Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,037
- 34,741
Eddy ameamua kuondoka nyumbani kwa wazazi wake na kwenda kupanga, kwa bahati nzuri anapata chumba katika nyumba moja yenye vyumba sita maeneo ya Mwananyamala kwa Kopa.
Nyumba hiyo imekaa Kiswahiliswahili kutokana na wapangaji wanaoishi ndani ya nyumba hiyo.
Kila chumba kimoja kilikuwa na mpangaji mmoja aliyekuwa akiishi na familia yake.
Pia katika nyumba hiyo iliyokuwa na mabanda ya uani, waliishi wapangaji ambao hawakuwa na wake wala waume.
Kati yao walikuwepo wasichana wazuri wenye maumbile ya kupigiwa methali, ambao wengi wao hawakuwa na shughuli maalumu za kuwapatia kipato.
Baba na mama mwenye nyumba nao walikuwa wakiishi ndani ya nyumba hiyohiyo.
Siku ya kwanza Eddy alipokuwa akihamia hakuwa na vitu vingi zaidi ya kitanda kidogo, kabati la nguo na vikombe sita vya chai.
Pia alikuwa na sahani mbili za chakula na jiko moja la Mchina. Kijana huyo aliamua kuanza maisha hayo ya usela japokuwa wazazi wake walikuwa na uwezo mkubwa sana.
Baba na mama yake walimsihi sana kuendelea kukaa nao maeneo ya Kinondoni lakini wala hakutaka kusikiliza ushawishi huo.
Kikubwa alichokuwa akikitaka Eddy ni uhuru, kwani alijiona ameshakua mkubwa, hakutaka kufanya mambo ya uhuni ndani ya nyumba ya wazazi wake.
Mbali na hivyo wazazi wake walikuwa wakimdhibiti sana kijana wao kuingia katika maisha ya kupenda wanawake, hawakutaka ajiingize huko mapema.
Eddy alivumilia ucha Mungu wa wazazi wake kwa kipindi kirefu lakini alipomaliza shule tu hata kabla majibu ya kidato cha nne hayajatoka, akaamua kuhama.
Ushawishi huo aliupata kwa marafiki zake, Salim Raha na John Tupatupa ambao walikuwa na uhuru mkubwa wa kuingiza vyumbani mwao kila aina ya warembo.
Naye alitamani uhuru huo, akaamua kuwaaga wazazi wake na kuondoka katika nyumba ya familia.
Lakini kabla ya kuhama, mara kadhaa kijana huyo alikoswakoswa kunaswa na wazazi wake pale alipoingiza msichana chumbani kwake.
Siku ya kwanza alipoingia katika makazi mapya alikutana na Rehema, msichana wa Kizaramo aliyekuwa ameumbika vyema.
Eddy alishtuka kiasi hata Rehema mwenyewe kuhisi mgeni huyo alikuwa amepagawa kisawasawa. Siku hiyo mrembo huyo alikuwa akisugua miguu yake katika jiwe maalumu lililopo karibu na mlango wa kuingilia msalani.
Rehema alikua ametoka kuoga, akiwa amevaa kanga moja tu iliyokuwa imelowana na maji na kumfanya maungo yake ya ndani yaonekane.
Ndiyo, kanga ilikuwa imeshikana na mwili na kila Rehema alipokuwa akisugua kisigino chake, ndivyo alivyokuwa akimpagawisha Eddy kutokana na kuzalisha mtetemeko wa haja katika mlima aliokuwa ameufungashia nyuma ya mgongo wake.
Kijana huyo alibaki ameduwaa kwa kitambo kirefu akimwangalia Rehema huku akiwa ameshika sahani mikononi mwake lakini Rehema ndiyo kwanza akajifanya kama vile hakuwa amemuona.
Binti huyo akaendelea kufanya kile alichokuwa akikifanya, mara alishtuka aliposikia mlio wa vyombo vikipasuka.
Ndiyo, Eddy alikuwa ameziachia sahani alizokuwa amezishika mikononi mwake bila ya kutarajia.
Kufuatia mlio uliotokana na sahani kuvunjika, Rehema alimgeukia Eddy na kumuuliza kulikoni ndipo kijana huyo alimwambia zilimteleza kwa bahati mbaya.
Ndiyo kwanza mchezo unaanza, unataka kujua zaidi? Weka Like chini ndio nitajuwa munaipenda hii hadithi pasipo weka like sitoweza kuendelea na Hadithi Mpya mnasemaje kuhus hadithi mpya?