Mbezi Mwisho palivyonitoa ushamba

Kama unatokea Goba unaweza pia kuvuka daraja la kwanza then ukakata kushoto, utazunguka ile round about ya zamani, ukishaizunguka ukiwa kama unarudi Goba utaona kanjia mchepuko kushoto kwako kwa chini ukitambaa nacho kinakupeleka Malamba mawili, daraja la pili ulipopita kuzunguka kwa Yusuf mbali sana kule.
 
Tatizo ni udereva wa kukariri, hatuangalii vibao, tunaendesha kwa mazoea. Mbezi panajieleza sana. Kwa sisi tunaopita hapo daily hakuna shida, mgeni lazima usome vibao la sivyo utazunguka sana hasa kama unatokea Town unaenda goba, unatokea goba unaenda kinyerezi, unatokea kibaha unaenda kinyerezi, unatokea kinyerezi kuelekea goba au mpigi nk.
 
Inasikitisha sana.
Mimi nimekariri kuna kibao cha Goba ndo nakifata.
Chap naingia stand.
 
Ina maana leseni uliletewa nyumbani?

Mbona pale alama zaonesha vizuri tu
 
Kumbe tupo wengi, me pia kuna siku nimetoka njia ya Goba naenda Tabata..
Mbona jasho lilinitoka...
Sitaki hata kupasikia.
Mbona maelekezo yapo, vibao vingi sana
 
Inasikitisha sana.
Mimi nimekariri kuna kibao cha Goba ndo nakifata.
Chap naingia stand.
Kama una mda hujapita usiende kwa kukariri tena, usome vibao. Kama hutasoma vibao unaweza kupata shida kidogo. Au unishtue nikupitishe pale...
buku tu nitaridhika mkuu!!
 
Mkuu hizi cross roads huwezi kupotea kabisa maana alama zipo ni kubwa na zinaonekana, halafu wenzetu wanatumia mabango ya rangi ili kuzitofautisha hizi barabara, mf. Blue color hizi ni highways/freeways, means hata ukiwa kwa mbali utaona na kujua kuwa off ramp ile itakuingiza free way
 
Hahahaaaaaaaaaa, daaaah, umenichekesha sana aisee,

Anyway ndo njia yangu everyday, na nimebahatika kushuhudia mabadiliko yooooote yanavyotokea, ila kuna siku nilijisemea Hizi njia kama mtu hajapita loooong time lazima aipate fresh !

Pole aisee
 
Shida ndio hiyo iliyonikumba ,lakini pia alama sio kubwa sana,baada ya kutaka kwenda stand ya daladala ndio akili ikanirudia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha ha dah umenichekesha sana,pole sana kwa mkasa huo ndugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapajakaa vizuri kama umetoka Kibaha kwenda Tabata. Mimi baada ya kuona shida sana nikitoka Kibaha kwenda Tabata huwa napitiliza mpaka kwa Msuguri kwenye mataa pale napinda kulia kuna barabara mpya ya lami inatokea malamba mawili.
Itabidi tuungane kupita hiyo hiyo kwakweli .pale panakausumbufu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole aisee, lakini pia, ungeweza baada ya kuvuka daraja la kwanza namkuikuta round about, ungefuata uelekeo wa njia inayokuja tokea barabara kubwa, lakini kabla hujaifikia round about kubwa ya zamani ungeona barabara inayoshuka upande wa kushoto ambayo inaenda kupita chini ya daraja (la barabara inayoenda stendhal ya daladala) ambayo ukiifuata ungeweza kuelekea maramba mawili pia,

But inahitaji maelekezo kwakweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…