Mbichi na mbivu za Jeshi la Polisi Tanzania

Blood of Jesus

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
2,955
5,877
Toka nikiwa mdogo (sasa ni mtu wa makamo) nimekuwa nikisikia mabaya tu yakisemwa kuhusu utendaji kazi wa askari polisi. Hadi leo nimeona Kamati kuu ya ccm ikitoa maelekezo kwenda kwa serikali kulihusu Jeshi la Polisi. SWALI LANGU: Je, ni kweli kuwa Jeshi la Polisi Tanzania ni hovyo kila nyakati/miaka nenda rudi?

Ninajua humu JF kuna wataalamu mbalimbali, hivyo naomba kujua kama yapo mazuri yatendwayo na PT. maana kuna nyakati hali ilikuwa mbaya hadi baadhi ya wananchi wakadai bora lifutwe yaani lisiwepo!!!!

Karibuni.
 
Waache kuajiri vilaza...

Waunde jeshi la wasomi, kwa vyeo vyote sambamba na kuongeza mishahara inayoendana na hali halisi ya maisha...

Jeshi liwe la kisasa na dogo, matumizi ya teknolojia yapewe kipaumbele zaidi...
 
Kamanda Zero ndiye tatizo. Afukuzwe awekwe mwingine mwenye uelewa mpana zaidi.
 
Waache kuajiri vilaza...

Waunde jeshi la wasomi, kwa vyeo vyote sambamba na kuongeza mishahara inayoendana na hali halisi ya maisha...

Jeshi liwe la kisasa na dogo, matumizi ya teknolojia yapewe kipaumbele zaidi...
Asante mkuu kwa kujaribu kuleta "solution". Sasa unadhani ni kwanini hayo uliyosema hayafanyiki. Maana yanaonekana yako ndani ya uwezo.
 
Waache kuajiri vilaza...

Waunde jeshi la wasomi, kwa vyeo vyote sambamba na kuongeza mishahara inayoendana na hali halisi ya maisha...

Jeshi liwe la kisasa na dogo, matumizi ya teknolojia yapewe kipaumbele zaidi...
Kwani majeshi mengine elimu na mishahara wanatofautiana na hao unaowasema.
 
Elimu ipewe kipaumbele sio kwa elimu zao za mashuleni au vyuoni tu ila huko pia kwenye mafunzo ya uaskari wenyewe.

Elimu kwa jamii ya watanzania kuwa sio askari wote ni wakatili ila baadhi yao na pia askari ni binadamu kama sisi wengine , na kazi na majukumu yao ni vyema jamii ijulishwe kwa mapana yake.

Mshahara kwa hawa watumishi ni kheri uangaliwe upya ili kuepusha tamaa ndogondogo

AHSANTE.
 
Polisi wanalalamikiwa karibia kila nchi duniani hakuna mahali ambapo jamaa wanakaa kwa amani.
 
Polisi Wana maadui ambao hawaepukiki mfano mlalamikaji anapo mlalamikia mtu Kwa tuhuma mbalimbali na mlalamikiwa akikamatwa anamchukia Polisi badala ya aliyelalamika na akishindwa kutimiza matakwa mlalamikaji lazima Polisi achukiwe na upande usiotimiziwa matakwa yake.mfano mwingine katika uchaguzi walioshindwa wanamchukia Polisi kwamba ndiyo chanzo cha kushindwa kwao.

Sababu nyingine ni mmomonyoko wa maadili katika nchi kila taasisi ina watu wa Aina hii ya BAADHI ya Polisi wanaokiuka maadili tatizo linakuwa kubwa Kwa Polisi kwasababu kila shughuli za kila siku lazima ukutane na Polisi tofauti na taasisi nyingine ambazo hazigusi MAISHA ya kila siku.

Ajila Pia ni eneo linalochangia kwakuwa wanaajiliwa bila kufanyiwa vetting ya kutosha hivyo watu wa hovyo wamepenya na kuingia kwenye taasisi hii nyeti.

Viongozi wa Polisi ni chanzo kingine Kwa kushindwa kusimamia,kupanga Askari wao kulingana na weledi wanawapangia sehemu za KAZI bila Kuwa na vigezo ndiyo maana wenyefani kadhaa wanafanyia KAZI kwenye fani tofauti na walizobobea.

Serikali imewatupa kabisa waajiliwa wa Polisi sidhani kama wanazo haki kama za watumishi wengine hali hii inawafanya kisaikolojia Kuwa wanyama.

Suluhisho ni kubadili mifumo pamoja na SHERIA zinazoendesha jeshi la Polisi Pomoja na sheria mama. Kwasasa Kwa mujibu wa katiba Serikali ndiyo yenye mamlaka ya kuunda jeshi la Polisi nk. Hivyo ni Sawa na anayefuga mbwa kutoa amri Kwa mbwa huyo kufanya lolote Kwa maslahi ya mwenye mbwa.

Pamoja na mabaya wafanyayo Polisi Tanzania jaribu Kufuatilia wanavyoishi angalia vitendea kazi vyao angalia kama wanapewa vitendea kazi vinavyokidhi mahitaji Yao?epu tufikirie mtoto wako ukimnyima chakula atafanyaje?

Mwisho kila anayekamatwa na Polisi hata kama ni kwaajili ya Makosa yake lazima aweke kumbukumbu na chuki MAISHA yake yote.
 
Toka nikiwa mdogo (sasa ni mtu wa makamo) nimekuwa nikisikia mabaya tu yakisemwa kuhusu utendaji kazi wa askari polisi. Hadi leo nimeona Kamati kuu ya ccm ikitoa maelekezo kwenda kwa serikali kulihusu Jeshi la Polisi. SWALI LANGU: Je, ni kweli kuwa Jeshi la Polisi Tanzania ni hovyo kila nyakati/miaka nenda rudi?

Ninajua humu JF kuna wataalamu mbalimbali, hivyo naomba kujua kama yapo mazuri yatendwayo na PT. maana kuna nyakati hali ilikuwa mbaya hadi baadhi ya wananchi wakadai bora lifutwe yaani lisiwepo!!!!

Karibuni.
Sema ccm ndio mbaya siyo polisi
 
Toka ukoloni mpaka miaka ya sitini jeshi la polisi lilikuwa rafiki, ukiwa na tatizo wanakusaidia, ila la! Likafundishwa uadui na ukatiri dhidi ya raia.
 
Toka nikiwa mdogo (sasa ni mtu wa makamo) nimekuwa nikisikia mabaya tu yakisemwa kuhusu utendaji kazi wa askari polisi. Hadi leo nimeona Kamati kuu ya ccm ikitoa maelekezo kwenda kwa serikali kulihusu Jeshi la Polisi. SWALI LANGU: Je, ni kweli kuwa Jeshi la Polisi Tanzania ni hovyo kila nyakati/miaka nenda rudi?

Ninajua humu JF kuna wataalamu mbalimbali, hivyo naomba kujua kama yapo mazuri yatendwayo na PT. maana kuna nyakati hali ilikuwa mbaya hadi baadhi ya wananchi wakadai bora lifutwe yaani lisiwepo!!!!

Karibuni.
Ajabu sana taasisi ya usalama kupewa amri na chama cha siasa.
 
MAZURI ya Polisi yapo lakini yanafichwa na mabaya yao mfano Kuna watu wengi waliokolewa na Polisi baada ya kunusurika kuuwawa na WANANCHI wanaoitwa wanahasira Kali.
Pia watu wengi wanaoiba Kujeruhi,kuiba,kubaka NK WAMEKAMATWA na wamechukuliwa hatua za kisheria ikiwemo Polisi wenyewe.
Misafara ya viongozi HAO wanaoiponda Polisi inalindwa na Polisi na wakati wanawatuhumu Polisi huwa wanalindwa na Polisi.
Nionavyo Mimi Polisi ni jamii ambayo inamchanganyiko wa watu mbalimbali wenye malezi mbalimbali na hulka tofautitofauti.
Ukifumua jeshi HAKIKISHA unapata Askari Polisi kutoka jamii iliyolelewa vema vinginevyo utatoa wabaya na kuingiza wabaya zaidi.
Hivi umewahi kufikiri Wale jamaa WALIOKUWA wakiwavamia Polisi na kunyang'anya Silaha wangeshinda na kuwaua Polisi wote nini kingefuata?
 
Back
Top Bottom