Mbinu za kuingia nchi ya jirani kutafuta Fursa

Jojo123

JF-Expert Member
Jan 31, 2013
432
694
Hello JF guys!

Ni hivi:

Tuna zungukwa na Uganda, Rwanda, Malawi, Zambia na Msumbiji, Kenya na Congo

Kama mzoefu wa fursa za kiuchumi na upo hapa JF au ulisha wahi kuingia kwenye moja ya Nchi moja wapo katika hizo hapo juu tupeane mbinu zakuingia na urari wa maisha katika hiyo inchi.

Twambie chumba cha kupangisha mtaani kinachezea bei gani?

Je, njia za panya zipo mkoa gani uzoefu wako wa mipaka unauzungumziaje?

Biashara gani yenye maslahi ya mtu akizamia anaye anza maisha kwa kamtaji cha kubangaizia?

Maeneo gani katika nchi husika yenye uchangamfu na fursa ni zipi?

Una ushauri gani kwa mtu anayetaka kuzamia hiyo inchi kulingana na uzoefu wako kwa wenyeji?

Asanteni. Nilitamani kuzamia Malawi kujaribu maisha au Zambia ili nikifanikiwa kuingia na kufanya biashara nika dunduliza ni zamie South Africa kabisa.

Elimu yangu Degree, umri 33. Mwanaume
 
Hello JF guys!

Ni hivi:
Tuna zungukwa na Uganda, Rwanda, Malawi, Zambia na Msumbiji, Kenya na Congo

Kama mzoefu wa fursa za kiuchumi na upo hapa JF au ulisha wahi kuingia kwenye moja ya Nchi moja wapo katika hizo hapo juu tupeane mbinu zakuingia na urari wa maisha katika hiyo inchi...
Mkuu Arovera njoo huku umsikie mdogo wako
 
Kama unaenda kutafuta ukwasi unajisumbua tu hakuna lolote huko bora upambane apa nyumbani na 33 yako bado 7 uanze maisha rasmi

Ila kama unaenda kama hobby hapo sawa tuendelee na ushauri maana kwa hizi nchi jirani Ni too simple.
Sasa najiuliza hapa ukwasi si sehemu ya utafutaji ata nikiwa hapa Tz au ume maanisha kule ukwasi shida kupata?
 
Sasa mpaka kwenda Kenya Rwanda sijui congo unataka njia za panya? Mbona ukifata process ni rahisi sana

Fata utaratibu, unaenda kutafuta pesa bado unakua na uoga wa kukimbia vyombo vya sheria ugenini? Mbona mnapenda kujitesa?
 
Nchi zote zlizotuzunguka wanatamani kuhamia Tanzania,Bongo kutamu sana
Kweli kabisa kutamu unaumizwa huku unachekewa kwa unafiki hatujambo
Ila kuna watu wanakula nchi labda ndio maana wanatamani kuja kwetu.

Yaani mtu anaiba hela za umma na za miradi halafu anahamishwa safi sana.

Ndio maana wanatamani kuja.
 
Kweli kabisa kutamu unaumizwa huku unachekewa
Kwa unafiki hatujambo
Ila kuna watu wanakula nchi labda ndio maana wanatamani kuja kwetu

Yaani mtu anaiba hela za umma na za miradi halafu anahamishwa Safi sana

Ndio maana wanatamani kuja

Hivi unajua wanasiasa wa kenya walivyo matajiri kuzidi wetu?wizi ni asili ya miafrica,we tafuta maisha usiwafikirie hawa wanasiasa
 
So hakuna aliyopo uko kwenye nchi tajwa ata anipe majibu ya alivyo ingia na maisha yakoje uko na ana dhani mtu akiingia afanye issue gani yenye mzunguko wa uhakika wakipato?
 
Binafsi sijawahi kufika katika hizo nchi jirani, ijapokuwa nimeishi na vijana wanaotoka hizo nchi. Mitazamo yao juu ya nchi zao na fursa za kiuchumi haitofautiani sana na yetu, yaani na wao wanaakili za kutoka nje ya nchi yao, au kuamini pengine nchi za jirani zinafursa zaidi kama wewe unavyoamini.

Mimi nimeishi nchi fulani ya Afrika japo sio hizi za East Afrika, lakini hali ya kimaisha hazitofautiani sana na kwetu, na hivi ndivyo hali ilivyo kwa nchi nyingi za Afrika, ukitoa chache ambazo kidogo zimepiga hatua kama South Afrika n.k

Hivyo suala la mtu kutoboa akienda katika hizo nchi halina guarantee kama vile mgeni anavyoweza kuja Tanzania, hivi utamwambia afanye mishe gani atoboe? ikiwa hana mtaji wa kueleweka anaanzia chini kwa kufanya shughuli ndogo ndogo.

Lakini hili halikanushi uwepo wa fursa za kibiashara kama wanavyofanya wengi kwa kuchukua bidhaa huku na kupeleka kule au vise versa, hizi zipo.

Lakini hili la kwenda kuanza maisha huko ukiamini huwenda kuna fursa zaidi ya kutoboa, hili halina guarantee kama ilivyokuwa hapa kwetu.
 
Asante ndugu kwa ushauri
 
Uzi ume simama kabla ya kumpata mzoefu aliyepo field?? Msinifanyie hivyo mazee..
 
Kama urapata walau laki 5(pesa ya kubangaiza) nenda Msumbiji sehem za Machimbo toka dar na bidhaa hata kama ni nguo, viatu ama vipodozi maana kuna Machimbo mengi sana na watanzania wamejaa + wenyeji na mataifa mengine kikubwa pata kubali cha muda maana kwao ishu ni ufate utaratibu. Wengi wametoboa sana msumbiji kupitia Biashara sehem za Machimbo ya dhahabu na Rubi.
 
Back
Top Bottom