Mbinguni ni wapi?

Mbinguni ni wapi?

Mbinguni ni kanisani kwa nabii yaspi Paulo bendera yupo buza kipera mnara wa voda, ndipo Mungu anaishi hapo na malaikwa wanamhudumia.
 
Wacha kudumaza ubongo hakuna kitu kisicho wezekana ukiweka nia thabiti...
Ungejua mechanism of brain usingesema hivi..vingine hatuwezi kujua..ukifikiria sana unweza kupalalaizi..limity ya brain kutambua vitu inaangukia kwenye faith..
Wapi wapi mwanasayansi hawckings.
 
Ndiko huko mkuu
15bc278942cc2fc8149092a1d85802e0.jpg
 
Salute comrades,

Wakuu, naomba kufahamishwa, Mbinguni anapoishi Mungu ni wapi?

Ukisoma Biblia, Katekisimu etc zinasema Mungu yupo Mbinguni na mahali pote duniani. Je Mbinguni ni wapi?

Ni kule juu angani kwenye mawingu? Qur'an inasema zipo Mbingu saba na Mungu anaishi Mbingu ya saba, je Mbingu hiyo iko sehemu gani?

Pia tunaambiwa Nimrod na wenzie walijenga mnara ulikua unakaribia kufika Mbinguni kwa Mungu, je huko Mbinguni ni kule juu angani?

Kama Mbinguni ni huko juu angani mbona sasa hivi kuna vifaa mbalimbali ambavyo vinapita huko angani kwenda sayari zingine?

Mbona Mungu hayazuii kama alivyowazuia kujenga mnara wa Babeli sababu wanapita huko angani inaposadikika ndio Mbinguni.

Da'Vinci
Mbingu ya kwanza ndio hii tunayoishi mimi na wewe na wengine tunao waona.hii tunaiita physical plane frequency zake nimezisahau kidogo(..mhz) hapa vitu vinamove verry slow kiasi kwamba brain inaweza kudetect na limity yake ni speed of light..mbingu ya pili ni astra plane hii mbingu vitu vinameve very fast kiasi kwamba brain na sensor zake aziwezi kudetect au ikitokea imedetect brain itakwambia ni hallucination or dream..vitu hapa vinamove at higher speed of light inamaana mtu akiwa katika mbingu hii anaweza kutravel past present au future ya physical plane..mfano mtu akiwa anakufa huwa anaona yoote ya nyuma aliofanya mabaya au mazuri(past time travel) zimebaki plane tano nimechoka kueleza..ila chamsingi mbingu sio mawingu yale ya atmosphere (biosphere ionosphere etc) iliomaanishwa ilitamkwa hivyo kwenye vitabu kutupatia picha tu kwamba kunamatabaka may be kutokana na uprimitive uliopo kipindihicho.
NB:haya nlioandika ni mafikirio yangu tuu ..nahofia huenda ikawa sio kweli MWINGI WA REHMA AKANIADHIBU kwa kumsemea uongo.
 
Kuna mtu alishawahi fika pale ktk ile buluu
Ile blue ni atmospheric light scatered..anga inachuja mwanga wa jua wenye rangi saba na kubakisha blue yenye high frequecy...wale wanaopaa kwa rocket wakiipita atmosphere ya dunia huko juu kunakuwa kweusi
 
Minjibu vizuri ila nna maswali mawili tu
1. Ikiwa rangi ya buluu imebaki kule juu inamaana humwanga unaotufikia sisi hapa ardhini?
1. Mbona nikienda pale city light clock tower kuna mataa mengi mle ndani yanawaka ila sioni hiyo scattering ya buluu?
 
1. Huo mwanga unatoka kwenye Jua na ulivyo mkali ukiutazama kwa macho ya kawaida ungekuwa kipofu na mwili wako haungeweza kuuhimili, lakini ukikaribia dunia kuna kuuchuja mpaka unapata ulio salama!.. hebu fatilia ishu za Ozone layer na Ultraviolet rays.
2. Hizo taa umefatilia zinaundwa na rangi ngapi na intensity+ukubwa wake kuweza kukufanya uone rangi ya blue!?..Ni taa nyeupe zinazotoa mwanga mweupe blue huwez iona lakini let say ugeuke sisimizi/siafu kuna chance ukaiona blue pekee
 
Mkuu ule ni urefu wa macho yako, Dogo wa futi 3 na wewe wa futi 6 mtaona tofauti kitu kimoja!..Hebu sumbua bando lako tafuta hii kitu Rayleigh Scattering!..
Kuna vitu vinahitaji kufikiria zaidi ya elimu ya mzungu, ila nna maswali mengi ngoja kwanza nianzie hapa, kwani scaterring iwe kwa blue tu? Je scatterung inatokea karibu na uso wa jua au dunia?
 
Salute comrades,

Wakuu, naomba kufahamishwa, Mbinguni anapoishi Mungu ni wapi?

Ukisoma Biblia, Katekisimu etc zinasema Mungu yupo Mbinguni na mahali pote duniani. Je Mbinguni ni wapi?

Ni kule juu angani kwenye mawingu? Qur'an inasema zipo Mbingu saba na Mungu anaishi Mbingu ya saba, je Mbingu hiyo iko sehemu gani?

Pia tunaambiwa Nimrod na wenzie walijenga mnara ulikua unakaribia kufika Mbinguni kwa Mungu, je huko Mbinguni ni kule juu angani?

Kama Mbinguni ni huko juu angani mbona sasa hivi kuna vifaa mbalimbali ambavyo vinapita huko angani kwenda sayari zingine?

Mbona Mungu hayazuii kama alivyowazuia kujenga mnara wa Babeli sababu wanapita huko angani inaposadikika ndio Mbinguni.

Da'Vinci
" Mbinguni ni mahali ambapo amepafanya mungu kua makazi yake amepachagua yeye ili kupaishi pamoja nakuwa umeandika kama msomi na mwandishi mzuri lakini umeshindwa kujua alipo mungu; Niwazi kwamba khabari za mungu umezigusagusa haujazisoma na kama umezisoma sio katika kitabu sahihi na usidhani tutakuelekeza alipo kwakuwa huwezi kwenda ukiwa hai kwanza ufe ...

" Kuusu vifaa kwenda angani sio hoja kabisa kwakua haviendi kwalengo la kumtafuta mungu ni ishu nyingine za kisayansi ambazo sio zote zinaaminika tatizo mambo mnayo yasoma katika vitabu vya watu mbalimbali wenye kuandika na kukana uwepo wa mungu vimekuharibu akili sana kwamaana hiyo una mashaka flani yasio na hoja za msingi ...

* Kuusu mungu kuzuia vitu hivyo hajashindwa kufikiri kwako ndiko kumeshindwa tatizo wenye kuvirusha wana mawazo kama ya kwako hivyo huachwa wateseke na ujinga ambao ni mzingo mkubwa kwao kumbuka pia khabari za mungu amezifunua kidogo sana kwetu sisi wanaadamu hata aishipo yeye huko ambako kunakutatiza wewe ni wajibu wako kujifunza kumuusu zaidi ..

" Kuusu Quran na biblia kuthibitisha kwamba mungu yupo juu ni kweli ila nasikitika hukuelewa makusudio ya aya ulizo zisoma kwa upana wake chakufanya jitahidi sana kusoma mana huna elimu inayohusu mambo ya imani naomba kuwasilisha ...
 
Kuna vitu vinahitaji kufikiria zaidi ya elimu ya mzungu, ila nna maswali mengi ngoja kwanza nianzie hapa, kwani scaterring iwe kwa blue tu? Je scatterung inatokea karibu na uso wa jua au dunia?
Mkuu umesoma hicho kitu nilichokupa ukitafute?...Mbona jibu lipo humo!...Unabadiri topic ya Da'Vinci sasa!..
 
Kuna vitu vinahitaji kufikiria zaidi ya elimu ya mzungu, ila nna maswali mengi ngoja kwanza nianzie hapa, kwani scaterring iwe kwa blue tu? Je scatterung inatokea karibu na uso wa jua au dunia?
Miale inayokuja duniani in rangi mbalimbali lakini rangi ya blue ina wavelength fupi hivyo inakuwa rahisi kutawanywa hiyo inapelekea macho yako kuona rangi ya blue lakini kiukweli kuna rangi nyingi!...Umeshajiuliza nini kinatokea unaona Upinde wa Mvua (rainbow)?. Hebu ingiza translate hiki kipande!.
The sunlit sky is blue because air scatters short- wavelength light more than longer wavelengths. Since blue light is at the short-wavelength end of the visible spectrum, it is more strongly scattered in the atmosphere than long-wavelength red light. The result is that when looking toward parts of the sky other than the sun, human eye perceives them to be blue.
 
Hayo yaliyomo humo hayajibu hayo maswali yangu mkuu halafu wengi hua hamkielewi huchi kitabu vuzuri nikipita wasaa nitakichambua...
1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
Ufunuo wa Yohana 21 :1

2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Ufunuo wa Yohana 21 :2

3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Ufunuo wa Yohana 21 :3
Mbinguni ni eneo flani hivi la kiroho, huwezi kupaelewa kwa kutumia hizi akili za kibinadamu (ambazo ni batili)

Tengeneza maisha yako ya kiroho vizuri then yamkini malaika wa Bwana wanaweza kukuchukua siku moja na kukuonesha uzuri wa mbingu! JITAHIDI KUTENGENEZA ROHONI KILA LEO
 
Roho ni nini?
 
Back
Top Bottom