Ndolezi Petro
Member
- Jun 26, 2024
- 7
- 6
Safari ya Ubunge Jimbo la Kigoma Kusini 2025.
Kwa heshima na taadhima, napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wananchi wa Kigoma Kusini kupitia chama chetu cha ACT-Wazalendo kwa safari tuliyoitembea pamoja tangu mwaka 2020 baada ya uchaguzi Mkuu. Tumekuwa bega kwa bega katika kujenga chama, kuimarisha mshikamano, na kuibua imani mpya ya kisiasa kwa wananchi wa jimbo letu.
Kwa heshima hiyo hiyo, naomba pia kuwataarifu umma wa Ndugu, Jamaa na Marafiki kuwa kura za maoni hazikutosha kunipa nafasi ya kugombea kiti cha Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini mwaka 2025 na Kamati Kuu ya Chama chetu ilimteua ziliyetosha. Hata hivyo, najivunia kazi kubwa tuliyofanya pamoja, mshikamano tulioujenga, na matumaini tuliyowasha miongoni mwa wananchi.
Natoa shukrani za dhati kwa kila mmoja wenu mliesimama nami katika miaka minne ya ujenzi wa chama baada ya uchaguzi wa 2020. Tumepitia changamoto nyingi, tumepambana kwa pamoja, na tumefanikisha mambo makubwa ambayo leo yanatupa nguvu ya kuendelea mbele.
Mambo Matatu ya Msingi
1. Kwa kazi kubwa tuliyofanya tangu 2020, leo hii ACT-Wazalendo ndicho chama chenye nguvu kubwa zaidi Kigoma Kusini. Tulifanikiwa kujenga ushawishi na kuunganisha nguvu na kilichokuwa chama kikuu cha upinzani NCCR-Mageuzi, chama kilichokuwa ngome ya upinzani jimboni, na leo wote tupo nao kwenye jahazi moja la ACT Wazalendo.Kwa msingi huu, ninaamini kwa dhati kwamba mwaka 2025 tutashinda Ubunge, tutashinda madiwani, na tutaongoza Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza.
2. Mshikamano na Umoja ndio nguzo ya ushindi ndivyo nilivyofanya baada ya kura za maoni kutoa wito kwa wafuasi wangu wote na wanachama kwamba tunapaswa kushikamana na kumuunga mkono atakayeletwa na Chama. Hivyo nitaendelea kumuunga mkono aliyepewa dhamana na Chama Kugombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini.
3. Wito kwa Vijana wenzangu, safari yangu imenifundisha kuwa siasa ni mapambano ya muda mrefu. Njia si rahisi, changamoto ni nyingi, lakini kukata tamaa inapaswa kuwa mwiko. Vijana wenzangu, tusikate tamaa tunapojikwaa. Huu ni wakati wetu wa kusimama na kuongoza mabadiliko ya kweli katika Taifa letu. Fursa zetu zitafika, na tutapata nafasi ya kuwatumikia wananchi wetu na kulijenga taifa letu lenye uchumi imara na maisha bora kwa wote.
Matumaini ya kuendelea na Mapambano ninapata nguvu nikikumbuka historia ya mapambano ya wazee wetu. Vita ya MajiMaji ya mwaka 1905 chini ya Kinjekitile Ngwale haikuletea uhuru mara moja, lakini iliwasha moto wa mapambano uliozaa uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 chini ya Mwalimu Nyerere na wenzake. Leo na sisi tuna wajibu wa kuendeleza mapambano ya kizazi chetu—mapambano ya haki, demokrasia na maendeleo ya kweli. Naamini kabisa siku yetu itafika. Na kwa wale vijana wenzangu waliopata fursa ya kugombea basi kazeni kamba kwelikweli na mpatapo nafasi tambueni mnawajibu wa kusimama na umma wa Tanzania. Kumbukeni mnawajibu wa kuongoza sauti ya mabadiliko tuweze kujenga Taifa jumuishi kiuchumi na kujenga uchumi wenye kuzalisha ajira nyingi zaidi kwa watu wetu.
Asanteni sana kwa mshikamano wenu.
Tutakutana tena kwenye medani za mapambano kwa ajili ya wananchi
Eng. Ndolezi Petro
Waziri Kivuli – Ofisi ya Waziri Mkuu: Bunge, Sera, Vijana, Kazi na Ajira
ACT-Wazalendo
06 Septemba 2025