Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,581
Salaam wakuu. Nimeona leo tuweke mawazo hapa namna ambavyo mtu anaweza kukuibia gari yako:
1. Usiazimishe gari ovyo
Kuazimisha gari kunafanya ufunguo wako kuwa popular/exposed (kufahamika) sana na watu wengi kiasi kwamba siku wakiuchonga mwingine, hutajua ni nani kafanya hivyo
2. Simamia gari yako ikiwa kwenye matengenezo
Kuna tabia ya mtu kumwachia fundi gari wiki nzima anatengeneza tu garage kwake na wewe uko nyumbani au kazini kwa raha mustarehe. Mafundi wana kamtindo ka kupokezana sana gari inapokuwa service. Kupitia huko ni rahisi sana kudukua aina ya ufunguo wako
3. Epuka kuacha gari wazi
Unapopaki gari mjini au nyumbani au popote pale, epuka sana kuacha gari milango wazi. Kuna mafundi ni watundu wa kufungua bonet ya gari yako na kuwasha gari na kuondoka
4. Epuka kuacha ufunguo wa gari yako ukining'inia nje yamlango au kwenye switch ya gari uwapo haupo
5. Weka mfumo wa kufuatilia gari yako (car tracker) .Itakurasihishia kujua mahali ilipo gari yako pindi ikishaibiwa
6. Kata bima kubwa (Comprehensive insurance). Hii inakuweka salama kabisa na gari yako pindi inapoibiwa
Mwenye nyongeza jamani.Kiukweli kuibiwa gari inauma sana, tena sana, pia ni umaskini mkubwa.