Abigail2011
JF-Expert Member
- Feb 15, 2012
- 519
- 230
Wana jf salam kwenu;Jamani kumekua na mbinu mpya wanoyoitumia vibaka hapa arusha kuwapora watu hususani muda wa asubuhi na jioni mida ya saa mbili usiku hadi saa tatu hivi;Mbinu hii ni kwamba wanatumia TOYO wanabebana mshikaki mmoja kazi yake ni kuendesha na hawa wawili wana mapanga!,wanakua wanazunguka barabarani zaidi ni zile sehemu zilizojitenga kama yale maeneo ya Arusha technical college,ambapo hamna nyumba za raia karibu,wakikukuta mwanawane wanasimama na jamaa wanaku ambush kwa mapanga na kukupora kila kitu;Imewatokea majirani zangu wawili;Mmoja ilikua jioni na mwingine asubuhi akienda kazini tena huyu walimuumiza sana!.Nimeona niwashirikishe ndugu zanguni wana jf.