Mbinu za kudai katiba mpya

monde arabe

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
8,490
13,022
Habar za wakati huu ndugu wanajukwaa,rejeeni uzi wangu wa Trh 23/06/2021 unaotutaka Watazania wa rika zote kuungana ili kuweza kudai katiba mpya...thread ya leo ni mwendelezo tu

Ndugu zangu Watanzania wenzangu,tunapaswa kutumia akili nyingi katika suala hili la katiba mpya,katiba mpya siyo hitaji wala takwa la CCM, wala siyo hitaji la Chadema;katiba mpya ni hitaji la Watanzania wote kutokana na mahitaji ya wananchi wote kwa kuzingatia nyakati tulizonazo

Hizi ndizo mbinu tunazopaswa kuzitumia kudai katiba mpya

1.Kwenye mikusanyiko ya mpira wa miguu
Mashabiki wa mpira wa miguu kila tunapokutana Kwenye mechi za mpira wa miguu tunaelimishana kuhusu umuhimu wa kuwa na katiba mpya.Pia,ikitokea mchezaji amefunga goli sisi kama mashabiki tunashangilia "tunataka katiba mpya,tunataka katiba mpya,tunataka katiba mpya tunataka katiba mpya,tunataka katiba mpya"

Tuitumie mikusanyiko ya mpira wa miguu kama platfoam ya kudai katiba mpya.Kwa wale msiofahamu zamani sana wakati Wazee wetu wanadai uhuru Wazungu walipiga marufuku mikusanyiko ya kisiasa so,wenye fikra pevu walikuja na wazo la kuanzisha Club ya Yanga ili waitumie kama jukwaa la kudai uhuru so,kila siku Yanga walipokuwa wakifanya mazoezi kuna Wazee walikuwa wakienda kuangalia mazoezi na wakifika mazoezini wanaanza kujadili namna ya kupata uhuru na hawakuweza kushtukiwa na Wazungu kwa kuwa walikuwa wanajifanya kama wanaangalia mazoezi ndyo maana ukiigusa Yanga au Simba unakuwa umeigusa serikali (huwezi kuitenganisha Yanga/Simba na Serikali)

Pia,tunapoingia uwanjani tusivae sare za vyama vya siasa kama Chadema,CCM,ACT Wazalendo kwa kuwa tunaweza kukatazwa kuingia ndani ya uwanja.Kila mmoja goli linapofungwa apaze sauti "tunataka katiba mpya" na slogan hii itaanza kutumika kwenye game ya Simba na Yanga ya Trh 03/07/2021

2.Kwenye matamasha ya Wasanii,Wanamuziki na Wanamichezo wengine,hapa kila mmoja anapokwenda kuhudhuria tamasha lolote la burudani au starehe ahakikishe anashangilia kwa kutamka sentensi "tunataka katiba mpya" na atamke mara nyingi na kwa sauti kadri atakavyoweza.Mfano ukienda kwenye matamasha ya Wasanii wa Bongo flavour huwa wanaimba halafu wanageuza mic kwa mashabiki ili waweze kuimba pamoja hakikisha msanii akigeuza mic kwenye audience sote tuliohudhuria hiyo concert/show tunatamka "tunataka katiba mpya" na tufanye hivyo hata asipogeuza mic kwa mashabiki. Pia,baadhi ya Wasanii huwa wanatafuta mzuka wa shoo wanasema "woyoooooo,woyo woyo" halafu wanageuza mic kwa mashabiki...wakigeiza mic tu kila mtu aseme "tunataka katiba mpya" na tufanye hivyo mara nyingi zaidi kwa kuwa hawa Wasanii hawapo pamoja na sisi wananchi bali wapo pamoja na majambazi ya ccm. Watanzania tukumbuke hakuna mtu au kundi litakalo tutetea au kutupigia tofauti na sisi wenyewe kujipigania

3.Tudai katiba mpya kwenye mikusanyiko ya kidini kama vile kanisani (kwenye ibada mbalimbali na mafundisho) pamoja na misikitini bila kusahau mihadhara

Hakuna kiumbe kilichosalama ndani ya Tanzania bila katiba mpya.Hakuna uchumi imara ndani ya Tanzania bila katiba mpya.Bila katiba mpya tutaendelea kuishi Tanzania kwa hisani ya viongozi/ majambazi ya ccm kwa kuwa usalama wetu unategemea utashi na ufahamu wa viongozi au majambazi na mashetani ya ccm.

Tafadhali mods,naomba uzi huu usiunganishwe na uzi wowote ule

Asanteni sana!
 
Back
Top Bottom