Mbona CCM na Magufuli hawazungumzii Utajiri wa Gesi? Sababu ni sawa na kuwa na mafuta kwa waarabu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,883
Nchi hii nawaza hadi kichwa kinauma ila yote kheri ndo nchi yangu.

Kwanini katika mambo yote siwasikii CCM wala Rais Magufuli akisema juu ya utajiri wa nchi hii hasa baada ya kugundua utajiri adimu wa gesi toka mtwara.

Kuwa na gesi ni sawasawa kabisa na utajiri wa mafuta kwa baadhi ya nchi za kiarabu ambao kwa kutumia mafuta wameweza hadi kugeuza jangwa kuwa shamba la kilimo. Wamehamisha bahari na kufanya ujenzi mkubwa wa vitega uchumi na utalii.

Kwa pesa hizo hizo wamehamisha mbuga zetu na kutengeneza zao na watalii kumiminika kwebda kuona wanyama kwao.

Katika kampeni na bunge lililopita tuliambiwa kwa utajiri wa gesi tulionao ni zaidi ya utajiri wa nchi zinazozalisha maguta.

1. Mbona kwenye mapato ya nchi hatuoni gesi imezalisha kiasi gani?
2. Mbona bajeti pendekezwa 2017/18 hakuna mapato yatokanayo na gesi yetu.
3. Au Tanzania tuna gesi ambayo ni "hewa" maana tunawatumishi hewa bila shaka tunaweza kuwa na gesi hewa.
4. Mbona rais na serikali yake katika yote hii huwa hawasemi? Au mikataba ishatufunga midomo kama madini tunapata mrahaba tu wa 0.00000001%

Naombeni majibu
 
Cha ajabu wanahangaika na mchanga wa Dhahabu migodini wana acha gesi ambayo bado ina muda mrefu kutumika,inadaiwa migodi ya dhahabu ina chini ya miaka ishirini ifungwe

Gesi ndio Kwanzaa!! Na huko ndiko hasira zilitakiwa zielekezwe

Nchi inahangaika kukopa ijenge uwanja wa ndege mtwara wakati hapo jirani kuna matrilioni
 
Mkuu biashara ya gesi sio kama kuuza juice.Makampuni mengi yamefungwa kwa kukosa mtaji ndio maana husikii hayo mambo.Kwanza uchumi wa gesi ulitetereka kidunia; pia mkumbuke gesi yetu nyingi ni kutoka majini; hiyo ni gharama
 
Acheni utapeli maneno mnayoyasema kwenye madini ndo mnayaleta kwenye gesi. Wengine wanachimbaje?
 
Zile sheria zilizopitishwa kwa hati ya dharura zinasemaje. Pengine hizo ndio zinaweza tupa mwelekeo wa kile tunachoweza kipata kwenye gesi. Kama ni mrahaba au vinginevyo.
 
Bora tungeacha kuharibu mazaliya ya samaki kwa kitu ambacho hakitulipi.
Kwenye madini tungeacha watu walime tu badala ya kuambulia mishimo!
 
Kikwete alisema yeye ndiye Rais wa mwisho kuongoza Tanzania maskini. Hali haionyeshi hivyo mpaka sasa.
 
Haihitajiki rocket science ili kupata maendeleo kutokana na raslimali za asili. Tatizo kubwa ni mawazo kwamba inahitajika hiyo.
 
Nchi hii nawaza hadi kichwa kinauma ila yote kheri ndo nchi yangu.

Kwanini katika mambo yote siwasikii CCM wala Rais Magufuli akisema juu ya utajiri wa nchi hii hasa baada ya kugundua utajiri adimu wa gesi toka mtwara.

Kuwa na gesi ni sawasawa kabisa na utajiri wa mafuta kwa baadhi ya nchi za kiarabu ambao kwa kutumia mafuta wameweza hadi kugeuza jangwa kuwa shamba la kilimo. Wamehamisha bahari na kufanya ujenzi mkubwa wa vitega uchumi na utalii.

Kwa pesa hizo hizo wamehamisha mbuga zetu na kutengeneza zao na watalii kumiminika kwebda kuona wanyama kwao.

Katika kampeni na bunge lililopita tuliambiwa kwa utajiri wa gesi tulionao ni zaidi ya utajiri wa nchi zinazozalisha maguta.

1. Mbona kwenye mapato ya nchi hatuoni gesi imezalisha kiasi gani?
2. Mbona bajeti pendekezwa 2017/18 hakuna mapato yatokanayo na gesi yetu.
3. Au Tanzania tuna gesi ambayo ni "hewa" maana tunawatumishi hewa bila shaka tunaweza kuwa na gesi hewa.
4. Mbona rais na serikali yake katika yote hii huwa hawasemi? Au mikataba ishatufunga midomo kama madini tunapata mrahaba tu wa 0.00000001%

Naombeni majibu

Mkuu :Return Of Undertaker!
Tafuta kazi ya kufanya hiyo dhahabu tunayoundia tume sio ya Watanzania tunaambulia mrahaba wa 4% kuna watu wameweka akili za Wadanganyika mfukoni eti wanalipa corporate tax lakini ukweli ni kwamba ukiwa smart you don't pay anything kama kodi hata hiyo VAT ni interim kwani if you compute its a pass through cost which cancels itself. Aliwahi kusema Jakaya Kikwete development ya mine it's endelevu na kulipa kdoi ni ndoto. Ndio maana Marehemu Nyerere alikataa kuruhusu makampuni ya Mabepari kuchimba dhahabu. CCM ni wezi waliingizwa choo cha kike awamu ya Mkapa!kwa kifupu Dhahabu ni ya wawekezaji zaidi ya ajira kwa watu wachache na ujira usiojulikana au kudhibitiwa na Wizara ya Kazi hakuna kitu. Kwenye Gesi Asilia ndio kuna majanga Gesi sio ya Watanzania ! Makampuni yaliyochimba visima vya Gesi asilia ndio wamiliki na bei ya kuuza kwa TPDC wanaamua wenyewe ili kulipa gharama zao za uwekezaji kwa hiyo endelea kulia tu kufaidi gesi asilia ni sawa na kutarajia kifaranga wa kuku anyonye! Bila kuachana na CCM kufaidi Gesi au Dhahabu ni ndoto za alinacha and it will take over 100 years! Kazi kwenu!
 
Hujasikia waziri kishaanza kuwalaumu watu wake Wa idara ya sheria?Kwa mikataba mibovu?kilimo kwanza,gesi ilikua awamu ile na sasa ni viwanda hewa
 
"...Kitengo cha sheria hapa Wizarani ndio mwiba na chanzo cha matatizo yote ya Wizara, wameingia mikataba mibovu isiyo na faida..."

Waziri Sospeter Mhongo
Leo, Aprili 12

Huwezi jua inaweza kuwa hadi kwenye gesi tushachezewa akili.
Gesi inazidi kupanda kuliko hata kwa nchi ambazo hazina gesi.
 
[QUOTENanirrytz, post: 20638717, member: 112987"]"...Kitengo cha sheria hapa Wizarani ndio mwiba na chanzo cha matatizo yote ya Wizara, wameingia mikataba mibovu isiyo na faida..."

Waziri Sospeter Mhongo
Leo, Aprili 12

Huwezi jua inaweza kuwa hadi kwenye gesi tushachezewa akili.
Gesi inazidi kupanda kuliko hata kwa nchi ambazo hazina gesi.[/QUOTE]
Kwani nani alikuwa boss wa sheria hapo wizarani
 
JK aliingia mikataba 17 kwa mara moja na wachina juu ya gesi kwa manufaa yake na familia yake. Gesi ishauzwa mkuu, ndiyo maana jpm hawezi kuongelea gesi ya watu binafsi.
 
Mkuu biashara ya gesi sio kama kuuza juice.Makampuni mengi yamefungwa kwa kukosa mtaji ndio maana husikii hayo mambo.Kwanza uchumi wa gesi ulitetereka kidunia; pia mkumbuke gesi yetu nyingi ni kutoka majini; hiyo ni gharama
Some people don't understand issues...wanaongea kisiasa. Thanks for clarification. Bei ya mafuta imeshuka sana, ikiwemo gas. Is it viable to extract it is a subject of many discussions among the investors.

Sisi wengine tunafikiri ni biashara ya korosho

Pooor us
 
Acheni utapeli maneno mnayoyasema kwenye madini ndo mnayaleta kwenye gesi. Wengine wanachimbaje?
Ushawahi kufanya biashara ya aina hiyo au biashara yoyote? Uliifanyaje?

Bei za mafuta zimeshuka sana...kuwekeza kunahitaji kijiridhisha vyakutosha.

Sio biashara ya njugu ati
 
Nadhani ndo umetua na ndege kutoka utokako pole kwa safari ndefu tengewa maji ukaoge then chukua sm yako.

Ingia millad ayo magazet soma headline za magazet yote kuanzia siku umesafir had leo.

Jiridhishe mwenyewe kuwa ni kipi kimepewa kipaumbele kwenye mijadala mbalimbali.

Mpaka bunge limeacha hizo mada zako za msingi na zenye manufaa kwa jamii.

Pole na karibu bongo.
 
Back
Top Bottom