Mbilia bell v/s Tshala mwana

Mbilia bell v/s Tshala mwana

Huo ni Nadina.

Hao jamaa ni talented kweli kweli na wala siyo maigizo. Kama ni Vocal ni Vocal ya ukweli, mtu ananata na beats ananoga na kukolea kushingo.

Asante mkuu kwa kunikumbusha, ndio wimbo huo unaitwa "Nadina".

Hawa wamama mwimbaji ambaye angekula nao sahani moja ila akokasa nyenzo ni SAIDA KALOLI.
 
kweli kabisa Masuke mfano kitu kama boyaye kuanzia mpangilio wa sauti mpaka ala imetulia sana mpaka huwa najiuliza sana hivi hawa watu ilikuwa ni uwezo binafsi au walikuwa na maproducers wazuri sana?
Hapo hujaweka Beyanga, bado Nakei Nairobi (sisi tulikuwa tunaimba twende Nairobi, tukamwona baba Moi), uje uweke Nadina halafu malizia na Mazili Mazili pamoja na Shauri Yako. Aiseeeee Mama Mbilia Bel anajua sana uje ujumlishe na umbo lake na kasura kake kale kabla hajaanza kutumia mkorogo aise huchoki kumwangalia ndo maana mzee mzima Tabu Ley Rochereau alijichukulia kifaa.
 
Last edited by a moderator:
nikusahihishe kidogo papa mopao wimbo wa monica aliimba ndala kasheba, kama utakukumbuka vizuri ilikuwa ni kesi ya kanga na muhusika alilimbilia zambia

Mkuu nashukuru sana kunifahamisha...

Lkn maana yangu ni kwamba walimu wangu walionifanya niupende muziki wa kizairwaa walikuwa wawili, moja ni hao mapacha wa Tancut Kasalo Kyanga na Kyanga Songa na mwalimu mwingine ni kupitia kwenye huo wimbo wa Monica!

Tupo pamoja kaka, Kizairwaa ina ladha tamu sana!
 
Cindy yeye size yake ni MEJE 30,mtoto aliyekulia kwa Malkia wa Mutuashi, Tshala Mwana. Wote wana uwezo wa kuimba miziki ya manguli wao.

bila kumsahau faya tessy
 
kila mtu atamtaja wake kwa uzuri wake ni sawa na kuwafananisha werasoni na jb mpiana kila shabiki ana uchaguzi wake.
 
Wote wanajua mziki kiukweli siwezi watenganisha kiuwezo. Mimi naelekea muhongo wa tatu kiumri. Lakini mziki ya Congo na ukanda wa maziwa makuu naupenda mno hiyo yote inatokana na uwezo wa sanaa ya miaka hiyo ilikuwa ya hali ya juu. Niliipenda sana TP Ok Jazz ingawa nimezaliwa haipo lakini huwa nakumbukia nyimbo zao kibao ikiwa ni pamoja na wimbo wa kumuenzi Franco uliopigwa 1992 nikiwa nipo na akina na Nyboma na Madilu ....... Hasa kuna kipengelee nitakiandika kwa kusikika vile huwa nasikia(kimakosa)
" Madilu dikanga na acanisa Lwambo Francoo na Afrique ye mokili mobimba bakucanisayee, na ulrajaa jule na molende cola ndanda teyooo" natamani ningekuwa naelewa ningeandika kwa usahihi sana na kufafanua maana. Na nikikumbuka wimbo wa yule kiumbe Sam Mangwana alioimba Franco " Muongo na mulozi" ile wimbo huwa ikipigwa na hizi bendi zetu za Hotel huwa nalazimika kuamka na kwenda kutuza pamoja na wimbo wa mabibie wawili wa kwa Mandela yaani Brenda Fassie au Ivone Chakachaka. Jamani hivyo vizazi walijua mziki wacha nibaki niendelee na Koffi Olomide kwa kuwa ni mmoja kati ya mwanamziki ambaye amedumu viazazi vinne vya muziki ya Congo na binti Cindy aliyetolewa mahali kama heshima ya kuombwa adumu katika Bendi na sio kurukaruka . . .
Miziki iliimbwa enzi hizo nikimkumbuka marehemu anko alikuwa muheshiwa TRC na alikuwa promota wa muziki katika mkoa miaka hiyo natamani miaka irudi nyuma maana na nikienda kucheki Bendi zetu zinazopandia nyimbo za kizazi hicho napata kero ya nafsi kwa wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja nao huwa wanaudhuria sasa hata starehe ya mziki inapotea kwani roho inakuwa inakereketa kumuona mwanaume mwenzako anafanya kituko sasa hata starehe ya mziki inapotea. Nitendeleaa . . . ni RTC na sio TRC
 
Nakumbuka nilipiga picha na Mbilia Bell alivyokuja Arusha na Rigo Star, mpaka leo nikiiangalia nakumbuka mbali sana ingawa nilikuwa mtoto mdogo, Nadina naipenda sana , Kuna mwingine Beyou Cell alikuwa vizuri
 
Braza kwa sound kama mulugo vile katika ubora wake!! Ahahahha mpaka miti nayo inapiga soukous!?

Mulugo Babako! Tena Ukome Kunifananisha Na Takataka Wenzako Hao. Nini Mpaka Miti Kutikisika Hata M.A.T.A.K.O Yako Nayo Yatatikiswa Na Magitaa Ya Diblo Na Dally.
 
Sidhani kana walikuwa na maproducer wazuri sana ila walikuwa talented sana. Mfano sauti ya Mbilia Bel katika nyimbo kama Nakei Nairobi, Beyanga nk haina mfano wake.

Kuna wimbo aliuimba mara mbili kwa lingala na baadae kiswahili sijui unaukumbuka mkuu? Nakumbuka maneno kadhaa ya wimbo huo kama "majani, vidudu.......kazi ya binadamu" .

........tumuombe Mungu baba japo mara moja kwa jumaaa....
 
Wote wakali ila Mbilia zaidi! Mziki wa Zaire(DRC) ni noma,me napenda ya 2000 kurudi nyuma! Inanikonga sana.
 
Daaaah leo hapa umenifanya nifikiri tofauti ya Sukari nyeupe na ile brown. Hawa kila mtu alikuwa Shida kwake
 
Back
Top Bottom