Mbinu za matapeli update 2021

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
25,554
45,853
Kwa wamiliki wa saluni,

Unapigiwa simu kuna deal la kusuka watoto yatima wa kituo cha Mama Mkapa kila Jmosi toa hela upewe tender.

Mama ntilie na wapika chips.

Kuna tender ya chips kuku na mayai kila week mara tatu kwa watoto yatima 100.

Toa hela upate kazi.

NB: Wanangu tu hawali chips kuku na mayai mara tatu kwa week loh

Endelea
 
Kwa wale wajasiriamali mfano watengenezaji wa sanitizer au viungo vya vyakula au handwash hizi.tapeli anapiga simu anakuambia product yenu imependwa sanaaa na unatakiwa kesho yake saa mbili asubuhi

Uwe Dodoma kwenye ofisi ya makamu mkuu wa raisi ili kidiscuss jinsi ya kisupply kwenye ofisi za serikali Dodoma. Sasa ukiangalia muda uliopigiwa simu na logistics za kufika Dodoma ni impossible kufika huko Dodoma huo muda wa asbuhi.

Lazma upande ndege ya asubuhi, hapo ndio ujanja wao na wanasema ndege hamna lakini wana connection ya kukupatia ticket maana nafasi imebaki moja. Hapo ndio wanataka uwatumie hela sasa ya hio ticket.
 
Back
Top Bottom