, wao ni kulipana maposho tu ya kila aina.
  Ni rahisi mno kwa wahusika kufanya lolote, ila wao wanaangalia matumbo yao tu, hivyo vitengo vyote viko chini ya wizara zake, cha kustaajabisha mawaziri ndio utasikia wanaponda mahela kwa masafari, na Mh JK anawatazama tu?! Inasikitisha kwa kweli!
   
Loading...