Mbona hakuna mabadiliko ya maisha

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,357
6,422
Nimekuwa nikifuatilia mienendo ya watanzania kumshangilia Mh kila analolifanya. Strange maisha ndiyo yanazidi kuwa ya shida. Jana nimepita hospitali, rushwa ndio imepamba moto.

Barabarani usiseme. Mnashangilia nini? Ni ile ya tukose wote, ni wivu wa sisi masikini;

Nimekuja kugundua na wala siyo kuwa masikini wanashangilia (masikini wanaoshangilia) kuwa tunaelekea kuzuri. Tatizo la sisi masikini tukiona tajiri kaporomoka, tunapata usingizi mzuri kama vile tumepata nafuu ya maisha.

Wanashangilia Kabwe kaangushwa, of what direct benefit to you from today!
 
Yaani sijui watz wamelishwa unga gani. Ili uyaone mabadiliko ya sera za uchumi bora yaone kwanza mfukoni mwako na kisha kwenye familia yako. Huku kushangilia wanaotumbuliwa bila kujua kuwa wamepewa likizo ya kwenda kutumia na kutumbua walichochota ni uzuzu! Hebu badilikeni kwa kuona mnavyozugwa na wanasiasa.
 
Yaani sijui watz wamelishwa unga gani. Ili uyaone mabadiliko ya sera za uchumi bora yaone kwanza mfukoni mwako na kisha kwenye familia yako. Huku kushangilia wanaotumbuliwa bila kujua kuwa wamepewa likizo ya kwenda kutumia na kutumbua walichochota ni uzuzu! Hebu badilikeni kwa kuona mnavyozugwa na wanasiasa.
Watanzania wenzangu wanatia kinyaa, wale wanaoshangilia upupu bila tafakuli ya kina.
 
Miezi 6 unataka mabadiliko, je ukifuga Ng'ombe, unahitajika muda gani kumkamua maziwa, hivyo mipango inafanywa kuwa mpole mkuu
 
Enzi za Nyerere kipindi waziri mkuu Sokoine
hali ilikuwa kama hivi
watu wanaruka ruka kwa furaha wakisikia walanguzi wamekamatwa
hawajiulizi why unga na sigara viwe adimu hadi kuwepo walanguzi....

na bado wapo watu wanakwambia hakuna kama Sokoine....

taifa zima tunajikunyata jioni kusikiliza Nyerere leo kaongea nini
umasikini ulipamba moto
enzi hizo msichana akivaa suruali mtaa mzima mnatoka kumtazama

Akaja Mwinyi akafungua milango..watu wakajua TV
wakajua fashion
wakajua kununua vyakula na kuweka ndani kwenye friji

still watu hao hao wanakwambia Sokoine alikuwa bonge la kiongozi
Mwinyi hawamtaji.....

Hii ya Magufuli kutumbua majipu itavuma kwa mda mrefu
hata asipokuwepo Magufuli watasema 'angekuwepo Magufuli' angewatumbua

hata kama utumbuaji wenyewe una walakini nyingi....lakini ndo hivyo...
ndo watanzania hao
 
Enzi za Nyerere kipindi waziri mkuu Sokoine
hali ilikuwa kama hivi
watu wanaruka ruka kwa furaha wakisikia walanguzi wamekamatwa
hawajiulizi why unga na sigara viwe adimu hadi kuwepo walanguzi....

na bado wapo watu wanakwambia hakuna kama Sokoine....

taifa zima tunajikunyata jioni kusikiliza Nyerere leo kaongea nini
umasikini ulipamba moto
enzi hizo msichana akivaa suruali mtaa mzima mnatoka kumtazama

Akaja Mwinyi akafungua milango..watu wakajua TV
wakajua fashion
wakajua kununua vyakula na kuweka ndani kwenye friji

still watu hao hao wanakwambia Sokoine alikuwa bonge la kiongozi
Mwinyi hawamtaji.....

Hii ya Magufuli kutumbua majipu itavuma kwa mda mrefu
hata asipokuwepo Magufuli watasema 'angekuwepo Magufuli' angewatumbua

hata kama utumbuaji wenyewe una walakini nyingi....lakini ndo hivyo...
ndo watanzania hao
Nashukuru umenisoma. Watu tunakuwa wepesi wa kusahau! Nyerere alisema tufunge mikanda, nina uhakika yeye na wanaomzunguka hawakuwahi kukosa sabuni, dawa ya mswaki , nguo etc. Watanzania tukashangilia lakini walio na akili waliona kukosea kukubwa kwa Nyerere. Leo wanashangilia kila cha mtukufu anachokifanya hata kama kina dosari za wazi!
 
Nimekuwa nikifuatilia mienendo ya watanzania kumshangilia Mh kila analolifanya. Strange maisha ndiyo yanazidi kuwa ya shida. Jana nimepita hospitali, rushwa ndio imepamba moto. Barabarani usiseme. Mnashangilia nini? Ni ile ya TUKOSE WOTE, NI WIVU wa sisi masikini; nimekuja kugundua na wala siyo kuwa masikini wanashangilia (masikini wanaoshangilia) kuwa tunaeleke kuzuri. Tatizo la sisi masikini tukiona tajiri kaporomoka, tunapata usingizi mzuri kama vile tumepata nafuu ya maisha. Wanashangilia Kabwe kaangushwa, of what direct benefit to you from today!
Watanzania wengi wana roho mbaya na wanafiki, wanaangalia maisha ya wengine sio ya kwao, ndio maana mpaka sasa sehemu nyingi hawajaendelea kwa sababu hata ukienda likizo na suruali mpia unalogwa, ukijenga wanaloga,ukiwapa kazi hawafanyi bali wanataka pesa, hatutaki majizi na washikwe lakini waweke mifumo na sheria rafiki ili watu waweze kufanya biashara wanajua kuwa wao wenyewe ndio wameharibu kwa manufaa yao kwa nini kuwatesa watz ambao wanakesha usiku na mchana kutafuta pesa, weka sheri ya kodi iwe wazi ondoa makadirio ya kodi bali fuata inivoice au risiti ya manunuzi na ondoa kodi lukuki ambazo hazifai, hao masikini wanaoshangilia siku zinahesabika wataanza kulia
 
Kilio kilio kilio kila kona twende wap jamani? Au tukimbilie Kenya yeuwiiiiiiiiie auwiiiiiiiiie yeuwiiiiiiiie jaman nife au nibaki?
 
VIPI ARIFU..... UNATAKA UOKOTE MANA KAMA WAYAHUDI NDO UAMINI KUNA MABADILIKO. PIGA KAZI.
 
hali si shwari mtaani kila kona njaa, pesa haipatikani aisee sijui wameificha wapi ? kila kitu bei juu dollar nayo inaanza kushika helm tena, watawala wako busy kutumbua wanaitana majipu siku hizi, wakishatumbua wanaitana kwenye corridor wanaambizana usihofu nitakupangia kazi nyingine kale bata kwanza mwanangu.
huku kwetu tunalia unaweza ukafa njaa chakula unakiona kisa kila unapoingiza mfukoni unakutana na vumbi lililojaa kila aina ya ghadhabu ya kupotea kwa kura yako mabadiliko hayaonekani.

wapo wanaoshangilia et kisa mtu katumbuliwa ila wanashangilia umaskini kuendelea kunenepa kwa sababu mtumbuaji hana nyembe ya kutumbuliamajirani waliozoea kutuazima wamefunga milango hawataki kusikia kila siku tunaazima halafu tunarudisha tukiwasimanga.

tuende wapi jamani kurudi kijijini nauli juu, nitembee kwa miguu ? watasema ni mzururaji na ombaomba hawataki mtu aombe siku hizi ati ataiba serious?

siku hizi hawataki hata tuwasikie wale jamaa kule kwenye nyumba ya fujo wanasema tufanye kazi tu halafu watatafuta muda wa kutuhadithia tukiwa tumepumzika saa nne usiku!!! si tutakuwa tumechoka pamoja na njaa zetu ? wanauhakika tutakuwa hatujalala kweli?
 
kubadilisha maisha ya waafrika katika nchi masikin kama Tanzania si suala la kukurupuka, linahitaji viongozi imara na ambao hawana woga ktk kutetea masilahi ya Taifa, tushukuru mungu tumepata Rais anaeonekana mwenye nia kama hiyo. ufisadi ktkt nchi za kiafrika ndo jambo kubwa linarudisha nyuma maendeleo ya taifa mheshimiwa hajakosea kuanza na suala hili, cha muhimu ni kumuunga mkono Mr.President. Maendeleo sio jambo la kulala usiku ukiamka asubuhi unakuta maendeleo, bali nchi kama yetu hii ambayo kuna mnyoror mrefu ambao umesukwa tangu kipindi hicho na wajanjawajanja ambao wako kwa ajili ya kujinufaisha wenyewe na matumbo yao lazima ufunguliwe ili pato la Taifa hata mtu wa hali ya chini aweze kunufaika nalo na aweze kuliona, hiyo ndo kazi ya magufuli aliyoanza nayo. Cha muhimu ni tuwe wavumilivu huku tukimuombea Mr.President akamilishe kazi yake baadae tutakuja kuona matunda hata kwa yule mzee aliyejichokea kule kijijini.
 
Back
Top Bottom