Elections 2010 Mbinu nyingine chafu dhidi ya Dr Slaa hii hapa

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Uvumi ulioenea jana kuwa kuna lori lina makaratasi ya kupigia kura Tunduma, kama kweli si za kweli basi huenda hizi zikawa ni mbinu nyingine chafu dhidi ya Dr Slaa..

Wanajua kuwa Dr Slaa hana vyombo vya usalama na upelelezi kuweza kutambua kuwa habari alizopelekewa kuwa si za kweli, na kutokana na kwamba zinahusu ushindi wake, walijua lazima atalizungumzia tu ili wapate sababu nyingine ya kutuambia kuwa huyu ni mlopokaji na hafai kuaminiwa.

Inawezekana pia kuwa mzigo wa hizo karatasi uko nyuma unakuja na huu uvumi umeenezwa ili baadaye ule mzigo wenyewe ukifika tukilalamika kuwa ni karatasi watuambie kuwa tumezoea kuzusha na hakuna kitu kama hicho.

Tunatakiwa tuwakatalie na tusonge mbele..

DR SLAA for President 2010
 
Dr Slaa amezungumzia kuwepo kwa taarifa za kukamatwa kwa lori lililobeba karatasi za kupigia kura. Huo ni ukweli ambao hata polisi wamekiri na wakafanya uchunguzi. Sioni tatizo hapo. Wafanyakazi wa TRA waliopo Tunduma wangekuwa na msaada mkubwa sana kwa nchi yetu kama wangetueleza walichokiona kwenye lori linalodaiwa kupakia vipodozi. Tatizo ni kwamba wamekuwa wakisemea chini chini tu.
 
na kweli ni mropokaji
Tueleze kasema nini hainatosha kusema ni mropokaji bila kuainisha alichosema, nikisema na wewe ni kimbelembele mlamba matapishi nitakuwa nakosea. Slaa si kama Kikwete kaona messeji usiku asubuhi akarukia kuzizungumzia bila kufanya utafiti.
 
na kweli ni mropokaji
mshukuru Mungu ulizaliwa Tanzania. watu wenye udini kama wewe tunahitaji kuwaelimisha. Hebu angalia sahihi yako, utajua tu unamchukia Slaa kwa Imani yake. Mi sikubaliani na JMK na sitamchagua, lakini sitamchukia kwa kuwa anavaa baraghashia na kanzu na kusika Koran na tasbihi. Kwa nini usibadili uraia ukaishi kwa amani huko kwa mh. Ahamadnejad?
 
Nashangaa watanzania tunapoelekea!

Kila mjadala unaoanzishwa hapa jamvini, chembe chembe za udini lazma ziingizwe.

Nawaomba tuwe makini Watanzania. Hatujui ni nani yuko behind ya hii motive!

Let us keep our eyes open!
"Tunapopelekwa" si penyewe...
 
Nashangaa watanzania tunapoelekea!

Kila mjadala unaoanzishwa hapa jamvini, chembe chembe za udini lazma ziingizwe.

Nawaomba tuwe makini Watanzania. Hatujui ni nani yuko behind ya hii motive!

Let us keep your eyes open!
"Tunapopelekwa" si penyewe...

Halafu cha ajabu wengi wa wale wanaoonyesha mwelekeo wa udini wamejiunga hapa kati ya September 2010 na sasa, je kuna azimio maalum limepitishwa la kujiunga kwenye mitandao ya kijamii ili wapenyeze hizo hila zao chafu????
 
Wanajua kuwa Dr Slaa hana vyombo vya usalama na upelelezi kuweza kutambua kuwa habari alizopelekewa kuwa si za kweli, na kutokana na kwamba zinahusu ushindi wake, walijua lazima atalizungumzia tu ili wapate sababu nyingine ya kutuambia kuwa huyu ni mlopokaji na hafai kuaminiwa.

Inawezekana pia kuwa mzigo wa hizo karatasi uko nyuma unakuja na huu uvumi umeenezwa ili baadaye ule mzigo wenyewe ukifika tukilalamika kuwa ni karatasi watuambie kuwa tumezoea kuzusha na hakuna kitu kama hicho.

Keep it up Ntemi...............that was a powerful observation of proclaiming Dr. Slaa is a "cry wolf"
 
Hata alipozungumzia EPA aliitwa mzushi na mropokaji, wajamaa waliporudisha fedha JK na wabunge wake wakagombea mgao wakijidai eti JK anapambana na ufisadi kwa vitendo!
 
Keep it up Ntemi...............that was a powerful observation of proclaiming Dr. Slaa is a "cry wolf"

We are waging a war against very clever criminals. All the brains at JF need to go into politics.... Plato once observed that

"One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors."

We must support all the brave and learned people who are entering the politics arena.
 
Dk Slaa smart bwana hawawezi kumuondoa kwenye real battle au kuharibu concentration yake, si unaona issue ya Mzee wa East Africa kufa walijua atadandia treni kwa mbele, Dk wetu walaa akaendelea kuchakachua kura kihalali kabisaa:dance:
 
Uvumi ulioenea jana kuwa kuna lori lina makaratasi ya kupigia kura Tunduma, kama kweli si za kweli basi huenda hizi zikawa ni mbinu nyingine chafu dhidi ya Dr Slaa..

Wanajua kuwa Dr Slaa hana vyombo vya usalama na upelelezi kuweza kutambua kuwa habari alizopelekewa kuwa si za kweli, na kutokana na kwamba zinahusu ushindi wake, walijua lazima atalizungumzia tu ili wapate sababu nyingine ya kutuambia kuwa huyu ni mlopokaji na hafai kuaminiwa.

Inawezekana pia kuwa mzigo wa hizo karatasi uko nyuma unakuja na huu uvumi umeenezwa ili baadaye ule mzigo wenyewe ukifika tukilalamika kuwa ni karatasi watuambie kuwa tumezoea kuzusha na hakuna kitu kama hicho.

Tunatakiwa tuwakatalie na tusonge mbele..

DR SLAA for President 2010

Mimi kama Muasisi wa Chadema nimeshawasiliana na NEC, nikishauri kwamba huyo ofisa wa TRA aliyesema karatasi hizo za Tunduma ni za kupigia kura ahojiwe na athibitishe alikuwa na ajenda gani kutoa tamko zito kiasi hicho. Tamko lake limefedhehesha na kutatanisha sana umma wa Tanzania unaotegemea haki na uhuru ktk kura za tarehe 31 Oktoba.

Kuhusu Mgombea wetu wa kiti cha u-Rais, kulaumiwa eti ni mropokaji, nategemea ktk jambo zito kama hili la kupatikana shehena kubwa ya Karatasi za kura feki, ingekuwa ni mtu asiye makini na jambo analodhamiria kufanya kama Dk. Slaa angepuuza tukio kama hilo. Ni lazima alizungumzie, kwani ni kura ndizo zitaweza kumtea ushindi.

Kama IGP Mwema amethibitisha ni uongo, basi tumwamini. Lakini Chadema na mawakala wetu siku ya kupiga kura tuchukue tahadhari ya hali ya juu, kwa vile huenda kutakuwepo na kura feki. Pia hata kama shehena yenye kura za feki kweli itafuata baadae, basi vijana wetu wawe macho pale mpakani, kwenye viwanja vya ndege n.k. ili isiwe wametugeresha tu, halafu wapitishe karatasi za kura feki baadae au mahala pengine, kiulaini.

Kauli Mbiu yetu ni ile ile: Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke!!!!!!!!!!!!
 
Mimi kama Muasisi wa Chadema nimeshawasiliana na NEC, nikishauri kwamba huyo ofisa wa TRA aliyesema karatasi hizo za Tunduma ni za kupigia kura ahojiwe na athibitishe alikuwa na ajenda gani kutoa tamko zito kiasi hicho. Tamko lake limefedhehesha umma wa Tanzania unaotegemea haki na uhuru ktk kura za tarehe 31 Oktoba.

Kama IGP Mwema amethibitisha ni uongo, tumwamini. Lakini Chadema na mawakala wetu siku ya kupiga kura tuchukue tahadhari ya hali ya juu, kwa vile huenda kutakuwepo na kura feki. Pia hata kama shehena yenye kura za feki kweli itafuata baadae, basi vijana wetu wawe macho mpakani, kwenye viwanja vya ndege n.k. ili isiwe wametugeresha tu, halafu wapitishe karatasi za kura feki kiulaini. Kauli Mbiu yetu ni ile ile: Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke!!!!!!!!!!!!
Mzee umefanya vyema kabisa.
Pamoja na hiyo taarifa ya NEC tunayosubiri. nauliza kama ni utaratibu kwa wawakilishi wa vyama kuzikagua karatasi za kura wakati zinaingizwa ili kuondoa tashwishwi ya kuibiwa ama kuchakachuliwa kura.

Pia najitahidi kumwamini MWEMA ila bado nasema kwamba kwa kuwa hakuna idara ya serikali inayofanya kazi kwa uhuru basi tuchukulie kwamba amesema na ndiyo ilivyo usoni pa nchi ila chinichini kuna INDOOR PLUMBING inaendelea,

Mungu atatuvusha salama na kushuhudia Dr. Slaa akiapishwa rais Mpya wa tano wa Tanzania kwa amani na utulivu.
 
Mimi kama Muasisi wa Chadema nimeshawasiliana na NEC, nikishauri kwamba huyo ofisa wa TRA aliyesema karatasi hizo za Tunduma ni za kupigia kura ahojiwe na athibitishe alikuwa na ajenda gani kutoa tamko zito kiasi hicho. Tamko lake limefedhehesha na kutatanisha sana umma wa Tanzania unaotegemea haki na uhuru ktk kura za tarehe 31 Oktoba.

Kuhusu Mgombea wetu wa kiti cha u-Rais, kulaumiwa eti ni mropokaji, nategemea ktk jambo zito kama hili la kupatikana shehena kubwa ya Karatasi za kura feki, ingekuwa ni mtu asiye makini na jambo analodhamiria kufanya kama Dk. Slaa angepuuza tukio kama hilo. Ni lazima alizungumzie, kwani ni kura ndizo zitaweza kumtea ushindi.

Kama IGP Mwema amethibitisha ni uongo, basi tumwamini. Lakini Chadema na mawakala wetu siku ya kupiga kura tuchukue tahadhari ya hali ya juu, kwa vile huenda kutakuwepo na kura feki. Pia hata kama shehena yenye kura za feki kweli itafuata baadae, basi vijana wetu wawe macho pale mpakani, kwenye viwanja vya ndege n.k. ili isiwe wametugeresha tu, halafu wapitishe karatasi za kura feki baadae au mahala pengine, kiulaini.

Kauli Mbiu yetu ni ile ile: Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke!!!!!!!!!!!!

Mwaasisi umenena vema.
Ingekuwa vema zaidi afisa wa TRA akakamatwa na kuhojiwa na police kwanini alitoa taarifa za uongo. Then Mwema aje atusomee ripoti ya mahojiano yake na afisa wa TRA. Nafikiri hapo ukweli utajulikana.
 
Uvumi ulioenea jana kuwa kuna lori lina makaratasi ya kupigia kura Tunduma, kama kweli si za kweli basi huenda hizi zikawa ni mbinu nyingine chafu dhidi ya Dr Slaa..

Wanajua kuwa Dr Slaa hana vyombo vya usalama na upelelezi kuweza kutambua kuwa habari alizopelekewa kuwa si za kweli, na kutokana na kwamba zinahusu ushindi wake, walijua lazima atalizungumzia tu ili wapate sababu nyingine ya kutuambia kuwa huyu ni mlopokaji na hafai kuaminiwa.

Inawezekana pia kuwa mzigo wa hizo karatasi uko nyuma unakuja na huu uvumi umeenezwa ili baadaye ule mzigo wenyewe ukifika tukilalamika kuwa ni karatasi watuambie kuwa tumezoea kuzusha na hakuna kitu kama hicho.

Tunatakiwa tuwakatalie na tusonge mbele..

DR SLAA for President 2010

sio kumchafua ni kweli anaropoka san huyu mgombea zengwe anajitengenezea mwenyewe....
 
Back
Top Bottom