Mboga za makaburini

Lima bustani nyumbani mdau ,ila pole sana nimekusikitikia na kuumia mno maana ni kama ulikuwa unakula minofu ya wafu .
Nasema pole tena aisee
Watu wanawaza biashara na pesa tu badala ya afya zetu. Kujilimia mwenyewe nyumbani ndio suluhisho pekee lililobaki kwa sasa, vinginevyo tunaendelea kulishwa magonjwa mchana kweupe
 
Unapanda kama unavyopanda maua kuzunguka nyumba yako tu , nunua mifuko ya cement jazaa udongo na mbolea weka mboga ,mwagilia polepole ndani ya wiki 3 unakula mboga zako na nyanya fresh kabisa.
Duhh, ushauri mzuri japo siwezi kuufanyia kazi! Inapendeza uwe na kwako ununue mifuko mingii upande zile mbegu! Sijui viwanja shingapi saizi😁
 
Gentleman,
Sisi ni mavumbi na mavumbini tutarudi,

Mwenyezi Mungu anatulinda waja wake kwa mengi sana, hasa watu waishio mijini. Hilo umegundua kwenye mboga tu, sijui ukigundua kwenye mtandao wa maji safi na salama ya bomba, jinsi mtandao ulivyopita kwenye chemba za maji taka, zinavovuja mpaka zije kugunduliwa watu wamesha kunywa na kutumia kinyesi kwa muda mrefu sana na wako vizuri tu.

Lakini pia,
hata maji ya kumwagilia hizo mboga za majani umeshawahi kuyaona?
Maeneo mengi ni maji taka yanayoelekea panakostahili,

Ni muhimu sana kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake kwetu sote kwa yote 🐒
 
Duhh, ushauri mzuri japo siwezi kuufanyia kazi! Inapendeza uwe na kwako ununue mifuko mingii upande zile mbegu! Sijui viwanja shingapi saizi😁
Unapo kaa ndio kwako , unapokaa ukipatumia vizuri panakuokolea pesa nyingi sana , ukingia youtube unajifunza njia nyingi sana za kurahisisha maisha kwa kujifunza njia za kuzalisha mboga , samaki na nk kwenye eneo dogo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…