MBEYA: Rais Magufuli ahutubia wananchi Uwanja wa Ruanda Nzovwe. Agusia usajili wa laini na machinga

RECEIPT

JF-Expert Member
Nov 6, 2013
284
198
Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh Magufuli atazungumza na Watanzania mapema leo.

UPDATES

Hotuba ya Rais Magufuli

Kuhusu usajuli wa laini, Watanzania wapo milion 55 lakini waliosajiliwa NIDA ni million 15 tu.Hivyo tangazo la TCRA kuwa mwisho tarehe 1 mwezi wa tano itapelekea watanzania zaidi ya milioni 25 kukosa haki ya kumiliki mawasiliano.

Naongeza muda mpaka tarehe 31 Desemba, hata hivyo muda utakuwa mwisho endapo usajili wa vitambulisho utakuwa umekidhi vigezo.Kama usajili haujakamilika watu waendelee kumiliki simu zao mpaka NIDA watakapokamilisha usajili wa vitambulisho.

Kuhusu wamachinga, nwaagiza viongozi wa mkoa wa Mbeya kuandaa eneo la Uwanja wa Ndege wenye zaidi ya hekta 5 ili kuwa eneo la wamachinga.

Pia kama kutakuwa na eneo linalobakia wameagizwa kujenga soko la dhahabu huku, kujengwe vyoo pamoja na sehemu ya kupaki magari.

Baada ya wamachinga kuhamia eneo hilo na kuanza kufanya biashara wasidaiwe ushuru hasa pale wanapokuwa wamevaa vitambulisho shingoni.

Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Chadema Jimbo la Mbeya Mjini
Sio kwamba hatukuungi mkono kwa Kila jambo, kuna mambo mengi sana tunakuunga mkono lakini hawasemi. Kwenye suala la Wamachinga nakuunga sana mkono.
 
Mapema asubuhi ni saa ngapi, kuanzia saa moja mpaka saa 2 au?
 
Hao raia vipi tena,biashara zao ama kilimo watafanya saa ngapi,Ama posho zimeshatembea tayari
 
Hivi haya majitu yanayovaa sare za kijan hayana nguo zingine?huu sio mkutano wa ccm Bali ni wa raisi na wananchi wake iweje wavae majez yao je na chadema wakiamua kuvaa jez zao kwa hapo mbeya najua fika ccm hawatatosha kulinganisha na watakaovaa jez za chadema ifike kipindi raisi apige marufuku hawa kenge wanaojipendekeza kila mahal
 
Jiongezeni hizo sare mnazoziona wengi ni wanafunzi wa vyuo mbali mbali vinavyopatikana mbeya, wameamua kwenda kubeba wanafunzi vyuoni kujaza watu na kuonyesha mbeya ccm ipo juu, ukibahatika kuona picha angalia umri wa hao waliovaa sare wengi vijana chini ya miaka 30, kwaiyo kijana kama kahaidiwa pesa pengine shilingi elfu kumi kwanini asiende.

Pia mjiulize kwanini katika ziara zote mlizoona magufuri kafanya uko shinyanga, mwanza, Mara hakuona sare za ccm nyingi kama mbeya, maana mbeya tangy jana barabarani mnaona sare za ccm leo ndio balaa

Ombi tu kwa waratibu wa zoezi hilo siku nyingine msivalishe wanafunzi sare nyie ratibuni mpango wenu kimya kimya wanafunzi waje na nguo za nyumbani wao kwa wao wanajuana ambaye hatoenda hapati mgao wake wa elfu kumi kumi
 
Tuseme hoja zako za kweli...nini NIA na kwa matokeo gani. Najua unaruhusiwa KUFIKIRIA lakini shida inakuwa unapofikiri huku tayari uko limited by uchama.
 
Hivi haya majitu yanayovaa sare za kijan hayana nguo zingine?huu sio mkutano wa ccm Bali ni wa raisi na wananchi wake iweje wavae majez yao je na chadema wakiamua kuvaa jez zao kwa hapo mbeya najua fika ccm hawatatosha kulinganisha na watakaovaa jez za chadema ifike kipindi raisi apige marufuku hawa kenge wanaojipendekeza kila mahal

Mwanzoni rais aliwahi kuwaambia wanaccm waache kuvaa sare za ccm kwenye mikutano ya serikali, huenda ulikuwa ni ushauri wa mtu. Lakini wakaendelea kuvaa huku yeye akionyesha kabisa ccm ndio mpango mzima. Kwa maneno marahisi yeye ndio anataka aonyeshe wakati wa utawala wake ccm ndio ilikuwa na nguvu. Mtu ambaye sio mwanachama kwenda kwenye mikutano ya rais ni kwenda kulishwa uccm kwa gharama nafuu.
 
Habarini wakuu,, Niende kwenye mada ,

Teyari tumeshakusanyika katika viwanya vya Rwanda nzonzwe watu ni wengi sana,, Mheshimiwa ndo anaingia sasa tusubiri atasemaje .
 
Habarini wakuu,, Niende kwenye mada ,

Teyari tumeshakusanyika katika viwanya vya Rwanda nzonzwe watu ni wengi sana,, Mheshimiwa ndo anaingia sasa tusubiri atasemaje .
Mkuu upo uwanjani sehemu gani nikupokee simu, still itaonekana niwewe umepost
 
Habarini wakuu,, Niende kwenye mada ,

Teyari tumeshakusanyika katika viwanya vya Rwanda nzonzwe watu ni wengi sana,, Mheshimiwa ndo anaingia sasa tusubiri atasemaje .
Kuweni makini msimpige mawe kama JK, maana idadi ya mawe mtakayomtupia ni sawa na idadi ya miaka mtakayoswekwa ndani.
Asante.
 
Habarini wakuu,, Niende kwenye mada ,

Teyari tumeshakusanyika katika viwanya vya Rwanda nzonzwe watu ni wengi sana,, Mheshimiwa ndo anaingia sasa tusubiri atasemaje .
wakati unasubiri sikiliza hi halafu ukatulie home

Ondoka juani
 
Back
Top Bottom