Mbezi Beach: Mitaa yakosa maji baada ya bomba kubwa kupasuka wakati wa ujenzi wa barabara. DAWASCO ingilieni kati

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,654
9,254
Mbezi beach mtaa wa Bondeni jirani na kituo cha daladala kuna shughuli za ujenzi wa daraja la juu (fly over).

Katika shughuli za ujenzi huo wakati wakichimba mtaro mafundi walikosea wakatoboa bomba kubwa la maji (main pipe) pakatokea mafuriko,Sasa tokea juzi wamekata maji na wananchi hawakuwa wamejipanga na hawakuwa na taarifa yoyote na kuna dalili za wao kutumia siku nyingi kuziba hiyo sehemu au inawezekana wakakaa kimya kabisaa na wakaendelea shughuli zao nyingine huku wananchi wakiendelea kuteseka kwa ukosefu wa maji na sijajua kama wanamamlaka halali ya kukata maji.

DAWASCO tunaomba mlifanyie kazi hili jambo mitaa kadhaa haina maji mpaka sasa, kama hamkuwa na taarifa basi fuatilieni.
 
Mimi imetokea barabara ya feza nyuki wakaja baada ya kuja wanasema tutowe pesa tuwalipe kwa ufundi wakati maji yao kwanza unaweza waita wakachukuwa mwezi
 
Ahh uko kwa mabosi wanaweza nunua kwenye tank zinazo tembeza, alafu mna kelele sisi huku kwa mwezi mara mmoja na yanakuja yakiwa machafu, mwanaume kugangamara tuliipendaa wenyewe wacha tuisome wote
 
Back
Top Bottom