Mbinu mpya ya utapeli

dany_Biggie

Member
Aug 21, 2013
55
124
Jamani, haswaa wadada mjihadhari na mbinu mpya inayo tumiwa na matapeli mtandaoni ngoja nikupe hichi kisa cha ya huyu dada kilicho mkuta hivi leo.

Dada mmoja alikuwa anachati na njemba flani kwenye mtandao wa Facebook wakaanza kudate mtandaoni kisha wakanogewa na kutaka kuonana.

Wakakubaliana kuonana, Uyo binti akakubali kumtembelea njemba huyo, Njemba akamwelekeza binti mtaa anakoishi then leo wakakutana mtaa flan hapa Arusha then huyo njemba akamuomba huyo binti mkoba wake amsaidie. Wakafika kwenye geti flan mtaa flan njemba akamwambia binti hapa ndiyo ninakoishi then njemba akasema nimesahau kununua soda akamwambia huyo dada duka liko pale ngoja nikanunue soda baridi wewe nisubiri hapa.

Njemba akaelekea njia ya dukani kisha likaingia mitini binti kasubiri mpaka kachoka uzalendo ukamshinda akaamua kugonga geti. Amegonga geti mimi ndiyo nimetoka eti anamuhulizia Kelvin. Nikamwambia aishi hapa binti wa watu ndiyo kashtuka katapeliwa.

Amelia kweli na ameondoka kinyonge eti ananiomba nimpe nauli nimemnyima hili siku nyingine awe na akili.
 
Mkuu acha hiyo roho mbaya. Nauli tu unashindwa kumsaidia wakati wewe ni shuhuda wa mkasa uliompata huyo mwanadada?
 
Pole sana sasa wewe ulimpaje mkoba wako mtu ambae ndio mara ya kwanza kumwona

Hahah.. inavyoelekea ilikuwa ni mara ya kwanza kuonana. Ila walikuwa wameshakulana sana na mno kwa style zote kunako chats za simu.

Hivyo bidada alikuwa huru na amerelax maana alikuwa na mpenzi wake.😂😂
 
Mmmmhh nauli ungempa bana, ww mwanaume wa wapi? Mtu kapata shida ya hivyo hata nauli unamnyima tena mwanamke?
 
Back
Top Bottom