Mbona kama siviamini CHAUMMA na ACT WAZALENDO?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,645
Reaction score
10,865
Ingawa nilianza kupiga kura mwaka 2000, lakini sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.

Ingawa sina Chama, nilikuwa ninafurahia ninapoona ushindani wa kisera kati ya CCM na CHADEMA! Kwa bahati mbaya, mpaka sasa hakuna uhakika wa CHADEMA kushiriki uchaguzi wa mwaka huu.

Vyama vinavyotajwatajwa kwa sasa ukiacha CHADEMA, ni ACT WAZALENDO na CHAUMA! Lakini mimi nikiviangalia, sioni kama ni vyama vya siasa vinavyotanguliza mbele maslahi ya nchi. Ni kama vile vinafanya maigizo tu ama vinatumiwa na Chama tawala kwa manufaa yake!

Mtu unawezaje kukubali kushiriki uchaguzi ambao unafahamu ni mshindani wako ndiye mwenye uamuzi wa mwisho juu ya matokeo?

Mtu unakubalije kushiriki uchaguzi ambao unaona wazi kabisa kuwa hauna maslahi kwa Taifa? Ubunge na udiwani ni bora kuliko matakwa ya wananchi?

Kuna anayeweza kunishawishi niwaamini akina ZITTO KABWE, JOHN MREMA, SALUM MWALIMU, n.k?
 
CHADEMA ndiyo chama cha upinzani nchi hii,hiyo imewafanya akina Heche kumuunga mkono Lissu katika mapambano.Amini CHADEMA,amini baadhi ya viongozi wake kama Lema,Lissu,Heche na wengine wengi.
 
Wewe njoo Chauma sasahivi sio wali maharage,sasa ni biriani ya kuku.

Mzee Hashim Rungwe tuvushe mwamba tuvushe😅😂
 
Samia Vs Hashim Rungwe,na bado CCM wataiba kura ili wamshinde
 
Ingawa nilianza kupiga kura mwaka 2000, lakini sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.

Ingawa sina Chama, nilikuwa ninafurahia ninapoona ushindani wa kisera kati ya CCM na CHADEMA! Kwa bahati mbaya, mpaka sasa hakuna uhakika wa CHADEMA kushiriki uchaguzi wa mwaka huu.

Vyama vinavyotajwatajwa kwa sasa ukiacha CHADEMA, ni ACT WAZALENDO na CHAUMA! Lakini mimi nikiviangalia, sioni kama ni vyama vya siasa vibavyotanguliza mbele maslahi ya nchi. Ni kama vile vinafanya maigizo tu ama vinatumiwa na Chama tawala kwa manufaa yake!

Mtu unawezaje kukubali kushiriki uchaguzi ambao unafahamu ni mshindani wako ndiye mwenye uamuzi wa mwisho juu ya matokeo?

Mtu unakubalije kushiriki uchaguzi ambao unaona wazi kabisa kuwa hauna maslahi kwa Taifa? Ubunge na udiwani ni bora kuliko matakwa ya wananchi?

Kuna anayeweza kunishawishi niwaamini akina ZITTO KABWE, JOHN MREMA, SALUM MWALIMU, n.k?
Kuwaamini kwako au kutowaamini hakujawahi kuwa na maana kwao; we endelea kumuamini lissu na tone tone yake.
 
Ni CCM B n CCM C..hata Mzee wa Mpox anajua ndio maana havitaji wala kuvisakama asilani
 
Nakupa mbinu, ukiona chama chochote cha upinzani kila mara kinapambana kuonesha wanachama wa CHADEMA, jua kabisa hicho ni chama cha kimkakati.​
 
Act na chauma ni mtu na mdogo wake,

ACT kaachishwa ziwa,saivi chauma ananyonya,ndo last born
 
Vyama vya siasa vyote vilikuwa ccm B kwasasa uwepo wa Lissu ccm imepata mpinzani wa kweli.

Halafu ccm inaongozwa na kiongozi mwepesi sana huu mwaka huu ccm byeee🤣
Na Lisu pamoja na wenzake walishiriki kikamilifu kumuengua Dr Silaa na kumpokea hayati ENL kisha wakampa ugombea uraisi (kumbuka ni hawahawa Lisu na wenzake akiwemo asiyesahaulika Kubenea walimchafua ENL kama fisadi la mafisadi).

Hivi unapata wapi nguvu ya kumwamini mwanasiasa?
 
Dr Slaa alikuwa anatumika na CCM alipokuja Lowassa aliona siri yake itatoka ndio maana aliamua kuondoka mwenyewe.

Lissu na wenziwe kweli walikuwa wakimkosoa Lowassa lakini tatizo sio Lowassa ni ccm kuwepo madarakani ndio tatizo.

Unaweza ungana na adui yako kwa muda kuondoa tatizo kubwa halafu mkamalizana wenyewe kwa njia mutakayo ijua wenyewe.
 
Basi, naishia hapa
 
Back
Top Bottom