Mbezi Mwisho palivyonitoa ushamba

Hamna kitu mkuu, pale wanatumia uzoefu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni barabara ambayo karibia kila siku ya kazi, napita, ukitokea kibamba kabla ya kona ya kwenda standy kibao kipo upande wako wa kushoto, na kila penye mkanyiko kibao kipo, ila madereva hatusomi alama za barabatani tu.
 
Halafu polisi wamefanya mtaji, ukikosea ukaingia stand ya daladala wanakukamata
Kama wanafanya hivyo wanakosea, wanatakiwa kukuelekeza tu, maana wakikuchukua pesa hawezi kukuelekeza tena, wanachukulia umefanya makusudi.
 
Nikiwa na safari ya Mbezi lazima nitumie dereva.
Sitaki sitiresi mie.
Hapana kutoendrsha gari mwenyewe, kutakufanya uendelee, kutojua hizo njia, nimeona baadhi ya madereva wenye magari yao huko kibaha, wanaogopa kwenda na gari zao mjini.
 
Pale ukikosea kama unatoka mjini, unaenda mpaka kwa Yusufu, unakunja kushoto raund about, inakunja kushoto, utaifuata barabara ya juu, mpaka upande wa pili, hatimae magufuri.
 
Mbezi Pana round about 12 . Ukikosea kidogo umeenda Gonna au Mpiji
 
KWANINI WANAKAWIA KUWEKA MABANGO YENYE ALAMA(DIRECTION)
WALITAKIWA WAWE WASHAWEKA MUDA TU

ova
Vibao vipo vinaonesha kwa kwenda kila round about inakwambia huku wapi huku wapi tatizo madereva wengi wao wanangalia mbele tu ka maroboti...
 
Pale ukikosea kama unatoka mjini, unaenda mpaka kwa Yusufu, unakunja kushoto raund about, inakunja kushoto, utaifuata barabara ya juu, mpaka upande wa pili, hatimae magufuri.

Hiyo niliipita kwa wenge na kupanik sababu nilikuwa Lane ya kulia kuja kustuka nshaipita na siwezi ku reverse.....

Nilienda kugeuza mbele hukooo yaani sina hamu....😔😔
 
Hiyo niliipita kwa wenge na kupanik sababu nilikuwa Lane ya kulia kuja kustuka nshaipita na siwezi ku reverse.....

Nilienda kugeuza mbele hukooo yaani sina hamu....
Pole
 
Ukichelewa kujua pa kuingilia inakubidi ukageuze kwenye mataa yanayofuatia ambapo ni Mbezi kwa Msuguri au Luguruni.
 
Hakuna vibao pale.

Labda waweke leo.
 
Ukichelewa kujua pa kuingilia inakubidi ukageuze kwenye mataa yanayofuatia ambapo ni Mbezi kwa Msuguri au Luguruni.

Yaani mimi hayo yote niliyavuka, nilipaniki kuliko kupaniki kwenyewe....

Nilienda kugeuzia mbele hukooo... hata sijui wapi..
 
Hakuna vibao pale.

Labda waweke leo.
Vibao vipo, hata leo asubuhi nimepita pale ukitoka Goba roundabout ya kwanza ina vibao, roundabout ya pili ina vibao...
 
Shida husomi mabango ya maelezo na usomi alama za barabarani. In short wewe sio dereva bali mshika uskani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…