Mbinu za kudhibiti wizi wa mazao mashambani

Averos

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
993
695
Habari wakuu

Hongereni kwa kazi za ujenzi wa Taifa. Niende kwenye mada

Moja kati ya changamoto zinazowakumba wamiliki wa mashamba ni wizi wa mazao mashambani. Changamoto hii huwakumba zaidi wamiliki wa mashamba ambao wanaishi mbali na mashamba

Wapo wamiliki wa mashamba wanaolima mikoani wakiwa Dar es Salaam kwa mfano na hulazimika kuwaweka wasimamizi wa mashamba ili kuhakikisha shughuli za shamba zinakwenda vyema

Changamoto ya wizi wa mazao inakuwa kwa namna mbili, Kwanza ni wizi wa mazao kutoka kwa wananchi wanaoishi karibu na shamba na ya pili ni kutoka kwa msimamizi wa shamba

Mashamba mengi yenye wasimamizi changamoto ya wizi wa mazao haitokani na wizi wa watu wanaoishi karibu na shamba bali kutoka kwa wasimamizi wenyewe.

Pamoja na kuwahudumia wasimamizi wa shamba kwa chakula na posho ya kujikimu Bado wamekuwa na tabia ya wizi wa mazao

Naomba tushee uzoefu kwa changamoto hii ili tuone namna ambayo tunaweza kupunguza au kudhibiti wizi wa mashambani

Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom