Mbona Arusha peke yake?!!

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
32,662
59,798
Hivi ni hisia zangu tu au kuna ukweli ktk hili? Nimeona safari za Raisi na Waziri Mkuu ktk mkoa wa Arusha zimekuwa nyingi mno. Imefikia wakati akiondoka Waziri Mkuu, basi Raisi naye anaingia.

Jamani mbona mikoa mingine haipati baraka za ziara za Raisi na Waziri Mkuu kiasi hicho? Hata hapo Morogoro tu.

Suala lingine ni hizi harambee za hospitali na mashule. Hatupati habari toka mikoa mingine isipokuwa Arusha. Jamani, how about Lindi,Mtwara,Rukwa,Iringa,Kigoma,Kagera,Mara,Mwanza....?

Je, ni ukosefu wa habari toka mikoa hiyo, au hakuna kinachoendelea? Jamani naomba ufafanuzi na michango yenu.
 
Nadhani kuna kinachoendelea katika hiyo mikoa unayozungumzia,,,,kama Mwanza nadhani alikuwepo siku si nyingi na kama unakumbuka EL alikuwa huko akaulizwa maswali 'magumu' na watoto wa shule hadi akashindwa kujibu

Jambo jingine ni kwamba kuna mikoa ambayo hali yake kisiasa mara kwa mara ni 'tete', lolote laweze kutokea so lazima awepo kucheki mambo yanakuwaje..si unakumbuka apo AR juzi kuna 'kiini macho' kimetokea cha watu kukamatwa na vijana wa Hosea wakiwa kwenye mkao wa rushwa? Si umesikia kama kumetokea mgawanyiko? Lazima akapoze mambo

na kuhus hospitali nk, si ndo hao maaskofu waliosema kachaguliwa na Mungu? ndo lazima akashiriki kwenye harambee na mwengineyo...ebo! nani kasema kuna mtu anafanya kazi ya bure hapa?
 
Kwa mlolongo huu anzisheni THREAD ZA KUDUMU za JK na Nyingine ya EL...

Maana kila Thread JK na nyingi EL.... Kwa wao ndio miungu yetu,,, kwani bila wao hatuwezi endeleea!!!

Ebbboooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
acha kulialia damn it..

if you dont like it anzisha website yako na uiite

" nothreadszaEL&JKcoztheyaresmallgods.com "

badala ya kuanza kulazimisha watu cha kufanya hapa... mbona umeanza amri kama za lowasa? by the way kasungura kamewatosha?
 
Kwa mlolongo huu anzisheni THREAD ZA KUDUMU za JK na Nyingine ya EL...

Maana kila Thread JK na nyingi EL.... Kwa wao ndio miungu yetu,,, kwani bila wao hatuwezi endeleea!!!

Ebbboooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

mkuu hawa ndio manahodha wetu mkuu wanaweza peleka jahazi kokote na ndio tumewakabidhi nchi hii sasa ndio maana unaona issue nyingi hapa zinawahusu. Pia toka wakati wa kampeni na jamaa alipoingia madarakani tuu hata vyombo vya habazi kuanzia ukurasa wambele hadi ukurasa wa michezo ilikuwa ni JK na El tuu. Si unakumbuka hapa hadi timu ya taifa ilibadilishwa jina na kupewa jina la JK boyz? Anyway wao ndio wamebeba thamani ya watanzania mkuu may bee ianzishwe sehemu ya kuwajadili viongozi wa juu wa nchi na nadhani itaangukia huku huku tuu.
 
Arusha kwa sasa hivi na Mwanza ndio kwenye hisa za wahujumu wa uchumi kwa hiyo ni lazima waende huko. Jiulize waende Morogoro kuna nini? Waulize TAKUKURU kilichowafanya wawashike Kondoa na si kwenye mafia.

Hebu angalia Arusha - mtalii analipa $100,000.00 kwa safari moja ya kuja kuwinda, Ngurdoto vyumba bei yake ya kutisha na nani wanakaa huko? Huko ndio kwenye maneno.

Nenda ukanda wa ziwa Mwanza - Barrick wakishirikiana na mafisadi wazawa kutudhulumu rasilimali zetu kwa bei poa, Mkataba bomu wa Buzwagi n.k. Need I say more?
 
Hivi ni hisia zangu tu au kuna ukweli ktk hili? Nimeona safari za Raisi na Waziri Mkuu ktk mkoa wa Arusha zimekuwa nyingi mno. Imefikia wakati akiondoka Waziri Mkuu, basi Raisi naye anaingia.

Jamani mbona mikoa mingine haipati baraka za ziara za Raisi na Waziri Mkuu kiasi hicho? Hata hapo Morogoro tu.

Suala lingine ni hizi harambee za hospitali na mashule. Hatupati habari toka mikoa mingine isipokuwa Arusha. Jamani, how about Lindi,Mtwara,Rukwa,Iringa,Kigoma,Kagera,Mara,Mwanza....?

Je, ni ukosefu wa habari toka mikoa hiyo, au hakuna kinachoendelea? Jamani naomba ufafanuzi na michango yenu.
Dah kweli kila zama na kitabu chake. Enzi za jiwe kanda ya Kaskazini alikuwa haitaki kabisa.
 
Hivi ni hisia zangu tu au kuna ukweli ktk hili? Nimeona safari za Raisi na Waziri Mkuu ktk mkoa wa Arusha zimekuwa nyingi mno. Imefikia wakati akiondoka Waziri Mkuu, basi Raisi naye anaingia.

Jamani mbona mikoa mingine haipati baraka za ziara za Raisi na Waziri Mkuu kiasi hicho? Hata hapo Morogoro tu.

Suala lingine ni hizi harambee za hospitali na mashule. Hatupati habari toka mikoa mingine isipokuwa Arusha. Jamani, how about Lindi,Mtwara,Rukwa,Iringa,Kigoma,Kagera,Mara,Mwanza....?

Je, ni ukosefu wa habari toka mikoa hiyo, au hakuna kinachoendelea? Jamani naomba ufafanuzi na michango yenu.
ukiona hivo ujue hao viongozi ni wamewekeza au wanataka wawekeze mali zao binafsi huko Arusha.
 
Back
Top Bottom