Pilau la Christmas hili hapa

thomas_360

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
1,459
1,428
Kama ilivyo ada Leo ilikuwa siku nzuri ya kuonyeshana nani zaidi kwenye mapishi hasa msosi pendwa PILAU aka wali mchafu..

Haya fuatilia mapishi yangu yalivyokuwa..

MAHITAJI YA MAPISHI

1) MCHELE 3/4
2) VITUNGU MAJI (3)
3)VITUNGU SWAUMU (2)
4) IRIKI ( pakiti 4 @ tsh 50)
5) MDALASINI ( pakiti 4 @ tsh 50)
6) BINZALI NYEMBAMBA ( Pakiti 4 @ tsh 50)
7) PILAU MASALA
8) TANGAWIZI

MAANDALIZI YA AWALI

1) Menya vitunguu maji, vitungu swaumu, tangawizi,
2) Chukua vitungu swaumu na tangawizi vitwange pamoja au tofauti ( utakavyopenda wewe)
3) Chukua maji ujazo wa kikombe kikubwa cha chai kisha mimina kwenye sufuria ambayo itakuwa na mchanganyiko wa iriki, mdalasini na binzali nyembamba kisha chemsha mpaka zichanganyane vizuri halafu chuja maji yake pembeni.
4) Chemsha maji mengine pembeni kwa ajili ya kupikia weka chumvi kabisa kuangalia kiwango kizuri.
5) Chambua mchele wako na uoshe Mara moja kama sio mchafu sana! angalizo kuosha mchele Mara nyingi nikupunguza ladha na harufu nzuri ya Mchele.

MAPISHI YENYEWE:

1) Bandika sufuria lako jikoni na kadiria mafuta ya kula kadri ya uwezo wako maana raha ya pilau futa lionekane isee sio linakuwa kavu kama la shuleni

2) Weka vitungu maji vikaange mpaka viwe vinakaribia rangi ya brown kisha weka vitungu swaumu, tangawizi na pilau masala vijiko viwili au vitatu vya chakula. weka Yale maji ya mchanganyiko wa iriki, mdalasini na binzali nyembamba uliyochuja kidogo kisha acha vichemke kidogo.

3) Mchanganyiko wa hapo juu ukishachanganyika vizuri weka mchele wako hakikisha umechanganyika vizuri kisha malizia maji ya mchanginyiko wa iriki, mdalasini na binzali nyembamba, baada ya hapo yachukue Yale maji ya kupikia sasa uongezee kiwango ambacho yatavuka mchele wako kidogo, ( angalizo usiweke maji mengi pilau litakuwa bokoboko)

4) Kama unatumia jiko la gesi hakikisha moto usiwe mkali sana mwanzoni Ila maji yakishapungua punguza moto wako Ila usigeuze kwanza, kaa kama dk 10 baada ya kupunguza moto then geuza pilau lako hakikisha pande zote umehegeuza vizuri. baada ya kugeuza nyunyuzia maji kwa juu kidogo then acha kama dk 15 moto hakikisha ni mdogo, baada ya dk 15 geuza tena kisha acha kwa dk 5 kisha zima jiko lako subiri kama dk 5 zingine kisha upakue msosi wako.

Kwanini nimesema acha kama dakika 5 usipakue kwanza? Hii ni kufanya lile joto lilibaki liishia kwenye sufuria vizuri ili msosi uive vizur kabisaaaa!!

PILAU BILA KACHUMBARI HAINOGI

MAHITAJI
1) Limao/ndimu
2) Nyanya kulingana na idadi ya watumiaji
3) Matango
4) Karoti
5) Kitungu maji
6) Pilipili hoho

MAANDALIZI:
1) Chemsha maji kwa ajili ya kusagia kitunguu maji kisha saga vitungu maji pamoja na chumvi kidogo
2) Kata nyanya size ndogo
3) Kata karoti size ndogo
4) Kata matango size ndogo
5) Kata pili pili hoho size ndogo
6) Chukua chombo chako kwa ajili ya kuchanganya hivyo vitu vyote kisha weka limao/ndimu pamoja na chumvi.

HAPO DARASA LINAKUWA LIMEISHA KWA LEO

AHSANTENI

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom