Mbeya: Watoto wamchoma moto mama wa kambo

Mbeya: Watoto wamchoma moto mama wa kambo

Mocumentary

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
857
Reaction score
2,241
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili

1. EZEKIA LIZER [20] 2. BARAKA EZEKIA [24] wote wakazi wa Tarafani Mji Mdogo wa Mbalizi kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kutumia moto DAINES ROBERT MDEE [26] Mkazi wa ZZK ambaye ni Mama yao wa kambo kutokana na mgogoro wa mali za familia.

Tukio hili limetokea mnamo tarehe 18.10.2020 majira ya saa 06:00 asubuhi huko eneo la ZZK

– Mbalizi, Kata ya Utengule Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. Ni kwamba chanzo cha tukio hili ni mgogoro wa mali za familia zilizoachwa na mume wa mhanga baada yakufariki dunia hivyo watoto wa marehemu [watuhumiwa] kumtuhumu mhanga kutumia hati za nyumba za marehemu Baba yao kukopea pesa Benki kiasi cha Tshs.Milioni 40 na baadae kuondoka na kuacha Benki ikitaka kuuza nyumba hizo.

Kutokana na kitendo hicho, watuhumiwa walimvizia mama yao wa kambo wakati anaenda kufungua duka kisha kummwagia mafuta ya Petroli ujazo wa lita 10 yaliyokuwa kwenye ndoo na kisha kumchoma moto kwa kutumia kiberiti.

Mhanga amelazwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matabibu. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

​

Chanzo: Global Tv online
 
Watu washajichokea na maisha hayaa na wewe unataka kuwachosha aisee Pole lakini mamdogo.

Let's meet at the top, cheers 🍻
 
Mzee wangu tulitofautiana hivihivi kwa sababu za kikuda kama hizi. Mpaka leo sijui kwake ni wapi na mara ya mwisho tunawasiliana ni pale nilipokuwa admitted chuo mwaka jana. Sasa ona hawa wanaenda kusota kisa matofali na michanga iliyosimamishwa kwenye mawe.

Huyo danga nae ana tamaa alikuja kula mafao anaona wanamkata matumaini. Ukute kahusika kuchangia kifo kisaikolojia, haiwezekani uweke bond nyumba ili iuzwe uikose.
 
Hakuna mama wa kambo hapo wote ni watoto wa marhemu. Wana umri sawa! Pole yao hao boys, maisha yashaharibika tayari!
Mkuu mawazo yako hayo ni hatari sana.

Tena unatakiwa kufanyiwa brain wash ili kukuondolea makandokando yaliyopo kichwani mwako.

Ina maana 'title' ya mtu inaendana na umri, are you serious?

Ungelikuwa kwenye majeshi ungelipata tabu sana, maana kijana mdogo makamo ya mwanao ndiyo boss wako anayetakiwa umnyenyekee ukiwa attension wakati ukimpigia saluti!

Labda nikuulize, babako akioa kasichana kadogi unakokazidi umri hauwezi kukaita 'mama' kwa unyenyekevu?
 
Mkuu mawazo yako hayo ni hatari sana.

Tena unatakiwa kufanyiwa brain wash ili kukuondolea makandokando yaliyopo kichwani mwako....
Hahahahaha.......kwa kweli sijui kama nitamwita. Ila haya mambo ni magumu, marhemu mzee Mengi alivutaga Kyline mwenye umri sawa na watoto wake wa mke mkubwa!

Mara nyingi baba akioa kabinti mwenye umri sawa na watoto wake anakosa heshima kutoka kwa watoto na kwa jamii kwa ujumla! Watoto wakishakuwa wakubwa, usioe tena lkn kula maisha polpole na masimbe.
 
Mzee wangu tulitofautiana hivihivi kwa sababu za kikuda kama hizi. Mpaka leo sijui kwake ni wapi na mara ya mwisho tunawasiliana ni pale nilipokuwa admitted chuo mwaka jana. Sasa ona hawa wanaenda kusota kisa matofali na michanga iliyosimamishwa kwenye mawe.

Huyo danga nae ana tamaa alikuja kula mafao anaona wanamkata matumaini. Ukute kahusika kuchangia kifo kisaikolojia, haiwezekani uweke bond nyumba ili iuzwe uikose.
Sasa unaona sifa kukunjiana na mzazi wako?
 
Marehemu alikua na Moto. Ana kijana wa miaka 24 huku ana mchepuko wa miaka 26.

Huyu mdada achunguzwe. Utaolewaje na mzee mwenye watoto unao lingana nao? Shame
 
Wazee tuwe tunacheki mama wadogo wa kuwaleta kitaaa sasa maza gani huyo wanalingana nae ndio mana heshima hakuna wanamuona mdangaji kafata mali sidhani kama mama mdogo angekua na miaka 43 wangefanya hvo hao madogo dah

Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
 
Huyo mama na watoto mbona sawa Aisee. Pole ziwafikie
 
Tukio limetokea saa 6.00 asubuhi! Wa Tz tubadilike!
 
Sasa unaona sifa kukunjiana na mzazi wako?
"Kukunjiana" maana yake nini. Wewe kipi bora kati ya staying away vs. behind bars kama hawa wanakoelekea.

Unatakiwa uache usumbufu kwa watu wasiohitaji wala kujari uwepo wako, tofauti na hapo unawakera na kujihuzunisha.
 
Kukasirikiana na mzazi wako unaona sifa?
 
Back
Top Bottom