Michael Chairman
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 922
- 583
Taifa lenye watu wanaofikili vizuri ni Taifa imara sana na Taifa hilo litakwenda likishindana na vizingiti vya kila aina vinavyokuja kwenye Taifa na kwa kutumia kanuni ndogo tu ya AKILI ifanye kitu.
Katika kutafakari jambo hili la uraibu wa madawa ya kulevya jambo ambalo limeshika kasi zaidi nchini kwetu mara baada ya Mkuu wa mkoa wa GIANT CITY kutangaza kuanza vita hiyo ambayo kwa maoni yake yeye ndiye anakuja kukata mzizi wa fitina wa jambo hili baya hapa nchini.
Kushamili kwa madawa ya kulevya kama kunavyoelezwa hapa nchini kunasemekana kunatoka na wafanyabiashara wakubwa kuachwa na wao kuendelea kufanya biashara hii bila kuguswa na mkono wa sharia ....jambo hili mimi kwa maoni yangu nakataa ukubwa wa jambo hili umesabishwa na haya yafuatayo..
1.SHERIA YA MADAWA YA KULEVYA.
Duniani kote kile kinachoitwa kuzuia jambo kwa kutumia sharia hakujafua dafu kuondoa tatizo , bali sharia hizi mara nyingi zimeendelea kuongeza kile kinachoitwa ukubwa wa tatizo husika , na hii ni dhahiri hata kwa Mwenyezi Mungu (YEHOVA) mwenyewe aliona haja ya kutumia sharia kwenye mambo mengi kulididimiza hatua za kumkomboa binadamu kutokana na masuala ya uharifu na kutenda dhambi na akaamua kubadili namna ya kushughulika na binadamu kwa kuondoa sheria ona mfano wa kuwaangamiza wanadamu waovu kwenye gharika , lakini baadaye waovu waliibuka tena kutoka kwa wasafi,
Sheria hizi kwa kiasi kikubwa zinaongeza ukubwa wa tatizo la madawa ya kulevya kule tu sheria kutamka kuzuia madawa ya kulevya huku kunaamsha hamasa ya watu kutaka kufanya udadisi na kujaribu kujua hiki kinachozuiwa kina nini ,
Tizama mfano wa jaribio hili la mwalimu wa akili alilowapatia wanafunzi wake , aliandaa chumba kizuri na ndani ya chumba hicho akaweka glass kumi za maji ya kunywa , glass tano akaziandika KUNYWA na glass tano zingine akaandika USINYWE , akawaruhusu wanafunzi hao (watano)kwenda ndani ya chumba hicho na kufanya yale watakayoona ndani ya chumba kile. sitatoa matokea ya jaribio hilo hapa....
2.VITA HII INAGHARIMU FEDHA.
Taifa la marekani hutumia zaidi ya $30,000,000,000/= kwenye vita ya madawa ya kulevya kwa mwaka , kiasi hichi cha pesa ni kikubwa sana nacho kinachochewa na kile nilichoeleza hapo juu , ukiangalia jambo hili kwa jicho la kiuchumi hiki kinachofanyika ni hasara kubwa sana kwani ingewezekana madawa haya ya kulevya yakaruhusiwa kuna fedha zaidi ya hizo wanazozitumia Taifa la marekani kupambana na vita hii ya madawa ya kulevya kwani madawa haya yakiluhusiwa ya kuna ukusanyaji mkubwa wa kodi kutokana na biashara chukulia mfano wa mkuu wa mkoa RC Makonda anasema kuna siku watu Fulani kumi walimfuata ofisini kwake kuahusiana na biashara ya shisha na wakamwambia wanapata zaidi ya faida ya milioni 35-45 kwa mwezi na yeye walitaka wawe wanamgawia milioni tano tano kila mmoja kwa mwezi ambapo makonda angeweza kupata milioni Hamsini kutoka kwa watu hao kwa mwezi , huo ni mfano wa haya tunayozunguzumza.
Kwahiyo tunaposema vita hii inagharimu fedha tunamaanisha kuna fedha watu wanapata kwa kuuza madawa ya kulevya na kuna fedha taasisi zingine zinapata kwa kukamata wauzaji wa madawa ya kulevya (faini za watuhumiwa kwa mahakama) n.k
haya ndiyo kwa kiasi kikubwa yanachangia hiki kinachoitwa madawa ya kulevya kushamiri duniani kote.
SULUHU YA TATIZO HILI.
Utafiti uliofanyika hivi karibuni na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) umebaini kwamba asilimia 71 ya watanzania wanatumia muda mwingi kufanya shughuli zisizokuwa za uzalishaji mali wala tija binafsi kwao na kwa Taifa kwa ujumla.
Akizundua taarifa ya utafiti huo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa idadi hiyo hufanya kazi zisizoleta tija kwao na taifa na muda mwingi huutumia kujihudumia binafsi kwa kulala na starehe nyingine.
2.MATIBABU NA ELIMU.
heko kwa serikali ya awamu ya nne chini ya Jakaya kikwete kuwasaidia kwa kiasi kikubwa waraibu wa madawa ya kulevya kwa kipindi ya uongozi wake na kwa hili yeye ni mtu kwa kupigiwa mfano duniani kote , kwanini waraibu wa madawa ya kulevya huwa wagonjwa ambao hawapaswi kupelekwa polisi bali kwenye matibabu kwa ajili ya kupata tiba , na hii itawasaidia sana ,
Elimu sahihi ndiyo nyenzo muhimu sana kukabiliana na jambo lolote lile duniani kuhimizwe watoto kujifunza madhara na faida ya vitu ambavyo jamii kwa kiasi kikubwa inapata shida na mambo hayo.
MWISHO....
MY take haya ni maoni na ushauri wangu binafsi kama mtanzania ninaye tumia ufahamu wangu kamili kujenga hoja , na hoja itufanye kufikiri mambo makubwa yanayoikabili nchi yetu ukilinganisha na hiki kinachoitwa vita ya madawa ya kulevya leo kwa kiasi kikubwa nguvu kazi ya taifa hili inapotea si kwasababu ya madawa ya kulevya bali kwa mifumo ya sera zisizo hamaisisha rasilimali hii kufanya mambo yake yenyewe kwa mafanikio yake leo junia la dengu linaiuzwa 200,000/= waambie vijana walime dengu kwa kuwapa mtaji na elimu na uhakika wa soko uone kama watashinda kwenye madawa ya kulevya ....
Elimu ni nyenzo

- BUNGE LITUNGE SHERIA YA KURUHUSU MADAWA YA KULEVYA YAWE HALALI.