Mbio za Urais,Mwigulu anaendelea Kung'ara, Vijana wameyasema haya hapa

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
Nyota ya Mwigula yazidi kung'ara urais
*Vijana wataka chama chake kimpe nafasi

Claudia Kayombo

WAKATI vyama vya siasa havijatangaza majina ya wagombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, vijana mbalimbali wameanza kutoa maoni ya nani anafaa kumrithi Rais Jakaya Kikwete.

Vijana wengi wamesema kuwa, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, ndiye anayestahili kumrithi Rais Kikwete kutokana na utendaji wake wa kazi.

Hatua ya vijana kumtaja Nchemba, ni mwendelezo wa malumbano yanayoshika kazi nchini na kwamba, ni mzee au kijana ndiye anayefaa kumrithi rais anayemaliza muda wake.

Katika mahojiano yaliyofanywa na gazeti hili Dar es Salaam jana kwa nyakati tofauti na baadhi ya vijana walimtaja Nchemba kuwa, ndiye anayestahili akifuatiwa na William Ngereja na Januari Makamba ambaye anashika nafasi ya tatu.

Dereva wa Selvas Maige mkazi wa Tegeta Dar es Salaam, alisema taifa kwa sasa linahitaji kiongozi mwenye kutoa maamuzi magumu dhidi ya mafisadi ili kukomesha tatizo hilo ambalo limekita mizizi nchini.

"Vijana tumechoka kula maharage (kuongozwa na wazee), kila siku, tunataka kuongozwa na damu changa yenye uchungu na nchi hii, ambaye atatoa maamuzi magumu dhidi ya mafisadi.

"Hawa wazee tunaowachagua hawana wanachofikiria zaidi ya kuwaachia urithi tu wajukuu zao, tunataka vijana wenye uchungu na taifa hili, wakatae rushwa, wawajibishe mafisadi," alisema.

Akifafanua, kwanini Nchemba anafaa kuwa Rais wa Tanzania, Maige alisema ni baada ya kuona utendaji wake hasiti kutoa maamuzi dhidi wa washukiwa wa ufisadi.

Alisema wakati wa sakata la ufisadi wa uchotwaji wa mabilioni ya fedha katika akaunti ya Escrow, Nchemba hakuonesha unafiki kwa kumwonea mtu aibu hata kama ni wa chama chake (CCM), bali alisimamia ukweli katika jambo hilo.

"Huyu jamaa hata wapinzani wenyewe wanamkubali, awali alipokuwa kiongozi wa chama pekee watu hawakumwelewa vizuri, lakini sasa imeonesha kuwa, ni mtu asiyekubali kulinda wezi," alisema.

Hata hivyo, alipohojiwa iwapo miongoni mwa wazee waadilifu ambao wakipewa urais wanaweza kufanya kazi kwa uadilifu, alimtaja Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.

"Tunamwona katika utendaji wake wa kazi kwamba, wanaotuhumiwa anawawajibisha kabla hajawaangalia usoni, huyu akipewa nchi anaweza kuongoza vizuri," alisema.

Mkazi wa Kivule jijini Dar es Salaam, Habibu Kujoka alisema taifa hili linahitaji kiongozi kijana mwenye maono ya mbalimbali, atayeweka mkazo kilimo bora cha kisasa na mapinduzi ya viwanda kama ilivyo dhamira ya Serikali kuwa ifikapo 2025, Tanzania iwe nchi yenye uchumi wa kati.

Kujoka alisema ni aibu taifa hili kuendelea kuitwa maskini wakati linazo rasilimali lukuki la kulifanya liwe lenye maendeleo endelevu.

"Tunataka rais kijana mwenye uwezo wa kuleta mapinduzi ya viwanda ambavyo vitafanya taifa kuinukia kiuchumi, lakini pia atakayewekea mkazo kilimo bora cha kisasa," alisema.

Mwanahabari, Rafael Malekele mkazi wa Ukonga Banana alisema ni dhamira ya vijana kupata rais kijana mwenzao mwenye maono ya kulifikisha taifa hili katika uchumi wa kati.

Pia, anayejali tamaduni ya nchi na mwenye uchungu na maskini wa mataifa hili, ambao wanahitaji mtu wa kuwatetea ili wawe na maisha mazuri.

Chanzo.Jambo leo
Tar.04.01.2015
 
Kwa hivyo chama chake kimwombe agombee au vipi, hivi ni muda gani umebaki mpaka hao CCM waanze mchakato wakuchuja wagombea wao. By now you'd expected all the candidates wawe wamesha julikana atleast na mikakati yao inajulikana wanataka kuwafanyia nini watanzania.

Katika viongozi waliotangaza nia so far January pekee ndio yupo clear the way things are done have to change sio ufisadi tu bali hata mbinu za kufanya kazi lazima zibadilike. Hao wengine naona wanachukua fomu tu na kukimbilia nyumba za ibada au labda wanategemea popular vote. Mwigulu kama anautaka uraisi ni wakati sasa na yeye kusema wazi sio indirect messages.

Hizi ndio ajabu zenyewe huko upinzani hakuna mgombea wa chama chochote mpaka dakika hii anaye julikana apart from the seasonal runner Maalim Seif ingawa ajasema lakini unajua siku ya form ikifika ataenda tu.
 
Mada za mwigulu ntaanza kuchangia kwa kuonesha msimamo mwezi wa tano.
 
Hatuhitaji mtunza mahesabu kama rais wa nchi, kwahiyo dogo akae miaka mingine kumi au ishirini akitafakari dira yake ya kutufikisha 'NEXT LEVEL'!

Nyota ya Mwigula yazidi kung'ara urais
*Vijana wataka chama chake kimpe nafasi

Claudia Kayombo

WAKATI vyama vya siasa havijatangaza majina ya wagombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, vijana mbalimbali wameanza kutoa maoni ya nani anafaa kumrithi Rais Jakaya Kikwete.

Vijana wengi wamesema kuwa, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, ndiye anayestahili kumrithi Rais Kikwete kutokana na utendaji wake wa kazi.

Hatua ya vijana kumtaja Nchemba, ni mwendelezo wa malumbano yanayoshika kazi nchini na kwamba, ni mzee au kijana ndiye anayefaa kumrithi rais anayemaliza muda wake.

Katika mahojiano yaliyofanywa na gazeti hili Dar es Salaam jana kwa nyakati tofauti na baadhi ya vijana walimtaja Nchemba kuwa, ndiye anayestahili akifuatiwa na William Ngereja na Januari Makamba ambaye anashika nafasi ya tatu.

Dereva wa Selvas Maige mkazi wa Tegeta Dar es Salaam, alisema taifa kwa sasa linahitaji kiongozi mwenye kutoa maamuzi magumu dhidi ya mafisadi ili kukomesha tatizo hilo ambalo limekita mizizi nchini.

"Vijana tumechoka kula maharage (kuongozwa na wazee), kila siku, tunataka kuongozwa na damu changa yenye uchungu na nchi hii, ambaye atatoa maamuzi magumu dhidi ya mafisadi.

"Hawa wazee tunaowachagua hawana wanachofikiria zaidi ya kuwaachia urithi tu wajukuu zao, tunataka vijana wenye uchungu na taifa hili, wakatae rushwa, wawajibishe mafisadi," alisema.

Akifafanua, kwanini Nchemba anafaa kuwa Rais wa Tanzania, Maige alisema ni baada ya kuona utendaji wake hasiti kutoa maamuzi dhidi wa washukiwa wa ufisadi.

Alisema wakati wa sakata la ufisadi wa uchotwaji wa mabilioni ya fedha katika akaunti ya Escrow, Nchemba hakuonesha unafiki kwa kumwonea mtu aibu hata kama ni wa chama chake (CCM), bali alisimamia ukweli katika jambo hilo.

"Huyu jamaa hata wapinzani wenyewe wanamkubali, awali alipokuwa kiongozi wa chama pekee watu hawakumwelewa vizuri, lakini sasa imeonesha kuwa, ni mtu asiyekubali kulinda wezi," alisema.

Hata hivyo, alipohojiwa iwapo miongoni mwa wazee waadilifu ambao wakipewa urais wanaweza kufanya kazi kwa uadilifu, alimtaja Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.

"Tunamwona katika utendaji wake wa kazi kwamba, wanaotuhumiwa anawawajibisha kabla hajawaangalia usoni, huyu akipewa nchi anaweza kuongoza vizuri," alisema.

Mkazi wa Kivule jijini Dar es Salaam, Habibu Kujoka alisema taifa hili linahitaji kiongozi kijana mwenye maono ya mbalimbali, atayeweka mkazo kilimo bora cha kisasa na mapinduzi ya viwanda kama ilivyo dhamira ya Serikali kuwa ifikapo 2025, Tanzania iwe nchi yenye uchumi wa kati.

Kujoka alisema ni aibu taifa hili kuendelea kuitwa maskini wakati linazo rasilimali lukuki la kulifanya liwe lenye maendeleo endelevu.

"Tunataka rais kijana mwenye uwezo wa kuleta mapinduzi ya viwanda ambavyo vitafanya taifa kuinukia kiuchumi, lakini pia atakayewekea mkazo kilimo bora cha kisasa," alisema.

Mwanahabari, Rafael Malekele mkazi wa Ukonga Banana alisema ni dhamira ya vijana kupata rais kijana mwenzao mwenye maono ya kulifikisha taifa hili katika uchumi wa kati.

Pia, anayejali tamaduni ya nchi na mwenye uchungu na maskini wa mataifa hili, ambao wanahitaji mtu wa kuwatetea ili wawe na maisha mazuri.

Chanzo.Jambo leo
Tar.04.01.2015

Uhoro mtupu. Eti vijana wengi. Wengi wakutoka china au! Wapiga kura ndo sisi. Yan ninyi mnaohongwa na hao wasaka tonge ndo mnaojifanya eti vijana wengi? Shindweni kabisaa. Chochote alichowahi kuonesha mwigulu siku za karibuni kinachoonesha postives ni kwa ajili ya kusaka tonge la urais tu na sio vinginevyo. Mbona tokea hapo hakuwahi kuonekana akiwapiga vita mafisafi! Kwan mafisadi wameanzia lwa sakata la escrow tu? Wanafiki tu. Ccm hamna aliye okoka. Ukiwa ccm huwez kuokoka labfa uhame. Kikwete alikuja kwa lasi hi hi ya ari mpya na mguvu mpya lakini leo yupo wapi!!? Tafakari chukua hatua.
 
Hivi we TUNTEMEKE bado tu mpaka leo unatumika? Mi ninavyojua OilChafu cannot be used anymore as lubricant...!!
 
Last edited by a moderator:
Kilichonivutia sio habari bali I'd ya mleta mada TUNTEMEKE ndio upo kambi hiyo kwa sasa.?

Kambi ya Nyepesi umeitelekeza.?
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom