Mbilia bell v/s Tshala mwana

Mbilia bell v/s Tshala mwana

mkuu naomba niwe mkweli tu.sidhan kama atapatikana mshind hapa.hivi vilikuwa vichwa ni sheeeda.umenikumbusha .mbali mkuu

ni kweli mkuu Kozo binafsi najaribu kufuatilia nani alikuwa na nyimbo nyingi zaidi ya mwenzake na mafanikio makubwa either ya tuzo au utajiri
 
Last edited by a moderator:
Hapo ni sheeda kupata mkali kama ilivyo kwa dally Kimoko na diblo dibala kwenye gitaa la solo.

gide hawa wote walikuwa hawazuri na ingependeza ungetuwekea na nyimbo zao ili utuwatofautishe vizuri
 
Last edited by a moderator:
Wote Nawaheshimu Ila Gitaa La Diblo Hata Waliolala Wataamka Na Kucheza Wakati Gitaa La Dally Kimoko ( Dalikike au Gitare Enzanga Likwanza ) Malaika Wote Mbinguni Wanacheza Na Vichanga Tumboni Mwa Mama Zao Vinacheka Huku Miti Nayo Ikitikisika.

dah! Mkuu hapo umenichekesha kwa maana nyingine hapo hakuna mshindi. Tatizo jengine nililoligundua ni kwamba wao kama wao hawana nyimbo binafsi mara nyingi walikuwa wanashirikishwa na kumjua huya diblo mpaka wamtaje
 
napata faraja kukutana na wadau kwenye mada kama hizi adimu kwenye huu utandawizi wa kizazi kipya.

unaweza sema Elizabeth Muidakia a.k.a Tshala Mwana alikuwa malkia wa miziki ya mutuashi inayopatikana mashariki ya kongo pamoja yale maruhani yake ya kumwaga razi akiwa jukwaani.

Mbilia Bell alikuwa chiriku, malkia wa modern congo rhumba, mkali wa kushambulia jukwaa kama Tshala Mwana vilevile. ila unaweza sema alipewa kick sana na aliyekuwa mme wake Tabu Le ama Rocherou kupata umaarufu na vibao kama Eswo yo Wapi, Wendenda, Nakei Nairobi, Nadina, Phenomena etc

Ama kwa hakika wameacha urithi na alama ambayo haitafutika ya sanaa ya muziki katika ukanda huu wa maziwa makuu.

Mafanikio ya fedha, kama mnavyojua tena kipindi hicho haya mambo ya siku hizi hayakuwepo zaidi ya kupata mpunga wa kawaida.

Tshala Mwana kuna kipindi alikuwa kwenye utawala wa Kabila Junior akizochanga faranga wakati Mbilia Bell yupo Nairobi naye akiendesha maisha yake.
 
Mama Mbilia Bel ni habari nyingine kabisa. Kuna wimbo mmoja sijui kama ni Boya ye au Eswo yo wapi unanikumbusha mbali sana. kwa ujumla mimi namkubali sana Mama Mbilia Bel.
 
unapenda dezo dezo we bwana wee yatakushinda

kodi ya nyumba hulipi maji hutaki kulipa operesheni kata inakujaa...

Tshala Mwana nuksi

Huu wimbo aliu -copy kwa Fred Ndala Kasheba! Mzee wa kombora la nyuzi dazeni
 
unapenda dezo dezo we bwana wee yatakushinda

kodi ya nyumba hulipi maji hutaki kulipa operesheni kata inakujaa...

Tshala Mwana nuksi

Tshala Mwana nafikiri ni Mkongo wa mwisho ku perform pale Motel Agip. Vijana wa bongo fleva sijui kama wanaijua hotel hiyo.
 
tupo pamoja MPUNGA kwa maelezo unaonekana unaelewa na kuwaelewa vizuri wanamuziki hawa, japo mimi si kijana wa zamani sana lakini miziki yao nilitokea na mpaka leo naipenda hususani ujumbe na mpangilio.

Hivyo bado tunategemea mengi toka kwako mkuu
 
Mama Mbilia Bel ni habari nyingine kabisa. Kuna wimbo mmoja sijui kama ni Boya ye au Eswi ya wapi unanikumbusha mbali sana. kwa ujumla mimi namkubali sana Mama Mbilia Bel.

kweli kabisa Masuke mfano kitu kama boyaye kuanzia mpangilio wa sauti mpaka ala imetulia sana mpaka huwa najiuliza sana hivi hawa watu ilikuwa ni uwezo binafsi au walikuwa na maproducers wazuri sana?
 
Last edited by a moderator:
Tshala Mwana nafikiri ni Mkongo wa mwisho ku perform pale Motel Agip. Vijana wa bongo fleva sijui kama wanaijua hotel hiyo.

ah ah kila zama na nyakati zake bullet

mkuu bullet naomba unifahamishe kitu kimoja kuhusu tshala ni kweli kuwa alikuwa na sauti nzuri sana na mpangilio wa nyimbo zake ulikuwa mzuri sana na wa kuvutia lakini ukifuatilia kwa undani utakuta ni master copy mfano dezo dezo wa ndalla kasheba na masuwa ambayo original ni ya franco na tp ok jazz japo kwenye hiyo nyimbo inasikika sauti yake.
 
Last edited by a moderator:
Mpaka sasa Maisha yanavyoenda naona wa zamani walifaidi mziki zaidi kuliko sasa.
 
Tshala mwana sijawah mchoka mskiliza mbilia anaimba vizuri sana,lkn turufu yangu nampa mbilia
 
Wote Nawaheshimu Ila Gitaa La Diblo Hata Waliolala Wataamka Na Kucheza Wakati Gitaa La Dally Kimoko ( Dalikike au Gitare Enzanga Likwanza ) Malaika Wote Mbinguni Wanacheza Na Vichanga Tumboni Mwa Mama Zao Vinacheka Huku Miti Nayo Ikitikisika.

Braza kwa sound kama mulugo vile katika ubora wake!! Ahahahha mpaka miti nayo inapiga soukous!?
 
ah ah kila zama na nyakati zake bullet

mkuu bullet naomba unifahamishe kitu kimoja kuhusu tshala ni kweli kuwa alikuwa na sauti nzuri sana na mpangilio wa nyimbo zake ulikuwa mzuri sana na wa kuvutia lakini ukifuatilia kwa undani utakuta ni master copy mfano dezo dezo wa ndalla kasheba na masuwa ambayo original ni ya franco na tp ok jazz japo kwenye hiyo nyimbo inasikika sauti yake.

Ni kweli ni copyist mzuri lakini anazitendea haki nyimbo hizo. Kwa mfano Dezo Dezo yake japo ni copy, ina utamu kuliko orginal yake ya Kasheba. In fact iliifunika kabisa ile ya Kasheba kiasi inakuwa vigumu kujua kwamba Kasheba ndio mtunzi.
 
Last edited by a moderator:
............. Wivu mwingine bwana.

Sidhani kana walikuwa na maproducer wazuri sana ila walikuwa talented sana. Mfano sauti ya Mbilia Bel katika nyimbo kama Nakei Nairobi, Beyanga nk haina mfano wake.

Kuna wimbo aliuimba mara mbili kwa lingala na baadae kiswahili sijui unaukumbuka mkuu? Nakumbuka maneno kadhaa ya wimbo huo kama "majani, vidudu.......kazi ya binadamu" .
 
Huo ni Nadina.

Hao jamaa ni talented kweli kweli na wala siyo maigizo. Kama ni Vocal ni Vocal ya ukweli, mtu ananata na beats ananoga na kukolea kushingo.
 
Ukiwasikiliza manguli kwa dakika watakufanya uione dunia kama paradiso..kwa raha utakazopata....
Heshima kwao hawa wakongwe..
 
Back
Top Bottom