Mbeya: Mwekezaji ajinyonga baada ya ng'ombe wake 50 kukamatwa na Maliasili, RC Chalamila acharuka asihusishwe

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,933
141,902
Mwekezaji mzawa katika sekta ya mifugo huko Ihefu mkoani Mbeya amekutwa amejinyonga kwenye mti porini baada ya ng'ombe wake 50 kukamatwa na askari wa Idara ya Maliasili.

Baba wa marehemu amesema mwanae amejinyonga kwa kuhofia ufukara na umaskini baada ya kunyang'anywa ng'ombe wake wote ambao wamehifadhiwa ofisi ya wilaya.

Naye mkuu wa mkoa wa Mbeya mh Chalamila amekiri kupata taarifa za tukio hilo na ametaka Serikali isihusishwe kwa namna yoyote ile na uamuzi wa mwekezaji huo kujinyonga kwani huo ni uamuzi wake binafsi hakuna aliyemshinikiza.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Serikali isihusishwe na kifo cha mwananchi wake?

Je, huyo jamaa angepata utajiri na kuuza mifugo mpaka nje na kuletea kodi taifa tusingeiongelea serikali ya awamu ya 5?

When you take credit for all good things, don't forget to take responsibility when they go wrong.
 
Back
Top Bottom