Mbinu: Kutusua interview utumishi wa umma - PSPR

DanbyHR

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
285
388
Hello!! Mambo? Poleni na mishe za hapa na pale. Kabla ya yote napenda tanguliza shukrani zangu kwenu.

Nilikuwa naomba tupeane mbinu mbili tatu hata zaidi ikibidi namna ya kutusua kwenye usaili utumishi wa umma (Public Service Recruitment Secretariat). Hawa jamaa wana namna kadhaa ili kupata suitable candidate kwa wanavyoamini wao, kama vile written interview na oral yenyewe muda mwingine ikitegemeana na kada yako na uhitaji, unaweza fanya mpaka usaili wa vitendo, siku nyingine inakuwa oral tu.

Mimi nialianza kuapply kwa hawa jamaa mwaka huu mwanzoni mwanzoni mpaka sasa naendelea na huwa wananiita in short wananifahamu. Siku ya kwanza nafika kwenye hiyo interview pale UDSM nilikuta watu wengi zaidi ya buku 3, nikatamani nirudi home. Hiyo ilikuwa written interview, na sijawahi pita kwenda next stage, oral interview. Nimefanya pepa zao hawa jamaa kama 9 toka niitwe kwa mara ya kwanza.

Pepa yangu ya kwanza nilitusua 13, nikasema sio mbaya kwa kuwa ndo nimeanza. Matokeo ya pepa ya pili hayakuwa mabaya sana. Nikatafuta nyuzi kadhaa zilizowaongelea hawa jamaa na pepa zao nkapata nkasoma, nkafanyia kazi yale yaliyoandikwa. Yaani nikawa nondo najua mambo mawili matatu kuhusu pepa zao na maswali yao. Issue ikawa namna ya kutusua kupita mchujo.

Pepa yao ya juzi miezi kadhaa Security Officer II nilijinoa week nzima, nikapiga pepa pale DUCE nikatoka na 54 ila sikuwa selected maana yake walichukua watu wanne tu kwenda oral, nikalaani kichizi maana yake mara nyingi wanabeba kuanzia 50.

Hivyo niko hapa kuomba mbinu namna ya kutusua kwenye pepa zao. Maana yake pepa inakuwa na maswali 4, 5 au 6 ikitegemeana na siku hiyo wamekujaje alafu dakika 40 tu. So muda unakuwa hautoshi. Unafanyaje kumaliza maswali yote? Au una mention majibu yako unatembea?

Kichwani nakuwa sielewi elewi nimention au niandike maelezo kama swali linavyotaka. Maana yake maswali yote yanakuwa ya essay. Waliotusua kwenda oral ushauri tafadhari.

Asante.
 
Mbinu ya kwanza uwe unajua vitu. Kama unajua vitu unakua ni rahisi kushusha nondo na kumaliza maswali manne yote vizuri ndani ya muda

Mbinu ya pili andika majibu tu kwenye pepa, usiweke stori na mbwembwe.

Mbinu nyingine ya mwisho ni kumtumainia Mungu maana akikuandikia kupita utapita tu.
 
Kila mtu akimtumainia Mungu nani atapita nani ataachwa?
Mbinu ya kwanza uwe unajua vitu. Kama unajua vitu unakua ni rahisi kushusha nondo na kumaliza maswali manne yote vizuri ndani ya muda

Mbinu ya pili andika majibu tu kwenye pepa, usiweke stori na mbwembwe.

Mbinu nyingine ya mwisho ni kumtumainia Mungu maana akikuandikia kupita utapita tu.
 
Pale nikusoma sana madesa mitihani yao imeshiba yani soma sana unatoboa mimi nashukuru Mungu nilifanya moja nakupata kazi ila nlisaidiwa sana umu jf kupata muongozo
 
Eenhe!! Pazuri hapo, fanya kunipa baadhi ya muongozo uliopata kama unakumbuka mkuu...
Pale nikusoma sana madesa mitihani yao imeshiba yani soma sana unatoboa mimi nashukuru Mungu nilifanya moja nakupata kazi ila nlisaidiwa sana umu jf kupata muongozo
 
Pale nikusoma sana madesa mitihani yao imeshiba yani soma sana unatoboa mimi nashukuru Mungu nilifanya moja nakupata kazi ila nlisaidiwa sana umu jf kupata muongozo
Habari, eti wapi naweza pata past paper zao hawa jamaa nimeitwa written naogopa kichizi
 
Back
Top Bottom