Jihadhari na 'usanii' huu wanaoutumia watoto wa shule za msingi kujipatia pesa toka kwa watu wazima

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,858
Katika Kuonyesha kuwa Watoto wa Kizazi cha akina Kikwete na Magufuli huenda wakawa ni Werevu kuliko Kizazi chetu cha akina Nyerere na Mwinyi wameanza kuwa ' Wabunifu ' katika Kujipatia Pesa kwa ' Style ' ya Kipekee kabisa.

Wanajikusanya Watoto kama Watano (5) hivi kisha wanakaa katika njia Kubwa au Uchochoro kisha wakiona Mtu mzima anakuja wanaanza Kujifanya ' Kumpiga ' Mwenzao Kisha ' Mpigwaji ' analia sana huku akikuomba ' Msaada ' Wewe mpita njia ' umlipie ' Tsh 500/ au Tsh 1,000/ anayodaiwa na Wewe kwa ' Huruma ' yako (kama ya Asili niliyonayo GENTAMYCINE) ni lazima tu utatoa ili Kumsaidia na Kumuokoa huyo Mtoto ' Mdaiwa ' anayekula ' Kichapo ' cha Kutukuka na Wenzake.

Kilichoniuma zaidi ni kwamba baada ya Huruma yangu ya Kumlipia ile Tsh 1,000/ (Buku lile) yule Dogo aliyekuwa anapigwa hivi punde tu nimekutana nao katika Kibanda cha Chips wanakula Chips, Kuku na Mayai huku Mimi niliyetoa ' Buku ' langu nililokuwa nalo Mfukoni Usiku huu nalala kwa Kushindia tu Maji ya Dawasa (ya Wachina) hadi Kesho Asubuhi.

Baada ya ' Kudadisi ' nimeambiwa kuwa ' Mbinu ' hii ya ' Kiubunifu ' kabisa wanayoitumia hawa Watoto wa Shule za Msingi kwa Siku huwa inawaingizia kati ya Tsh 20,000/ Mpaka Tsh 30,000/ ambayo huwa wanagawana kulingana na Idadi yao isipokuwa tu Yule aliyekuwa ' akipigwa ' huchukua kiasi kingi kuliko wengine ili impoze ' Maumivu ' huwa ' wanampiga ' kiukweli ili Kumtengenezea Mazingira ya kuonewa Huruma na Sisi Watu wazima wapita njia.

Sasa baada ya leo GENTAMYCINE kuingizwa nao mjini (Kudanganywa) nimeamua kuwatengenezea ' Tego ' ambapo nawasahaulisha kwa Siku Tatu na Jumatano ijayo ' najipitisha ' tena katika hiyo njia Makusudi ili ' nijilipe ' vizuri ' Buku ' langu linaloniuma sana ambapo Kwanza nikiwakuta ' Wanampiga ' Mwenzao nami ' nawasindikiza ' katika ' Kumpiga ' kisha nikimaliza nawapigisha Wote Magoti na naanza ' Kuwasachi ' Mifukoni Mmoja Mmoja na ' Kuwakomba ' Pesa zote na ndipo watashika Adabu zao na kujua ni kwanini Mkoa wa Mara ( Musoma ) hakuna Kibao cha KARIBU MARA au kwanini Wimbo wa Taifa hauna Kolabo.

Je, nanyi mmekumbana na Usanii huu?
 
Mitaa ya Mnazi Baridi na Akiba Kuna madogo huwa wao wanajifanya wamepoteza nauli wanaomba kusaidiwa mia 5 nauli wanadai wanataka kurudi Mbagala. Ukiwaambia uwapandishe daladala ulipe nauli wanasema Kuna wenzao wapo nyuma.

Wakiisha kujua hawaombi wanatafuta sura ngeni ngeni. Wanapiga misele Sana unaweza ukawakuta mpaka Mnazi Mmoja mida ya kutoka shule.
 
Daah, kweli yaani Kuna madogo kama wawili waliniomba nauli aisee..
Mitaa ya Mnazi Baridi na Akiba Kuna madogo huwa wao wanajifanya wamepoteza nauli wanaomba kusaidiwa mia 5 nauli wanadai wanataka kurudi Mbagala. Ukiwaambia uwapandishe daladala ulipe nauli wanasema Kuna wenzao wapo nyuma.

Wakiisha kujua hawaombi wanatafuta sura ngeni ngeni. Wanapiga misele Sana unaweza ukawakuta mpaka Mnazi Mmoja mida ya kutoka shule.
 
Mjini mipango aisee... Ni mbaya sana watoto wadogo kujifunza upigaji mapema hivo..

Ila mkuu GENTAMYCINE unanifurahishaga sana kila nikisoma uzi wako lazima nitakuta umelitaja jina lako GENTAMYCINE atleast twice.
Ninalipenda sana na mno Jina langu hili.
 
Back
Top Bottom