Mbinguni ni wapi?

Mbinguni ni wapi?

Salute comrades,

Da'Vinci
wala hata usipoteze Muda ndani ya biblia hakuna mahala popote ilipoandikwa Mbinguni ni wapi zaidi ya kuandika tu uwepo wa huko mbinguni na kuwa ni juu tu! hakuna mahala ndani ya biblia inasema mbinguni ni mbingu ya tatu au hata ya saba labda kwenye vitabu vingine vya dini zingine
 
Mi nikizungukwa tu na wadada wenye makalio kama watatu naona tayari nimeshajitengenezea kambingu kangu
 
Ni huko juu alipoenda Yesu , kwa sasa mbinguni kumejaa, sijui sisi tutaenda wapi!
 
Jibu la Biblia
Katika Biblia, neno “mbingu” linatumiwa kumaanisha mambo matatu: (1) mbingu halisi; (2) makao ya kiroho; na (3) cheo kilichokwezwa au kutukuka. Katika kila kisa, muktadha unatusaidia kutambua ni maana gani iliyokusudiwa. *
  1. Mbingu halisi. Katika kisa hiki, “mbingu” zinawakilisha angahewa, mahali ambapo upepo unavuma, ndege wanaruka, mawingu yanatokeza mvua na theluji, na umeme. (Zaburi 78:26;Methali 30:19; Isaya 55:10;Luka 17:24) Inaweza pia kumaanisha anga za juu, mahali ambapo kuna “jua na mwezi na nyota.”—Kumbukumbu la Torati 4:19; Mwanzo 1:1.
  2. Makao ya kiroho. Neno “mbingu” pia linawakilisha mbingu za kiroho, au makao ya kiroho, eneo ambalo liko juu zaidi na nje ya ulimwengu halisi wa kimwili. (1 Wafalme 8:27; Yohana 6:38) Mbingu hizo za kiroho ni makao ya Yehova Mungu, ambaye ni “Roho.” Pia ni makao ya malaika ambao ni viumbe wa roho walioumbwa na Mungu. (Yohana 4:24; Mathayo 24:36) Nyakati nyingine, “mbingu” hurejelewa kama viumbe hai kuwakilisha malaika waaminifu, “kutaniko la watakatifu.”—Zaburi 89:5-7.
    Biblia pia inatumia neno “mbingu” kurejelea hasa sehemu fulani ya makao ya kiroho ambapo Yehova mwenyewe anakaa, “makao yake.” (1 Wafalme 8:43, 49;Waebrania 9:24; Ufunuo 13:6) Kwa mfano, Biblia ilitabiri kwamba Shetani namalaika waovu wangetupwa kutoka mbinguni, na hawangeruhusiwa tena kuingia mbele ya Yehova. Hata hivyo, bado wangeendelea kuwa katika makao ya kiroho.—Ufunuo 12:7-9, 12.
  3. Cheo kilichokwezwa au kutukuka. Maandiko yanatumia neno “mbingu” kuwakilisha cheo kilichokwezwa, hasa kuhusiana na mamlaka ya kutawala. Mamlaka hiyo ni kama ile ya:
Mbinguni kukoje?
Makao ya kiroho yana utendaji mwingi sana. Yana mamia ya mamilioni ya viumbe wa roho ‘wanaolitenda neno lake Yehova.’—Zaburi 103:20, 21; Danieli 7:10.
Biblia inafafanua mbinguni kuwa mahali palipo na nuru nyingi sana. (1 Timotheo 6:15, 16) Nabii Ezekieli alipokea maono ya kimbingu yaliyokuwa na “mwangaza” uliong’aa sana, naye Danieli aliona maono ya mbinguni yaliyokuwa na “mto wa moto.” (Ezekieli 1:26-28; Danieli 7:9, 10) Mbinguni ni mahali patakatifu, au safi, na maridadi.—Zaburi 96:6; Isaya 63:15;Ufunuo 4:2, 3.
Mandhari inayofafanuliwa katika Biblia kuhusu mbinguni ni yenye kustaajabisha. (Ezekieli 43:2, 3) Hata hivyo, haiwezekani kwa wanadamu kuelewa jinsi mbinguni kulivyo kikamilifu, kwa kuwa hisia zetu hazina uwezo wa kuelewa kabisa makao ya kiroho yalivyo.
 
Nani amekwambia mungu aliwazuia kufika mbinguni na je umesoma ukaelewa lengo la mungu kukasirishwa na huo mpango wao na ulisikia wapi hayo madege yamefika au yana pita mbinguni na umepata wapi vipimo vya umbali wa mbinguni na mbona hau ulizi kuhusu jehanamu iko wapi any way soma biblia na uliza kwa wasomi wa biblia
 
Hata mfalme Suleiman aliwahi kujiuliza maswali Kama yako na tafasiri yake ipo hv
Ukisoma biblia ya kiingereza kwenye hiki kitabu hapa
1KINGS 8:26 "
“But will God indeed dwell on the earth? behold, the heaven and heaven of heavens cannot contain thee; how much less this house that I have builded?”
Kwa tafasiri Sasa hayo maneno niliyoyapigia mstari ndio panamsingi wa baadhi ya majibu,biblia imesema "Heaven"(mbingu ya kwanza,then "heaven"(mbingu ya pili) halafu "of heavens" hii haimaanishi mbingu ya tatu hiyo "s" mwishoni inaweza kuwa 3,4,5,6...... Nakuendelea kwahiyo Kama biblia inasema mbingu hazimtoshi inamaanisha haishi mbinguni!
 
Unaelelea unasoma Biblia lakini huielewi au huna maono. Biblia imetoa mwelekeo wa Mungu alipo na ni nini. Soma Yohana 4: 20 - 23. Yesu akiwa kisimani na Mwanamke wa msamaria. Alisema watu wamwabudio Mungu wa muabudu kwa njia ya Roho na Kweli kwa sababau Mungu ni Roho.

Kama Mungu ni Roho inamaana yuko Rohoni in other words Mbiguni ni Rohoni. Roho sio mahali bali ni ile hali ya kuwa. (To be) ni consciousness. Juu mbinguni ni sawa na kusema high consciousness.

Sehemu nyingine kwenye biblia wametoa mwelekeo ni ufunuo 1:9 na kuendelea pale mtume yahona alipokuwa anamuabudu Mungu kwa njia ya Roho. Kuna kitabu kinaitwa Ghospel of Thomas kina mafundisho ya yesu akiwaambia wanafunzi wake ufalme wa Mungu uko ndani yao na nje yao, ila kuupata lazima wajijue angalia attachment.
Screenshot_20201107-165522_Drive.jpg
 
Mbinguni ni kule unakokuona ukiwa umefumba macho tu.
 
Yaani ulivyosema tu Gospel of Thomas baasi nikajua umekuwa brainwashed na hayo mavitabu ya kando kando! Soma vizuri biblia utaona Mungu anapoishi Ila sio Rohoni ,Rohoni hapawezi kumtosha Mungu.

Mungu akisema amekaa ndani yako haimaanishi yupo ndani ya roho yako maana yake kaweka neno lake ndani ya moyo wako akufundishe na kukuongoza vizuri,na ukisema Mungu anaishi mbinguni unakosea maana biblia inasema mbingu na ardhi vitapita Ila yeye hatapita Sasa unamuwekaje ndani ya kitu ambacho kitaisha???

Wakati anaumba mbingu na ardhi na vyoote vilivyomo alikuwa wapi?? Inamaana alikuwa nje ya hivyo vitu Sasa unamuwekaje ndani ya vitu alivyoviumba mwenyewe?? Huoni unampunguza ukuu wake????

Mungu aliumba Muda inamaana alipo yeye hakuna Muda yupo kwenye umilele na milele alikuwepo kabla ya uumbaji (zaburi 90:2) "TANGU MILELE NA HATA MILELE WEWE NI MUNGU" biblia ya kiingereza imeandika vizuri inasema "FROM EVERLASTING TO EVERLASTING YOU'RE GOD"!!!!!
Don't try to narrow God to his creation Brother
 
Chungu kimeumbwa kwa udongo ila kimefinyangwa na mafinyanzi. Kati ya mfinyanzi na Chungu kuna nafasi na Muda uliotimika kufinyanga. Kati ya Mungu na maumbile yake hatenganishi nafasi au muda. Ni moment au infinity state.

In your words una maana Mungu katufinyanga sio katuumba. Katufinyanga then yuko somewhere else.

Nimenukuu Ghospel of Thomas for understanding, mbona hujapinga nilipo nukuu kitabu cha Yohana. Spirituality can be drawn from many books, but the only reference i rely is within me. I WALKED THE PATH AND I REACHED THE TRUTH. AND I FIND IT TO BE ONE. No matter what is the color.

Ubarikiwe sana.
 
Na huu ndio ukweli,mbinguni imo ndani yako,,sio huko mawinguni
Kuna mtu hapa anasema nimekuwa brain wash. Kisa nime refer Ghospel of Thomas, Hajiulizi why RC wana Biblia yenye vitabu 72 na wa Lutheli Biblia yao ina vitabu 66? Nani aliamua na kwa manufaa ya nani? Kwani waliluwepo wakati vinaandikwa? Any way;-

Sisi ni wana wa Mungu. Miungu yaani Baba, Mama na Roho mtakatifu wameumba hekalu (MWILI amboa utokao kwa mbegu ya Baba na Yai la Mama), Roho mtakatifu akaweka Roho yaani Mungu mwana, kwa njia hiyo mwana atatakaswa ili amrudie Mungu Baba ili wawe Wamoja mbinguni. Its called ONENESS which is Our purpose in life, but is not happening that way, because other thing is merging between the two, The MIND, which belong to the physical or finity world (satan) take the control of the humbly Son of God so that instead of the serving the high purpose, he serve the needs of the Body possetions, richness, fame, positions which at the ends benefit the finity world the SON leave empty so the finity world win the infinity looses.

Only the choosen ones break the loop. Be among them.

This the story for 2 night friend Elungata. Sleep well.
 
Achana na vitabu 66 na 72 tutarudi kwenye historia na mapokeo tu chamsingi unatakiwa ujue Mungu hapingani na maneno yake mwenyewe maana kasema yeye sio mwanadamu mpaka aseme uongo kwahiyo vitabu vyoote ndani ya biblia vinatakiwa viwe in harmony to each other sio hiki kiseme hv kingine kiseme vile halafu vyoote vimnukuu Mungu huyo huyo then hapo Mungu atakuwa kafitinika!
Nimeona pia nimeona umeandika kuhusu utatu wa Mungu umeandika Mungu mwana,Mungu Baba then na Roho mtakatifu unauhakika na ulichoandika unakijua??? Nakuuliza hivi maana nikikuuliza nipe andiko lolote ndani ya biblia linalosema Hayo maneno utakuwa huna! Hamna mahali popote ndani ya biblia pameandika Hivyo!
Ukisema Mungu mwana,Mungu baba,na Roho mtakatifu maana kunakuwa na Miungu watatu Sasa halafu hapo hapo unasema Mungu ni mmoja! Wakati maandiko yanasema Mungu ni Mmoja tu na wala hajagawanyika! Wala Hana msaidizi wala Hana mshirika!
Ndiomaana nasema umekuwa brainwashed maana unayoyaandika hayapo ndani ya maandiko matakatifu sijui umeyatoa wapi????!
 
Back
Top Bottom