Mbinu za kumweka mmeo kiganjani kabaaaaang

Parata

JF-Expert Member
Jul 26, 2011
3,090
675
Mbinu chache za kuwaweka
waume zenu kiganjani.
Mpe mumeo anachohitaji :
Wanawake wengi wanashindwa
kujua wao wanatofautiana na
wanaume kwa hisia na hata
mawazo ya mapenzi. Wanaume
wana mambo wanayoyapenda
kutoka kwa wake zao hasa
katika masuala ya mapenzi.
Kwanza wanawake wajue
wanaume wengi wana hisia za
haraka za kufanya mapenzi
kuliko wanawake.
Mwanaume alivyoumbwa ni
kwamba akiona tu mfano
mwanamke umevaa kanga
moja au umevaa night dress
hiyo inatosha kusisimua. Wapo
wanawake wanaowasisimua
waume zao bila wao kujua.
Mfano umevaa tu kanga moja
au night dress ndani huna kitu.
Kwako ni jambo la kawaida
lakini kwa mwanaume sio la
kawaida kwa kukuona hivyo
tayari unakuwa umeamsha
hisia zake. Ukimwona anakuja
kutaka haki yake usidhani
anakusumbua. Ujue tayari
mwenzako alishafiria mbali
zamani we huna habari.
Ni vyema ukawa mwangalifu
kujua hisia za mwanaume huyo
mumeo kama inawezekana
mpe anachohitaji kwani
usipofanya hivyo unamwathiri
kisaikolojia na anaweza
kufikiria nje. Wanawake wengi
wa nje waliowaweka waume
zenu kiganjani hiyo ndio mbinu
wanayotumia. Akiwa na ahadi
na mumeo atamkuta kanga
moja au amevaa night dress na
kila anachohiji atapewa haraka
tena kwa madoido. Kwanini
akitaka hayo hayo kwa mkewe
hapewi je ana kosa gani
anapofikiria nje?
NB:
Nikisema mpe mumeo Hitaji
lake sina maana Umpe mpaka
kinyume na maumbile Ukiona
Mumeo kafikia hapo Huyo Hafai
si Mume mwenye Busara huyo
na wala hakutakii mema
mkatalie na Umwelimishe
madhara ya Tendo la ndoa
kinyume na maumbile.
Mvutie mumeo kwa
mwenekano wako:
Mvuto ni muhimu sana kwa
mwanaume. Wanaume
wanapenda wanawake
wanaowavutia kihisia.
Niwaambie wanawake
mlioolewa jueni kumvalia
mumeo mavazi yanayomvutia.
Sio vibaya kama nilivyosema
hapo juu ukavaa kanga moja
kama upo pamoja nae. Kama
nilivyoeleza hapo juu
mwanaume anasisimka kwa
kuona. Kwanini avaliwe kanga
moja na wanawake wa nje
wakati wewe unaweza kuvaa.
Wanawake jueni hili
mnapokuwa karibu na waume
zenu jianchieni Kwa mfano
hakuna ubaya wakati mumeo
karudi kutoka kazini akiwa
amechoka, wakati
unampotengea chakula ukavaa
kanga moja au night dress.
Unaweza kuona hilo ni jambo
dogo lakini kisaikolojia utakuwa
umefanya jambo kubwa. Hapo
hata kama atakuwa ameudhiwa
kazini atasahau na kukuona
wewe mpenzi wake.
Usafi panga vitu vyako vya
chumbani vizuri:
Jambo hili limekuwa
lizizungumzwa sana hadi
wengine wanasema mwanamke
usafi. Kisaikolojia mpangalio wa
vitu ndani na hasa chumbani
kama ni mbovu unaweza
kuathiri hata tendo la ndoa.
Kama chumba ni kichafu vitu
havijapangwa vizuri kisaikolojia
kunapunguza msisimko wa
mapenzi na hata kumfanya
mwenzako achukie kufanya na
wewe tendo hilo ukadhani
hakupendi.
Mwanamke tandika kitanda
chako vizuri panga chumba
chako tandika shuka nzuri. Siku
hizi kuna shuka zina maneno
ya mapenzi nunua hiyo uwe
unatandika. Kisaikolojia
utamfanya mpenzi wako
avutiwe chumba chako na hata
wewe mwenyewe. Mazingira
mazuri yatamfanya asisimke
haraka kimapenzi anapokuwa
na wewe na hata kuitamana
nyumba yake na kurudi
mapema nyumbani.
Jinsi chumba kilivyo rafu ndiyo
wanasakolojia wanasema
kunafanya ubongo uwe rafu
hata kuchukia. Unaweza
kumwona mwenzako anachukia
kumbe ni kutokana na
mpangilio mbovu wa chumba
ndio sababu inayomfanya
achukie.
Uwe msafi wa mwili:
Sio usafi wa chumba pekee
unatosha pia na usafi wa mwili
wako ni muhimu.
Niwakumbushe wanawake
hakuna kitu kinachowachukiza
wanaume kama mwanamke
mchafu. Asiyejipenda. Sio
lazima ujirembe sana lakini
jitahidi ukawa msafi. Oga vizuri
paka mafuta au lotion yako
jipulizie manukato kidogo
yanayomvutia mumeo. Sio
lazima utumie gharama kubwa
usafi wa kawaida unatosha na
kupaka rotion kuna fanya ngozi
ya mwanamke ikawa laini
inayovutia wanaume
wanapenda sana wanawake
wenye ngozi laini yenye
kuvutia inaleta msisimko
mumeo anapokuwa
anakuangalia mara kwa mara.
Wanawake wa nje hawana zaidi
ya hayo ni hayo hapo juu na
mengine ndiyo wanayotumia
kuwaweka waume zenu
kiganjani. Usijaribu kwenda
kwa mganga hakuna
atakachokusaidia memeo
atatoka kama wewe
humsisimui, hupangi vitu
vyako vizuri na pia kama
unaendekeza uchafu ni rahisi
mumeo kufikiria nje.
Kujiamini kwako iwe ni kwa
sababu unajua ‘kumhendo’
mumeo kwa kumpa mapenzi ya
kiwango cha juu, kumheshimu,
mjali na kumpatia mambo ya
msingi ambayo anastahili
kuyapata kutoka kwako.
Ukifanya hivyo utaifanya roho
yake imsute kila anapotaka
kukusaliti.
Hiyo ndiyo iwe sababu ya wewe
kujiamini na wala huna sababu
ya kujinadi kwa wenzako.
Tambua kuwa kuna wanaofikia
hatua ya kuhatarisha maisha
yao kwa kutoa ‘mtandao’
wakijua kuwa ni njia ya
kuwashika waume zao kumbe
wanajitafutia matatizo
makubwa.
Wapo waliopoteza fedha zao
nyingi kwa kwenda kwa
waganga ili waume zao
wasifurukute mbele zao lakini
imekuwa kazi bure. Shituka leo,
anza kutumia mbinu sahihi za
kuishikilia ndoa yako na
usijidanganye kwa kufanya
mambo ambayo ni sawa na
kutwanga maji kwenye kinu.
Mwanamke aliyekamilika ni
yule anayeuthamini mwili
wake, sasa kwa nini leo hii
ukubali ‘kumrukisha ukuta’
mumeo ili kumfanya asiende
nje? Kwa nini utumie fedha
zako kwenye kumtafutia
limbwata mumeo wakati wewe
mwenyewe ni limbwata tosha?
 
Hivi ina madhara gani kutumia mtandao, mbona ni nzuri tu, ufafanuzi tafadhali
kwa mwanamke na mwanamume!
 
Asante ndg mpendwa kwa mafunzo hayo...ila hawa wenzetu hawatabirikagi. Unaweza kuwa una perform all those vipengelez ila baaadooooo akatoka njee. Ngumu kweli kuwaelewa.
 
Mwanaume akishaoa anachukia sana kuona hali ya Uchafu nyumbani na uchafu huletea mume kupungua munkari ya mapenzi kwa mke:Cha ajabu mwanamke asafiri kidogo,utaona balaa lake,Mswaki,Kiwi,Lotion,dawa ya meno,plate ya chakula,brush za viatu,vyote vimewekwa sehemu moja,fagio lipo juu ya sofa nk..Hivi ni kwa nini? (Walio wengi wapo hivyo)

Mwanamke anatakiwa kuwa msafi wa mwili na nyumba na atumie tekniki zingine za kumvutia mume wake.Mwanaume akiwa na mke hujitahidi kubadilika na kuwa msafi kiasi chake (kama alikua mchafu), ,
 
SAMRICH1 hii iko poa! Wanasemaga nyumba ni mwanamke na pia, mwanamke yule mwenye busara huijenga nyumba yake mwenyewe lakini yule asiye na busara huibomoa kwa mikono yake. Kuna baadhi ya wababa huchukia na kuchukia kurudi nyumbani just kwa sababu ya mazingira mabovu ya nyumbani na pengine na tabia za mke.

Lakini hii si justification ya sisi akina baba kuwa na nyumba ndogo. Kama wakuu wa familia twapaswa kuwapenda na kuwaenzi wake, watoto na familia zetu na kuwatunza ktk viwango na ubora unaotakiwa. Kwa ushirika wa namna hii, ndoa lazima itakuwa kwenye furaha wakati wote. Maana ndoa si mwanamke kwa ajili ya mwanaume au mwanaume kwa ajili ya mwanamke, bali ni watu wawili ktk nafsi pamoja.

Nawatakia amani wanandoa wote!
 
hiyo nzuri ila na mwanaume pia ajue kumuweka mwanamke kiganjani. kwani akimtimizia haja zake kitandani wallah mwanamke haendi nje ya ndoa. kwani wanaume wengi huwa wanahema tu kwa wanawake wakishakizi haja. Wanawake tunahitaji haki zetuu. Raha babu tule sote
 
Unapoweka jambo la kuwahusu wanawake jifunze tabia zao

Hawa watu ni wavivu sana wa kusoma

Somo lako limekua refu sana

Hivyo malengo yako hayataleta matokeo chanya sana

Tengeneza fupi!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom