Mbio za Urais 2015 CCM patachimbika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbio za Urais 2015 CCM patachimbika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Dec 19, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Magazeti kadhaa wiki hii yameandika kuhusu kuandaliwa mgombea wa urais Jamhuri ya Muungano kutoka Zanzibar, habari hiyo ikiwa chanzo chake ni gazeti la nje la huko Uingereza na kumhusisha Rais wa sasa kwamba ni mtazamo wake. Wakati huo huo watu wanapigana vikumbo mara baada ya uchaguzi nani wa kumrithi Kikwete.

  Tukumbuke kuwa mpasuko ndani ya CCM umezaa siri kufichuka na kuanikwa hadharani na matokeo yake yatakuja kujulikana kwani karne ya leo ni tofauti ya iliyopita, nadhani wananchi ni waamuzi wa mwisho vinginevyo kuwepo na serikali ya Tanganyika, la sivyo watanganyika watadai kutawaliwa na wazanzibar wakati wao wana rais wao.

  Makamu wa Kwanza wa Rais visiwani Hamad ametamka hadharani kuwa zamu ijayo ni ya rais wa Tanzania kutoka visiwani. Kwa tamko lake hilo sijapata kujua kama urais ni wa kupokezana au la. Na inawezekana viongozi wa visiwani wanachofurahia Muungano ni vyeo wanavyopata kutoka serikali ya Muungano.

  Napata ndoto za CCM kushikana mashati wakati wa kugombania kiti hicho ingawa kinagombaniwa na vyama vingine vya kisiasa. Hapa busara kubwa inahitajika ndani ya CCM, maana kuna dalili za kukimbizia suala la mgombea Zanzibar kwa vile kuna wabara wengi wameanza kutuhumiana kabla ya muda kuwadia.
   
 2. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  up to them
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Maalim Seif mjinga kwelikweli. Kwa sababu gani:
  1. Anasema na KATIBA inasema Zanzibar ni NCHI na mipaka yake imechorwa ndani ya katiba sasa. Raia wa nchi nyingine anakuwa Rais wa Tanzania?
  2.Kuna katiba ya JMT ameapa kuilinda na kuitetea. Analazimisha mambo ambayo hayapo kikatiba!
  3. Hajui kwamba nafasi aliopo ya Umakamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ipoipo tu kimagumashi.
  4.Wenzake ndani ya CUF wanalia chama chao kimekufa kwa yeye kukubali nafasi hiyo feki, anataka kujihalalisha kwa hoja za kijinga.
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,357
  Likes Received: 3,117
  Trophy Points: 280
  Zanzibar ni nchi kamili kwa katiba ya sasa ya zenji..............hicho kijarida cha uingereza ni uhuni mwingine wa wakoloni wetu kutuchagulia viongozi
   
 5. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Kwa asili binadamu wote tupo kimaslahi zaid!!!!!!!na hapo ndipo Nyerere ndipo was peculiar!!!!!!ok ngoja tuone kafulurization Hamad Rahid itakuwa lini!!!!yetu macho!!!!!
   
 6. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Aliapishwa lini, na ni nani aliyemwapisha?
   
 7. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...And so, your point is? Sasa ni wakati wa mzanzibari kuwa Rais wa JMT?
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  We uko dunia gani, siku hizi kuna mbinu nyingi kuvujisha siri. Siri ikivujishwa hapa rahisi kutafutwa mhusika na kumwagiwa tindikali. Kwa nini tusivujishie siri nje kuweka mambo hadharani, haya ya kubaki siri ya ikulu yashapitwa na wakati.

  Kugombea urais mtu anahitaji kujiandaa muda wa kutosha si kama zamani miezi miwili tu, hakuna mambo ya usiri, ila utandawazi.
   
 9. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  yaani Tanganyika itakuwa tunatawaliwa tena kama rais akitoka zanzibar! hii italeta kelele sana.
   
 10. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Niambie gamba walishajivua kwanza?
   
 11. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  huu mjadala hadi siku mtu atoke ngeu humu
   
 12. M

  Mtemakuni JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Naamini maalim seif ametumika tu kuwakilisha maoni ya viongozi wengi wa sisiem haswaa wa kutoka zenji..!!! But why wanasema this is tyme ya zenji kuwa rais wa muungano..? I think lugha nzuri hapo ingekua its tyme for sisiem kumsimamisha mzenji as a candidate wa presidential post 2015 caz kila chama kinampangilio wake and sio magambaz pekee ndo wenye fursa ya kutoa rais wa tz..!! Let them fight for choosing a candidate while we preparing for a 2015 president..!!:hat:
   
 13. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #13
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hapa umemaliza naomba waliweke wazi kwa kuwa utamaduni wa kuachiana wanao.
   
 14. MBURE JASHA

  MBURE JASHA JF-Expert Member

  #14
  Dec 19, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kumbukeni na Vijana wa UVCCM mkoa wa Pwani walishasema presidaa wa TZajaye yupo kwenye mfuko wa koti la Vasco dagama II
  Faizyfox,Rizone embu tutoeni tongotongo munasemaje kuhusu hili
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Aliapishwa na Rais wa Zanzibar mara tu baada ya uteuzi ule. Sikumbuki tarehe.
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwani Maalim Seif kakatazwa na nani kugombea urais wa JMT kupitia CUF? Kwa nini awasemee CCM wakati nafasi yakufanya hivo yeye anayo. Kwa nini anang'ang'ania kugombea urais wa Zanzibar tangu 1995?
   
 17. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #17
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  HALIKUHUSU.
  nyambafu!
   
 18. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #18
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  nyie cdm kwa ndoto za mchana mumezidi,huku mkiongozwa na malaika muasi dukitari silaha.
  ipo siku mtaota mko waiti hausi ya usa.
   
 19. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #19
  Dec 19, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  tatizo watu wanapeana madaraka kwa makubaliano
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mchezo unaochezwa hapa ni kama ule uliotokea kupata speaker wa sasa kwa kutoa visingizio vya gander, na sasa kwa na ya kuwatoa ngeu wanaowania nafasi hiyo wameamua kuyumbishia visiwani kama hoja kwa malengo yao. Labda rais wa sasa wa Zanzibar ndio anaandaliwa maana alivyoingia kwenye urais ni wajumbe wa bara waliompa shavu.
   
Loading...