Mbona kama nashindwa kufanya Diet! Wakuu mnawezaje?

Nawezaje kuepuka ugali
Nawezaje kuepuka wali

Maisha ya kigeto kgeto
Ugali una wanga ambao ni hatari
Wali una sukari ambayo ni hatari Sasa ntafanyaje mana migahawani hakuna diet wenzangu mnawezaje?
Kula Viazi,kula ugali wa Dona,kula wali,Fanya mazoezi,kula matunda,kula mbogamboga,kunywa maji mengi Hasa ya mboto!
 
usinywe soda ya aina yeyote wewe usile nyama na samaki .......Anza na ivyo kwanza ndio utajua maana ya diet
 
KAbla ya kwenda huko kwenye kufanya diet hebu tusaidie hapa kaka.
1. Umeoa?
2. Una umri gani?
3. Why unataka kufanya diet
4. Unajishughulisha na nini?
5. Unafanya mazoezi?

Diet hufanyi tu bila sababu. Unaweza kujiletea madhara ya kiafya
Sijaona
Nina 25 years
Nataka kufanya diet ili kuepuka magonjwa yasio ya kuambukizwa kama pressure kisukari na kansa
Ndio nafanya mazoezi

Naomba muongozo
 
Nawezaje kuepuka ugali
Nawezaje kuepuka wali

Maisha ya kigeto kgeto
Ugali una wanga ambao ni hatari
Wali una sukari ambayo ni hatari Sasa ntafanyaje mana migahawani hakuna diet wenzangu mnawezaje?
Nilipewa ushauri mzuri miezi kadhaa iliyopita, angalia labda utapata cha kukusaidia.

Nawezaje kuepuka ugali
Nawezaje kuepuka wali

Maisha ya kigeto kgeto
Ugali una wanga ambao ni hatari
Wali una sukari ambayo ni hatari Sasa ntafanyaje mana migahawani hakuna diet wenzangu mnawezaje?

Mfumo wa chakula wangu ni hivi
Kila siku nakula mara moja tu,

Saa Saba mchana
Nakula mara kwa mara ndizi na nyama kwa pamoja na nusu Lita ya mtindi.
Yani ndizi mixer nyama Nazi na vingine.

Nina uzito wa kilo 85
Urefu wangu ni 6.6 Ft

Nipeni muongozo Zaidi.
 
Wewe hujaelewa.
Wewe hutakiwi kuacha kula hivyo vitu. Unatakiwa kula kwa kiasi.
Fanya kwa kiasi. Kila jambo fanya kwa kiasi
 
Nawezaje kuepuka ugali
Nawezaje kuepuka wali

Maisha ya kigeto kgeto
Ugali una wanga ambao ni hatari
Wali una sukari ambayo ni hatari Sasa ntafanyaje mana migahawani hakuna diet wenzangu mnawezaje?
Ki-Tanzania ni vigumu kuepuka vyakula vya wanga kama vile Ugali, wali, viazi, mihogo n.k.

Vitu vya kufanya :-

Epuka kula kila muda. Endapo una Njaa, Tenga muda maalumu kwaajili ya kula na ukashiba sio kuonja onja mfano Chakula cha mchana na Usiku.

Tumia matunda ya msimu na epuka kula mchanganyiko wa matunda mengi kwa wakati mmoja, kula Tunda la aina moja kwa wakati moja.

Epuka kula Asubuhi, fiziologia ya Binadamu haikubaliani na Kula asubuhi mara baada ya kuamka. Unaweza kula muda wowote kuanzia mchana saa 6 mchana hadi Jua linapozama saa 12 jioni au 1 usiku. Ikikushinda sana mwisho saa 2 Usiku.

Kunywa maji ya kutosha Asubuhi na wakati unasikia Njaa au hamu ya kula nje ya muda wa kula.

Fanya mazoezi ya mwili mara 3 mpaka 4 kwa wiki kulingana na ratiba yako, Mapumziko ni muhimu kama ilivyo kwa mazoezi.

Unaweza kuchagua kutumia kanuni hii A:N. Ambapo A ni muda wa kutokula(fasting) na N ni muda unaoweza kula(Feasting). Chagua 16:8 au 18:6 zinafaa Ki-Tanzania. Mfano kama ni 16:8 unakula lunch saa 6 mchana basi supper ni saa 2 usiku. Kama ni 18:6 utakula lunch saa 6 mchana na supper saa 12 Jioni au utakula lunch saa 8 mchana na supper 2 usiku.

Punguza mawazo na hofu kuhusu vyakula, Muhimu ni mwili Upate wakati wa kufanya marekebisho na matengenezo yaani Wakati bila chakula. Mwili unapokuwa na chakula Tumboni hujikita katika umeng'enyaji wa chakula kilichopo na huahirisha shughuli nyingine kama matengenezo na marekebisho ya mwili mfano kuimarisha kinga, kuondoa sumu zitokanazo na vyakula na shughuli nyingine n.k.

Mwili wa Binadamu unaweza kujitibu pekee yake, Muhimu ni kuupatia Muda wa kufanya kazi hiyo.

Relax, Don't complicate, Avoid Obsession and Goodluck Lad.
 
Nashukuru sana mkuu
Mungu akubariki Zaidi.
 
Kama hauko overweight au obese kula tu kila kitu, cha muhimu fanya mazoezi. Wewe bado mdogo achana na mambo ya Janabi mpaka ufike 35 angalau
 
Siku 3 za mwanzo ni ngumu sana, baada ya hapo ni rahisi, Nina mwaka 5 sasa nakula mlo mmoja tu saa 10 jioni ( kasoro weekend )
 
Mfumo wa chakula wangu ni hivi
Kila siku nakula mara moja tu,

Saa Saba mchana
Nakula mara kwa mara ndizi na nyama kwa pamoja na nusu Lita ya mtindi.
Yani ndizi mixer nyama Nazi na vingine.

Nina uzito wa kilo 85
Urefu wangu ni 6.6 Ft

Nipeni muongozo Zaidi.
Yani unakula mara moja kwa siku na bado unataka kufanya diet.

Kijana wa miaka 25 unataka usile wanga au sukari ukifika 40 si utakua ukitembea unayumba yumba. Na ukioa mke si utakua unamwekea mkono tu?

Kula kijana, fanya mazoezi endelea na maisha.
 
Mimi nikitafuta kuongeza uzito nyie mnapunguza duuh,, 🤔

Afu wewe nipo dar usitutanie Juzi ulisema ushaanza kufubaa mara kupauka umekaa kwenye kiyoyozi mara hii
 
Back
Top Bottom