Mbeya: Watoto wamchoma moto mama wa kambo

Kukasirikiana na mzazi wako unaona sifa?
Sijakasirikiana nae. Au unataka na mimi nikagombee mali.
Kwa hiyo nawewe wale watoto wako watatu wenye mama tofauti huna habari nao makusudi ili badae uwaambie wasikukasirikie?
 
Step mother nao wanakuaga nao wakatili wapo after mali
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili

1. EZEKIA LIZER [20] 2. BARAKA EZEKIA [24] wote wakazi wa Tarafani Mji Mdogo wa Mbalizi kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kutumia moto DAINES ROBERT MDEE [26] Mkazi wa ZZK ambaye ni Mama yao wa kambo kutokana na mgogoro wa mali za familia.

Tukio hili limetokea mnamo tarehe 18.10.2020 majira ya saa 06:00 asubuhi huko eneo la ZZK

– Mbalizi, Kata ya Utengule Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. Ni kwamba chanzo cha tukio hili ni mgogoro wa mali za familia zilizoachwa na mume wa mhanga baada yakufariki dunia hivyo watoto wa marehemu [watuhumiwa] kumtuhumu mhanga kutumia hati za nyumba za marehemu Baba yao kukopea pesa Benki kiasi cha Tshs.Milioni 40 na baadae kuondoka na kuacha Benki ikitaka kuuza nyumba hizo.

Kutokana na kitendo hicho, watuhumiwa walimvizia mama yao wa kambo wakati anaenda kufungua duka kisha kummwagia mafuta ya Petroli ujazo wa lita 10 yaliyokuwa kwenye ndoo na kisha kumchoma moto kwa kutumia kiberiti.

Mhanga amelazwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matabibu. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

​

Chanzo: Global Tv online
Upelelezi gani tena ukamilike, no wonder kesi huwa zinachukua muda kutolewa hukumu
 
Hakuna mama wa kambo hapo wote ni watoto wa marhemu. Wana umri sawa! Pole yao hao boys, maisha yashaharibika tayari!
Hawa mama wa kambo ni watesaji huenda amavitesa sana hivi vitoto, ndiyo maana wakatumia njia ya kumtia moto
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili

1. EZEKIA LIZER [20] 2. BARAKA EZEKIA [24] wote wakazi wa Tarafani Mji Mdogo wa Mbalizi kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kutumia moto DAINES ROBERT MDEE [26] Mkazi wa ZZK ambaye ni Mama yao wa kambo kutokana na mgogoro wa mali za familia.

Tukio hili limetokea mnamo tarehe 18.10.2020 majira ya saa 06:00 asubuhi huko eneo la ZZK

– Mbalizi, Kata ya Utengule Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. Ni kwamba chanzo cha tukio hili ni mgogoro wa mali za familia zilizoachwa na mume wa mhanga baada yakufariki dunia hivyo watoto wa marehemu [watuhumiwa] kumtuhumu mhanga kutumia hati za nyumba za marehemu Baba yao kukopea pesa Benki kiasi cha Tshs.Milioni 40 na baadae kuondoka na kuacha Benki ikitaka kuuza nyumba hizo.

Kutokana na kitendo hicho, watuhumiwa walimvizia mama yao wa kambo wakati anaenda kufungua duka kisha kummwagia mafuta ya Petroli ujazo wa lita 10 yaliyokuwa kwenye ndoo na kisha kumchoma moto kwa kutumia kiberiti.

Mhanga amelazwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matabibu. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

​

Chanzo: Global Tv online
[/QUOT

Jingaz! Yaani Wanaume wawili wa.nashindwa kumdhibiti mwanamke mmoja was rika lao hadi kutaka kumchoma kwa petroli!!
Ngoja sasa wakacheze na moto !!
 
Kijana tafuta mali yako mwenywe wakati ukiwa hai. Mali ya baba na mama iwe ya baba na mama tu.
 
Hapo maam wa kombo roho yake kwatu kabisa mpaka hao madogo watoke nyumba ishapigwa mnada..
 
Sijakasirikiana nae. Au unataka na mimi nikagombee mali.
Kwa hiyo nawewe wale watoto wako watatu wenye mama tofauti huna habari nao makusudi ili badae uwaambie wasikukasirikie?
Mi sijaona ukisema mnagombea mali nimeona ukisema we na mzee wako mligombana na hadi leo hujui anaishi wapi
 
SOMO KUBWA HAPA: Wazee endeleeni kuoa watoto wadogo sawa na umri wa watoto wenu!!
 
Mi sijaona ukisema mnagombea mali nimeona ukisema we na mzee wako mligombana na hadi leo hujui anaishi wapi
Mzee wangu anaishi kwake ambapo sipakumbuki kwa kuwa nilitoka nikiwa mdogo. Na hatukugombana wala simchukii ila hatuwezi kaa wote akiwepo mke wake. Mtu kashasema nisimtafute kwa kuwa anajua nipo sasa kwa nini nisiwe muelewa
 
Mbeya, Mbeya, Mbeya!

Nasikia Police Commander Mbeya (RPC) aliondolewa kwa amri toka juu baada ya kukataa kuwakamata wafuasi wa Chadema kwenye suala la kuchugua form za kugombea?
 
Wee endelea kusikia tu,
 
1. EZEKIA LIZER [20] 2. BARAKA EZEKIA [24] wote wakazi wa Tarafani Mji Mdogo wa Mbalizi kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kutumia moto DAINES ROBERT MDEE [26] Mkazi wa ZZK ambaye ni Mama yao wa kambo kutokana na mgogoro wa mali za familia.
Mtoto Miaka 20
Mtoto Miaka 24
Mama Miaka 26
Kuna jambo la kujifunza je baba alikuwa na umri gani?
 
Back
Top Bottom